SEHEMU YA KWANZA
Ufugaji wa kuku wa mayai ni ufugaji wa kuku wa kisasa
wanaotaga mayai tu, mayai hayo ni kwa ajili ya kuliwa tu sio kuanguliwa, kwa
sababu hayajarutubushwa (Not-fertile) na dume (Jogoo). Kuku hawa wa mayai ni
aina pekee ya kuku ambao wanahitaji kulelewa kwanzia wakiwa vifaranga hadi
wakiwa wakubwa. Kuku hawa wanaanza kutaga mayai wakiwa na umri wa wiki 18 hadi
19 (Miezi 41/2 hadi 5), Wataendelea kutaga mayai mfululizo mpaka watakapofikia
umri wa wiki 72 hadi 78 (Miezi 18 hdi 20). Kama unataka kuzalisha vifaranga kwa
ajili ya kupata kuku wa mayai, hakikisha unaangalia tabia za kuku jike na jogoo
kabla ya kuwakutanisha ili kupata mayai ya vifaranga. Kuna aina mbalimbali za
jamii za kuku wanaozalisha sana mayai, na wanapatikana Duniani kote.
AINA ZA KUKU WA MAYAI (LAYER BREEDS)
Kuku wa mayai wamegawanyika katika makundi makubwa mawili
kulingana na rangi ya mayai. Ufuatao ni mchanganuo wa makundi haya mawili;
1. Kuku wanaotaga mayai meupe (White Egg laying Hens)
Hawa ni aina ya kuku wa mayai wenye maumbile madogo, na
wanakula chakula kidogo pia wataga mayai madogo na yenye gamba jeupe. Zifuatazo
ni aina mbalimbali za kuku hawa ambao hufugwa sana na watu wengi;
- Isa White
Photo Credit: www.isa-poultry.com
- Lehman White / Lohmann White
- Nikchik
- Bab Cock BV-300
- Havard White
- Hi Sex White
- Sever White
- Hi line / Hyline White
Photo Credit: www.hyline.com
- Bovanch White
Photo Credit: www.bovans.com
2. Kuku wanaotaga mayai ya Kahawia
(Brown Egg Laying Hens)
Hawa ni kuku wa mayai wenye
maumbile makubwa, na wanakula chakula kingi zaidi ukiringanisha na kuku
wanaotaga mayai meupe. Wanataga mayai makubwa kuzidi kuku wengine wa mayai, Pia
mayai yao yanakua na gamba lenye rangi ya kahawia (Brown)
Zifuatazo ni aina mbalimbali za
kuku hawa ambao hufugwa sana na watu wengi;
- Isa Brown
Photo Credit: www.backyardchickencoops.com.au
- Hi Sex Brown
Photo Credit: www.hisex.com
- Sever 579
- Lehman Brown / Lohmann Brown
Photo Credit: www.hylinena.com
- Hi Line Brown
Photo Credit: www.hyline.com
- Bab Cock BV-380
- Gold Line / Bovans Goldline
- Bablona Tetro
- Bablona Harko
- Havard Brown n.k.
KUCHAGUA AINA YA KUKU WA MAYAI
(LAYER HEN SELECTION)
Kabla ya kuchagua aina ya kuku
unaotaka kufuga, hakikisha unakua na taarifa muhimu kuhusiana na tabia za hao
kuku ikiwemo kiwango kikubwa cha kutaga mayai. Zifuatazo ni tabia za kuku wanaofaa
katika uzalishaji wa mayai;
- Kwa ufugaji wa kuku wa mayai kibiashara, hakikisha unachagua aina kuku wanaotaga kiwango kikubwa cha mayai.
- Nunua vifaranga wenye afya njema, wanaotoka kwenye wazalishaji wenye uwezo na wanaozingatia taratibu zote za Uangulishaji bora.
KULEA VIFARANGA (KEEPING CHICKS)
Kabla ya kuwaleta vifaranga
nyumbani kwako hakikisha unafanya maandalizi yafuatayo;
- Hakikisha umeandaa sehemu maalumu ya kuwalea vifaranga (Brooder)
- Hakikisha una taa za kandili au balbu zinazotumia umeme au jiko la mkaa kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga.
- Hakikisha umeandaa matandazo ya kuweka kwenye sakafu kama maranda ya mbao,mapumba ya mpunga n.k. kwa ajili ya kuwapa joto
- Eneo la mita mraba 1 (1m2) hutosha vifaranga 20 hadi kufikia umri wa wiki 4
- Dhibiti joto bandani au sehemu maalum ya kuwalea vifaranga (Brooder) hadi kufikia nyuzijoto 35°C kwa vifaranga wa siku moja na nyuzi joto 24 - 27°C kwa vifaranga wenye umri wa wiki 1.
Kufahamu kama joto uliloweka
linawafaa vifaranga wako au lah, chunguza hali ifuatayo;
*Ukiona vifaranga wamekusanyika
pamoja kwa kuzunguka chanzo cha joto ina maana kwamba kuna kiasi kidogo sana
cha joto.
*Ukiona vifaranga wamekaa mbali
na chanzo cha joto, ina maana kuna kiwango kikubwa cha joto.
*Ukiona vifaranga wametawanyika
sehemu zote, ina maana kwamba joto lililopo linawafaa.
Punguza kiwango cha joto kadiri
vifaranga wanavyoendelea kukua.
MUHIMU
Wiki ya kwanza baada ya
kuanguliwa, vifaranga wengi huwa hawataki kunywa maji hii ni kwasababu ya
hekaheka za kuwasafirisha kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kwa hiyo inatakiwa
uweke maji ya kutosha kwenye eneo lao lililotengwa (Brooder), pia inatakiwa
uwafundishe kunywa maji. Changanya maji yao ya kunywa na Glukosi (5% Glucose)
ili wapate nguvu haraka. Pia Wapatie aina yoyote ya Multivitamin na uchanganye
na maji yao ya kunywa, Multivitamin hii husaidia sana kuku pale
wanaposafirishwa umbali mrefu, hupunguza Uchovu wa vifaranga na upungufu wa
maji na pia husaidia kuwafanya vifaranga warudi kwenye hali yao ya kawaida.
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Ni somo zuri asanteni
ReplyDeleteNtawezaje kupunguza joto kwenye banda wakati natumia bulb ua umeme?
ReplyDeleteNaomba msaada jmn mm nataka kuanza kufuga kuku wa mayai kuku miambili je? Niandae kiasi gan
ReplyDeleteNaitaji kuanza kufuga kuku mambo gani muhim yakuzingatia kuku wa mayai
ReplyDeletePost a Comment