Mwananmuziki mkongwe wa Dansi nchini Tanzania Karama Regesu aliyekuwa bendi ya Msondo Ngoma ambae sasa yuko bendi ya Sikinde, alitoa ushauri kwa wanamuziki wa Tanzania kuhusu namna nzuri ya wasanii kulinda sauti zao kwa kutumia baadhi ya matunda na mbogamboga.
Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo beats kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Star Tv akihojiwa na mtangazaji Sauda Mwilima. Mwanamuziki huyo mkongwe alisema kwamba yeye ni mwanamuziki wa siku nyingi, kaanza sanaa ya muziki mwaka 1985 lakini bado sauti yake iko vilevile haijabadilika ingawaje umri wake umekwenda sana. "Mimi nimeanza muziki mwaka 1985 lakini bado sauti yangu iko palepale ingawaje nimezeeka" alisema Karama Regesu.
Mwanamuziki huyo alizungumzia baadhi ya matunda na mbogamboga ambazo zitawafanya wasanii wa muziki kuwa na sauti nzuri isiyo badilika muda mrefu huku akilaumu baadhi ya wasanii kunywa pombe kupita kiasi kabla ya shoo, na akatoa mfano wa wanamuziki P-square wa Nigeria.
Baada ya kuhojiwa na Mtangazaji Sauda Mwilima kuhusu ni namna gani yeye amekua na sauti nzuri tangu siku nyingi mpaka sasa, "Tupe siri ya sauti yako, kwa sababu umedumu na sauti hiyo nzuri tangu zamani mpaka sasa" aliuliza mtangazaji Sauda Mwailima.
Mwanamuziki Karama Regesu alijibu ifuatavyo " Ni kweli sauti yangu ni ileile tangu naanza muziki mwaka 1985 mpaka sasa, siri kubwa ni kwamba Mwanamuziki unatakiwa utambue aleji yako yani unatakiwa ujifanyie utafiti ni kitu gani ambacho ukitumia kitaathiri sauti yako. Mwingine akitumia pombe sauti inakata, mwingine pia akitumia vyakula vya mafuta sauti ina kua nzuri na mwingine inakata kabisa" alisema Karama Regesu.
Pia Mwanamuziki huyo mkongwe alienda mbali zaidi kuelezea baadhi ya matunda yanayoweza kutunza sauti kwa muda mrefu, "Naomba niwafundishe wasanii wachanga namna ya kuhifadhi sauti , kwasababu waliowengi walifundishwa namna ya kuimba tu lakini si kutunza sauti zao. Mimi huwa natumia Matango, Karoti na Ndizi, huwa nakula kabla ya kuimba. Kuna shoo moja ya P-square ilifanyika hapa Dar es salaam watu wakawa wanashangaa kuona P-square wanapiga shoo alafu wanaenda nyuma ya jukwaa na kula ndizi, mimi nikawambia sisi wakongwe ndo tunajua mambo haya nyie vijana hamjui, matunda haya ni mazuri sana kwa kutunza sauti. Unakuta msanii kabla ya shoo anakunywa pombe kupita kiasi na kufanya madudu mengine kiasi kwamba hawezi kufanya shoo kabisa. Kwa hiyo nawashauli wasanii wabadilike" alifafanua Karama Regesu.
Tazama video ifuatayo ikionyesha sehemu ndogo ya mahojiano hayo. (Video kwa hisani ya STAR TV) Coming soon....
Tazama wimbo wa Msondo Ngoma hapo chini, mtunzi Karama Regesu
Post a Comment