Imarisha misuli ya uume wako na kupunguza tatizo la kumaliza mapema kwa kutumia mazoezi madogo tu (Improve your Penis erection by simple exercise)


Imehaririwa Tarehe: 30/10/2022

Kumaliza mapema (Premature ejaculation) wakati wa tendo la ndoa ni tatizo linalowakumba wanaume wengi hivi sasa, Ingawaje dawa za aina mbalimbali zimekua zikitumika kutibu tatizo hili imeonekana kwamba bado tatizo hili linazidi kuongezeka kila kukicha. Tatizo hili limekua likichangiwa na mambo mengi sana, ikiwemo yafuatayo;
  • Mwenendo wa maisha wa hivi sasa yaani watu wengi wanakula vyakula visivyokua na virutubisho kamili.
  • Matatizo ya kiafya ya muhusika
  • Na sababu nyinginezo nyingi
Kama nivyokwishakusema hapo mwanzo kwamba sababu za tatizo hili ziko nyingi sana, hivyo basi inatakiwa tusuruhishe swala hili kwa kutibu mzizi wa tatizo. 

Mbali na sababu za kiafya na zinginezo Mfumo wa uzazi wa mwanamume una misuli ya uume iliyoanzia eneo la mifupa ya kiuno (Pelvic bone), misuli hiyo ndiyo kiini cha tatizo hili (Kumaliza mapema). Nikupe mfano mmoja; Chukua picha ya watu wanaoinua vitu vizito, watu hawa wanaongeza ukubwa wa misuli yao kwa kufanya mazoezi ya viungo. Je, unaweza kuongeza ukubwa na ukakamavu wa misuli kwa kunywa dawa?? Lahasha ni jambo lisilowezekana, bali kwa kufanya mazoezi ya viungo.

Kwa kutumia mfano wa hapo juu nikurudishe kwenye kipengele cha misuli ya uume, Misuli ya uume haina tofauti na misuli mingine ya mwili, mfumo wake ni uleule. Tatizo la wanaume wengi kumaliza mapema inasababishwa na kusinyaa kwa misuli hiyo (Pelvic muscle). Tazama picha hapo chini inayoonyesha misuli hiyo;



Misuli ya uume ikiimalika Mwanaume hamalizi mapema pia anakua na uwezo wa kusimamisha vizuri uume wake na unakua kakamavu sio legevu.

JINSI YA KUITAMBUA MISULI YA UUME (PELVIC FLOOR MUSCLE)
Misuli hii ya uume (Pelvic floor muscle) ipo mwanzoni kabisa mwa shina la misuli ya uume. Namna ya kuitambua misuli hii fanya ifuatavyo;

Nikuulize swali moja kidogo, Umeshawahi kubana mkojo?? Pengine upo maeneo ya hafla, darasani, ofisini, mpirani, kwenye gari ama safarini au sehemu ambayo unataka usipitwe na mada inayozungumziwa. Katika mazingira haya watu wengi wanajikuta wakibana mkojo kwa muda Fulani ili wamalizie uhondo wa mada Fulani au tukio fuani pengine yupo safarini na anajitahidi abane mkojo ili akojoe atakapofika.

Au ukiwa unakojoa maeneo Fulani yasiyo rasmi, pengine wakapita maofisa polisi ama migambo unajikuta unakatisha mkojo, Hivyo basi ile hali ya kubana au kukatisha mkojo unatumia misuli hiyo ya uume (Pelvic muscle), ndio breki ya mkojo.

Misuli hii ya uume ipo chini ya maungo ya mapaja katikati ya korodani na sehemu ya haja kubwa, mara nyingi sehemu hii ukiguswa au kutomaswa kwa kidole utaona uume unashtuka. Uuume unashtuka Zaidi ukiwa umesimama. 

Ndio maana wale watu wanaoingiliwa kinyume cha maumbile (Mashoga) wanaharibiwa misuli hii baadae mtu huyu (Shoga) anakuwa hana uwezo wa kusimamisha uume. Hivyo basi misuli hii ina kazi kubwa sana ya kuimarisha ukakamavu wa uume wako.

