Ufwatao ni mwenendo wa maisha
ambao una athari kubwa kwa ujauzito wako;
1. Kunywa Pombe
Mwanamke mjamzito hapaswi kunywa pombe. Unywaji wa pombe kwa
mjamzito husababisha mjamzito kujifungua kabla ya muda, kuzaa watoto njiti (low
birth weight babies), kuharibu mfumo wa ubongo au ufikiri wa mtoto na kuharibu
mfumo wa viungo vya mwili vya mtoto.
2. Kuzidisha kunywa vinywaji vya chai, Kahawa, Energy na
vyakula vya Chokoleti (chocolate)
Vinywaji vya Chai, kahawa, Energy
na vyakula vya Chokoleti vina kilevi aina ya Caffeine, Utafiti wa kisayansi
unasema kwamba kuzidisha sana kilevi cha Caffeine wakati wa ujauzito unaongeza
uwezekano mkubwa wa kuharibu ujauzito (miscarriage). Kwa hiyo inatakiwa
mjamzito apunguze matumizi ya vyakula hivi ili kunusuru ujauzito wake.
Inatakiwa mjamzito anywe si zaidi ya kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa
siku, pia kwa upande wa vinywaji vya Energy inatakiwa mjamzito anywe si zaidi
ya mls 250 kwa siku.
Picha: Chai ya rangi
Picha: Kahawa
Picha: Keki ya Chokoleti
3. Kula vyakula vya kupunguza
uzito
Mjamzito hapaswi kula vyakula vya
kupunguza uzito, kwani ulaji wa vyakula hivyo hata kwa muda mfupi huleta athari
kubwa kwa mtoto wako alie tumboni. Mjamzito pamoja na mtoto aliyetumboni
wanahitaji muendelezo wa virutubisho mbalimbali wakati wote wa ujauzito na
baada ya kujifungua. Kama nilivyokwisha kueleza kwenye makala ya kwanza
kuhusiana na Lishe kwa wajawazito, nilieleza kwamba Ongezeko la uzito kwa
mjamzito ni kiashiria tosha kinachoonyesha kwamba ujauzito una afya njema.
Ingawaje kwa upande mwingine vyakula vya kupunguza uzito havina virutubisho
muhimu vinavyotakiwa katika ukuaji na maendeleo ya mtoto aliyetumboni. Ongezeko
la uzito kwa mjamzito ni ishara ya ujauzito wenye afya njema, kwa hiyo mjamzito
asithubutu kupunguza uzito. Kusoma makala ya kwanza kuhusu "Lishe bora kwa wajawazito" Bofya hapa
Picha: Hivi ni baadhi tu ya vyakula vya kupunguza uzito, vitamfanya mjamzito ajisikie ameshiba wakati virutubisho vilivyopo ni kidogo sana vina uwingi wa maji, nyuzinyuzi (fiber) nyingi na vitamini ambazo bado hazitoshi kwa ukuaji wa mtoto. Hivi ni vyakula vya ziada kwa mjamzito.
Picha: Hivi ni baadhi tu ya vyakula vya kupunguza uzito, vitamfanya mjamzito ajisikie ameshiba wakati virutubisho vilivyopo ni kidogo sana vina uwingi wa maji, nyuzinyuzi (fiber) nyingi na vitamini ambazo bado hazitoshi kwa ukuaji wa mtoto. Hivi ni vyakula vya ziada kwa mjamzito.
4. Kutumia dawa za matibabu pasipo kuruhusiwa na wataalamu
wa afya.
Mjamzito haruhusiwi kutumia dawa
zozote zile za matibabu pasipo kuruhusiwa na daktari, Kwa sababu dawa hizo
huweza kuleta shida kwenye ujauzito ikiwa ni pamoja na kutoa ujauzito, shida ya
kujifungua na madhara kwa mtoto aliyetumboni.
Photo Credit: www.tervepotilas.fi
5. Kutumia madawa ya kulevya
Mjamzito haruhusiwi kutumia madawa ya kulevya ya aina yoyote
ile kama Unga (Cocaine, Heroine na nyinginezo) na bangi. Madawa hayo hupita kwa
urahisi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kuathiri ukuaji wa mtoto, vilevile
dawa hizo husababisha mjamzito kujifungua kabla ya muda, kujifungua watoto
njiti, mtoto kufia tumboni, watoto kufariki ghafra baada ya kuzaliwa kuanzia
siku 0 hadi miezi 6 pia hadi kufikia miaka miwili.
Picha: Dawa za kulevya aina Cocaine /Heroin Photo Credit: www.patch.com
6. Kuvuta sigara au bidhaa zingine za Tumbaku au kutafuna
Tumbaku
Uvutaji wa sigara au bidhaa zingine za tumbaku au kutafuna
Tumbaku ni hatari sana kwa afya ya mjamzito pamoja na mtoto, kwa hiyo mjamzito
haruhusiwi kutumia bidhaa hizo. Moshi wa sigara huzuia damu isifike kwa mtoto
kwa hali hiyo huzuia hewa safi ya Oksijeni, virutubisho kufika kwa mtoto pia
huzuia uchafu kutoka kwa mtoto kwenda nje ya mfuko wa mtoto. Hali hii huweza
kusababisha kifo cha mtoto akiwa tumboni. Vilevile uvutaji wa sigara
husababisha kuzaliwa watoto njiti, pia huharibu mfumo wa ukuaji wa mapafu ya
mtoto na huongeza atari ya kusababisha madhara ya mfumo wa upumuaji na kupata
ugonjwa wa pumu kwa mtoto (Asthma) mara atakapozaliwa.
*Kusoma makala ya kwanza kuhusu "Lishe bora kwa wajawazito" Bofya hapa
*Kufahamu matatizo madogo madogo kwa wajawazito yatokanayo na chakula Bofya hapa
*Kufahamu matatizo madogo madogo kwa wajawazito yatokanayo na chakula Bofya hapa
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
إرسال تعليق