Imehaririwa Tarehe: 30/10/2022
Kumaliza mapema (Premature ejaculation) wakati wa tendo la
ndoa ni tatizo linalowakumba wanaume wengi hivi sasa, Ingawaje dawa za aina
mbalimbali zimekua zikitumika kutibu tatizo hili imeonekana kwamba bado tatizo
hili linazidi kuongezeka kila kukicha. Tatizo hili limekua likichangiwa na
mambo mengi sana, ikiwemo yafuatayo;
- Mwenendo wa maisha wa hivi sasa yaani watu wengi wanakula vyakula visivyokua na virutubisho kamili.
- Matatizo ya kiafya ya muhusika
- Na sababu nyinginezo nyingi
Kama nivyokwishakusema hapo mwanzo kwamba sababu za tatizo
hili ziko nyingi sana, hivyo basi inatakiwa tusuruhishe swala hili kwa kutibu
mzizi wa tatizo.
Mbali na sababu za kiafya na zinginezo Mfumo wa uzazi wa mwanamume una misuli ya uume iliyoanzia
eneo la mifupa ya kiuno (Pelvic bone), misuli hiyo ndiyo kiini cha tatizo hili
(Kumaliza mapema). Nikupe mfano mmoja; Chukua picha ya watu wanaoinua vitu
vizito, watu hawa wanaongeza ukubwa wa misuli yao kwa kufanya mazoezi ya viungo.
Je, unaweza kuongeza ukubwa na ukakamavu wa misuli kwa kunywa dawa?? Lahasha ni
jambo lisilowezekana, bali kwa kufanya mazoezi ya viungo.
Kwa kutumia mfano wa hapo juu nikurudishe kwenye kipengele
cha misuli ya uume, Misuli ya uume haina tofauti na misuli mingine ya mwili,
mfumo wake ni uleule. Tatizo la wanaume wengi kumaliza mapema inasababishwa na
kusinyaa kwa misuli hiyo (Pelvic muscle). Tazama picha hapo chini inayoonyesha
misuli hiyo;
Misuli ya uume ikiimalika Mwanaume hamalizi mapema pia
anakua na uwezo wa kusimamisha vizuri uume wake na unakua kakamavu sio legevu.
JINSI YA KUITAMBUA MISULI YA UUME (PELVIC FLOOR MUSCLE)
Misuli hii ya uume (Pelvic floor muscle) ipo mwanzoni kabisa
mwa shina la misuli ya uume. Namna ya kuitambua misuli hii fanya ifuatavyo;
Nikuulize swali moja kidogo, Umeshawahi kubana mkojo?? Pengine
upo maeneo ya hafla, darasani, ofisini, mpirani, kwenye gari ama safarini au
sehemu ambayo unataka usipitwe na mada inayozungumziwa. Katika mazingira haya
watu wengi wanajikuta wakibana mkojo kwa muda Fulani ili wamalizie uhondo wa
mada Fulani au tukio fuani pengine yupo safarini na anajitahidi abane mkojo ili
akojoe atakapofika.
Au ukiwa unakojoa maeneo Fulani yasiyo rasmi, pengine
wakapita maofisa polisi ama migambo unajikuta unakatisha mkojo, Hivyo basi ile
hali ya kubana au kukatisha mkojo unatumia misuli hiyo ya uume (Pelvic muscle), ndio
breki ya mkojo.
Misuli hii ya uume ipo chini ya maungo ya mapaja katikati ya
korodani na sehemu ya haja kubwa, mara nyingi sehemu hii ukiguswa au kutomaswa
kwa kidole utaona uume unashtuka. Uuume unashtuka Zaidi ukiwa umesimama.
Ndio maana wale watu wanaoingiliwa kinyume cha maumbile (Mashoga) wanaharibiwa misuli hii baadae mtu huyu (Shoga) anakuwa hana uwezo wa kusimamisha uume. Hivyo basi misuli hii ina kazi kubwa sana ya kuimarisha ukakamavu wa uume wako.
Hivyo basi misuli hii (Pelvic floor muscle) ndiyo inayotakiwa
ifanyiwe mazoezi, sehemu hii ikiwa kakamavu uume unasimama vizuri na utaacha
kumaliza mapema (Premature ejaculation).
NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA MISULI YA UUME (PELVIC FLOOR MUSCLE EXERCISE/KEGEL EXERCISES)
Kama nilivyoeleza mwanzoni kwamba kiini cha mazoezi haya ni
misuli ya uume, Hivyo ile hali ya kubana mkojo ndio zoezi lenyewe. Sio kwamba
ubane mkojo, Lahasha inatakiwa uwe kama unabana mkojo wakati huna hamu ya kukojoa. Fanya hivyo kwa nguvu kwa sekunde 3 alafu utaachia, pia utafanya tena kwa
sekunde 3, Vilevile utaachia tena afu utafanya tena. Unaweza kuendelea hadi
sekunde 5, 10 na 30 kadiri utakavyokua unaweza. Fanya zoezi hili wakati wowote uupendao haijalishi uume umelala au umesimama, Pia ukifanya zoezi hili wakati uume wako umesimama itakua bora zaidi na misuri yako itakazika vizuri.
Utaratibu mzuri wa kufanya zoezi hili kwa seti
Hii pia ni njia nzuri ya kubana misuli hii kwa mpangilio maalumu, utaratibu huu huleta matokeo mazuri kwa haraka zaidi tofauti na kufanya kawaida, utafanya mazoezi haya muda wowote ukiwa umekaa, umesimama, umelala au umeinama. Namna ya kufanya zoezi hili ni kama ifuatavyo:
Kila seti ina mibinyo kumi (10)
Seti ya Kwanza: Fanya mbinyo kwa nguvu kwa sekunde 3 alafu achia, endelea hivyo mara 10 kukamilisha seti ya kwanza
Seti ya Pili: Fanya mbinyo kwa nguvu sekunde 3 alafu achia, endelea hivyo mara 10 kukamilisha seti ya pili
Seti ya Tatu.... na kuendelea kwa Siku kulingana na utakavyozoea, idadi ya sekunde za kubinya utaendelea kuziongeza kadri utakavyoendelea kuzoea yaani; Sekunde 3, 5, 10, 15 hadi 30.