Hivyo basi misuli hii (Pelvic floor muscle) ndiyo inayotakiwa ifanyiwe mazoezi, sehemu hii ikiwa kakamavu uume unasimama vizuri na utaacha kumaliza mapema (Premature ejaculation).


NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA MISULI YA UUME (PELVIC FLOOR MUSCLE EXERCISE/KEGEL EXERCISES)
Kama nilivyoeleza mwanzoni kwamba kiini cha mazoezi haya ni misuli ya uume, Hivyo ile hali ya kubana mkojo ndio zoezi lenyewe. Sio kwamba ubane mkojo, Lahasha inatakiwa uwe kama unabana mkojo wakati huna hamu ya kukojoa. Fanya hivyo kwa nguvu kwa sekunde 3 alafu utaachia, pia utafanya tena kwa sekunde 3, Vilevile utaachia tena afu utafanya tena. Unaweza kuendelea hadi sekunde 5, 10 na 30 kadiri utakavyokua unaweza. Fanya zoezi hili wakati wowote uupendao haijalishi uume umelala au umesimama, Pia ukifanya zoezi hili wakati uume wako umesimama itakua bora zaidi na misuri yako itakazika vizuri.

Utaratibu mzuri wa kufanya zoezi hili kwa seti
Hii pia ni njia nzuri ya kubana misuli hii kwa mpangilio maalumu, utaratibu huu huleta matokeo mazuri kwa haraka zaidi tofauti na kufanya kawaida, utafanya mazoezi haya muda wowote ukiwa umekaa, umesimama, umelala au umeinama. Namna ya kufanya zoezi hili ni kama ifuatavyo:

Kila seti ina mibinyo kumi (10)

Seti ya Kwanza: Fanya mbinyo kwa nguvu kwa sekunde 3 alafu achia, endelea hivyo mara 10 kukamilisha seti ya kwanza

Seti ya Pili: Fanya mbinyo kwa nguvu sekunde 3 alafu achia, endelea hivyo mara 10 kukamilisha seti ya pili

Seti ya Tatu.... na kuendelea kwa Siku kulingana na utakavyozoea, idadi ya sekunde za kubinya utaendelea kuziongeza kadri utakavyoendelea kuzoea yaani; Sekunde 3, 5, 10, 15 hadi 30.

Kwa siku unaweza kufanya zaidi ya seti 10.....sawa na mibinyo zaidi ya 50

Uendelee na zoezi hilo mara nyingi kadri uwezavyo, ukizoea utaweza kufanya zoezi hili kwa muda mrefu zaidi na sehemu yoyote ukiwa unatembea, ukiwa umekaa, kwenye gari na sehemu yoyote ile. Uzuri wa zoezi hili unaweza kufanya sehemu yoyote pasipo watu kujua.

NB:
Matokeo ya zoezi hili yanaanza kuonekana baada ya wiki 2-3 inategemea na mtu mwenyewe. Ukishapata matokeo mazuri usiache uendelee tu iwe ni kama sehemu ya maisha yako. Kwa mfano watu wanonyenyua vitu vizito wanakuza misuli yao na kua mabaunsa, lakini wakiacha mazoezi wanabadilika wanakua wazembe ama manyama uzembe. Vilevile kwa upande wa misuli ya uume, jitahidi kufanya mazoezi haya mara kwa mara ili kuikaza misuli ya uume wako. Kwa kuanzia unaweza kufanya mara 3 kwa siku, pindi ukizoea unaweza kufanya mara nyingi kadiri uwezavyo.

CHANZO: MTANDAO WA INTANETI

>>>Toa maoni yako hapo chini tushirikishane


Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

12 تعليقات

  1. Mkuu hongera sana na makala nzuri za kuelimisha....
    Kazi ya Kisusange Iyunga..Big up

    ردحذف
    الردود
    1. Shukrani sana ndugu, Japo umeposti kama Anonymous, Asante sana kwa response yako. Dah umenikumbusha pande za Iyunga Sec, enzi za Headmaster Kisusange, kweli siku hazigandi jamani!!. Shukrani sana ndugu, endelea kunifuatilia..Naandaa makala nyingine nyingi na nzuri kwa ajili yenu!.

      MJASIRIAMALI HODARI ADMIN

      حذف
  2. Tunashukuru kwa elimu Nzuri, ila nina swali hapo unasema unabana misuli je unabana moja kwa moja kwa hizo sekundi au unatakiwa kubana na kuachia kwa muda huo?

    ردحذف
    الردود
    1. Asante sana kwa kutembelea blogi yangu, Unachofanya hapo, unabana kwa nguvu kwa muda fulani alafu unaachia, unaweza ukabana sekunde 10, 15, au 30 na zaidi kulingana na ulivyozoea, ukibana kwa muda uliozoea unaachia alafu unabana tena alafu unaachia..UTAFANYA HIVYO MARA KADHAA KADRI UWEZAVYO. Pia sio kwamba unafanya siku nzima na kila wakati, unaweza ukateua masaa uyapendayo kufanya zoezi hili.

      Asante sana kwa maoni yako.

      LUSUBILO A. MWAIJENGO
      (MJASIRIAMALI HODARI ADMIN)

      حذف
  3. Hongera sana Kaka kwa kupata kipaji cha kuelimisha. Mimi nina swali moja. Je hili zoezi huwa lina imarisha misuli ya Uume tu au nakukuza? Au ni kuimarisha tuu pekee???

    ردحذف
    الردود
    1. Nashukuru ndugu, Hili zoezi linafanya mambo yote mawili kwa wakati mmoja yaani linaimarisha misuli na kukuza uume pia. Hii ina maana kwamba ukiimarisha misuli ya uume, uume utakuwa unasimama vizuri kwa nguvu nyingi, kwa hiyo uume ukiwa unasimama vizuri kutakuwa na mgandamizo mkubwa wa damu (pressure kubwa) kuelekea eneo la mbele la uume(kichwa cha uume). Mgandamizo huo wa damu hupeleka virutubisho vya chakula na Oksijeni kwenye misuli ya uume, pia husukuma kichwa cha uume kuelekea mbele zaidi, hii ndio inaleta matokeo ya kukuza uume pia (kukuza urefu na unene). Matokeo ya kukuza uume huwa ya taratibu na ya muda mrefu kidogo lakini manufaa yake ni ya muda mrefu na hakuna madhara yoyote.

      Nashukuru kwa swali lako zuri!, Nadhani hili swali litawapa faida na wengine.

      Karibu sana kwenye blogi yangu!

      LUSUBILO A. MWAIJENGO
      (MJASIRIAMALI HODARI ADMIN)

      حذف
  4. Je nikiwa nafanya zoezi LA kuubinya uume kwa mda wa wiki 1 to 2 kuna madhara

    ردحذف
  5. Wana sema vitunguu swaumu, asali na kitunguu vina, tibubuume usio simama je nikweli kama nikweli nikwa muda gani mtubhuyu ana kuwa nanguzu kama mwanzo

    ردحذف
  6. Hongera sana kaka kwa ushauri wako

    Ila mmi ninaswali hivi usipofanya tendo la ndoa mda mrefu ninaweza KUPATA tatizo gani la uume.? Afu mpenzi wangu anasema hataki kufnya tendo hilo mpka tufunge ndoa je ni nifanyaje mpk nisipata tatizo la uume wangu kutokuchoka maan kila siku nikiamka naona uume wangu hausimami kila asubhi sas sijui nimeishiwa nguvu za kiume kwa kutokushiriki tendo

    ردحذف
  7. Mi kuanzia leo nafanya zowez hlo

    ردحذف

إرسال تعليق

أحدث أقدم