Kwa siku unaweza kufanya zaidi ya seti 10.....sawa na mibinyo zaidi ya 50
Uendelee na zoezi hilo mara nyingi kadri uwezavyo, ukizoea
utaweza kufanya zoezi hili kwa muda mrefu zaidi na sehemu yoyote ukiwa unatembea, ukiwa umekaa, kwenye
gari na sehemu yoyote ile. Uzuri wa zoezi hili unaweza kufanya sehemu yoyote
pasipo watu kujua.
NB:
Matokeo ya zoezi hili yanaanza kuonekana baada ya
wiki 2-3 inategemea na mtu mwenyewe. Ukishapata matokeo mazuri usiache uendelee
tu iwe ni kama sehemu ya maisha yako. Kwa mfano watu wanonyenyua vitu vizito
wanakuza misuli yao na kua mabaunsa, lakini wakiacha mazoezi wanabadilika
wanakua wazembe ama manyama uzembe. Vilevile kwa upande wa misuli ya uume, jitahidi
kufanya mazoezi haya mara kwa mara ili kuikaza misuli ya uume wako. Kwa kuanzia
unaweza kufanya mara 3 kwa siku, pindi ukizoea unaweza kufanya mara nyingi
kadiri uwezavyo.
CHANZO: MTANDAO WA INTANETI
>>>Toa maoni yako hapo chini tushirikishane
Mkuu hongera sana na makala nzuri za kuelimisha....
ReplyDeleteKazi ya Kisusange Iyunga..Big up
Shukrani sana ndugu, Japo umeposti kama Anonymous, Asante sana kwa response yako. Dah umenikumbusha pande za Iyunga Sec, enzi za Headmaster Kisusange, kweli siku hazigandi jamani!!. Shukrani sana ndugu, endelea kunifuatilia..Naandaa makala nyingine nyingi na nzuri kwa ajili yenu!.
DeleteMJASIRIAMALI HODARI ADMIN
Tunashukuru kwa elimu Nzuri, ila nina swali hapo unasema unabana misuli je unabana moja kwa moja kwa hizo sekundi au unatakiwa kubana na kuachia kwa muda huo?
ReplyDeleteAsante sana kwa kutembelea blogi yangu, Unachofanya hapo, unabana kwa nguvu kwa muda fulani alafu unaachia, unaweza ukabana sekunde 10, 15, au 30 na zaidi kulingana na ulivyozoea, ukibana kwa muda uliozoea unaachia alafu unabana tena alafu unaachia..UTAFANYA HIVYO MARA KADHAA KADRI UWEZAVYO. Pia sio kwamba unafanya siku nzima na kila wakati, unaweza ukateua masaa uyapendayo kufanya zoezi hili.
DeleteAsante sana kwa maoni yako.
LUSUBILO A. MWAIJENGO
(MJASIRIAMALI HODARI ADMIN)
Hongera sana Kaka kwa kupata kipaji cha kuelimisha. Mimi nina swali moja. Je hili zoezi huwa lina imarisha misuli ya Uume tu au nakukuza? Au ni kuimarisha tuu pekee???
ReplyDeleteNashukuru ndugu, Hili zoezi linafanya mambo yote mawili kwa wakati mmoja yaani linaimarisha misuli na kukuza uume pia. Hii ina maana kwamba ukiimarisha misuli ya uume, uume utakuwa unasimama vizuri kwa nguvu nyingi, kwa hiyo uume ukiwa unasimama vizuri kutakuwa na mgandamizo mkubwa wa damu (pressure kubwa) kuelekea eneo la mbele la uume(kichwa cha uume). Mgandamizo huo wa damu hupeleka virutubisho vya chakula na Oksijeni kwenye misuli ya uume, pia husukuma kichwa cha uume kuelekea mbele zaidi, hii ndio inaleta matokeo ya kukuza uume pia (kukuza urefu na unene). Matokeo ya kukuza uume huwa ya taratibu na ya muda mrefu kidogo lakini manufaa yake ni ya muda mrefu na hakuna madhara yoyote.
DeleteNashukuru kwa swali lako zuri!, Nadhani hili swali litawapa faida na wengine.
Karibu sana kwenye blogi yangu!
LUSUBILO A. MWAIJENGO
(MJASIRIAMALI HODARI ADMIN)
Je nikiwa nafanya zoezi LA kuubinya uume kwa mda wa wiki 1 to 2 kuna madhara
ReplyDeleteWana sema vitunguu swaumu, asali na kitunguu vina, tibubuume usio simama je nikweli kama nikweli nikwa muda gani mtubhuyu ana kuwa nanguzu kama mwanzo
ReplyDeleteApana Mr
DeleteHongera sana kaka kwa ushauri wako
ReplyDeleteIla mmi ninaswali hivi usipofanya tendo la ndoa mda mrefu ninaweza KUPATA tatizo gani la uume.? Afu mpenzi wangu anasema hataki kufnya tendo hilo mpka tufunge ndoa je ni nifanyaje mpk nisipata tatizo la uume wangu kutokuchoka maan kila siku nikiamka naona uume wangu hausimami kila asubhi sas sijui nimeishiwa nguvu za kiume kwa kutokushiriki tendo
It is okey
ReplyDeleteMi kuanzia leo nafanya zowez hlo
ReplyDeletePost a Comment