Lishe bora wakati wa ujauzito ni
muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto akiwa tumboni. Wakati wa ujauzito ni muhimu kwa
mama kula vyalula vyenye lishe kamili (Balanced diet) ili kumpa mtoto aliye
tumboni makuzi bora.
Wakati wa ujauzito, mwili wa
mjamzito huongeza uwezo wa kufyonza virutubisho kwenye chakula isivyo kawaida.
Kwa hiyo kula vyakula mbalimbali vyenye virutubisho kutampa mtoto wako
aliyetumboni virutubisho kamili.
ONGEZEKO LA UZITO WAKATI WA
UJAUZITO
Wakati wa Ujauzito mwili wa
mjamzito hupitia mabadiliko mbalimbali na Ongezeko la uzito ni miongoni mwa
mabadiliko hayo. Ongezeko la uzito kwa mjamzito ni uthibitisho tosha
unaoashiria Ujauzito wenye afya njema. Mjamzito anapokula chakula vizuri na
anapoongezeka uzito unaofaa, husaidia kumlinda njamzito na Afya ya mtoto aliye
tumboni.
Ni kiasi gani cha uzito kinatakiwa, itategemeana na uzito
ulionao kabla haujapata ujauzito. Ongezeko la uzito linalotakiwa kwa mwanamke
mjamzito aliyepata ujauzito akiwa na uzito wa afya njema na aliyebeba mtoto
mmoja ni kuanzia Kilo 11 hadi 16.
Na mwanamke mwenye uzito wa chini (Underweight) akipata
ujauzito, Ongezeko la uzito linalotakiwa ni kuanzia Kilo 13 hadi 18.
Pia mwanamke mwenye uzito mkubwa (Overweight) akipata
ujauzito, Ongezeko la uzito linalotakiwa ni kuanzia Kilo 7 hadi 11.
MCHANGANUO WA ONGEZEKO LA UZITO
(WEIGHT GAIN PATTERN)
A. Wanawake wenye uzito wa kawaida
(Normal weight women)
Kwa wanawake wenye uzito wa kawaida, wanapopata ujauzito
wanatakiwa wawe na ongezeko la uzito kama ifuatavyo;
1. Miezi mitatu ya kwanza (First trimester)
- Ongezeko la Kilo 1.5 (1.5Kg)
2. Miezi mitatu ya pili (Second trimester)
- Ongezeko la Kilo 0.5 (0.5Kg) kwa wiki
3. Miezi mitatu ya mwisho (Third trimester)
- Ongezeko la kilo 0.5 (0.5Kg) kwa wiki.
*Kuanzia miezi mitatu ya kwanza hadi ya mwisho kunakua na
jumla ya ongezeko la Kilo 11 hadi 16.
B. Wanawake wenye uzito wa chini (Underweight women)
Kwa wanawake wenye uzito wa chini, inatakiwa wawe ongezeko
la Kilo 2 (2kg) kwa miezi mitatu ya kwanza na Ongezeko la Kilo 0.5 (0.5Kg) kwa
wiki kwa miezi mitatu ya pili na ya tatu. Kutakua na jumla ya ongezeko la kilo
13 hadi 18.
C. Wanawake wenye uzito mkubwa
(Overweight women)
Kwa wanawake wenye uzito mkubwa, inatakiwa wawe ongezeko
la Kilo 1 (1kg) kwa miezi mitatu ya kwanza na Ongezeko la Kilo 0.3 (0.3Kg) kwa
wiki kwa miezi mitatu ya pili na ya tatu. Kutakua na jumla ya ongezeko la kilo
7 hadi 11.
Ukipata uzito zaidi kuliko inavyotakiwa kwa kipindi cha
mwanzo cha ujauzito, usipunguze kula ili kupunguza uzito, Bali endelea kula
vyakula vitakavyo rekebisha uzito wako kama kula vyakula vyenye virutubisho
kamili au vyakula mchanganyiko (Balanced diet) kama vyakula vya protini + Wanga
+ Mboga na matunda + Madini + Mafuta + Maji n.k
MAMBO YANAYOTAKIWA ILI KUTENGENEZA
AFYA BORA YA MTOTO ALIYE TUMBONI
1. Furahia kula vyakula mbalimbali
Lishe bora humaanisha kula vyakula mbalimbali. Chakula cha
aina moja hakina virutubisho vyote vinavyotakiwa na mwili, isipokua maziwa ya
mama kwa mtoto hadi kufikia umri wa miezi sita. Kula vyakula mbalimbali
huongeza virutubisho mbalimbali kwenye mwili wa mama na mtoto. Kwa hiyo mama
afurahie kula vyakula mbalimbali vilivyopo kwenye mazingira yake kama vyakula
vya msimu na vinginevyo, kwani vyakula vinavyopatikana kwenye mazingira yake
huwa havina gharama na huweza kuvimudu kiuchumi.
2. Kula vyakula vya wanga
Vyakula vya nafaka vina wanga
(Carbohydrate) huupa mwili nguvu, madini ya chuma, vitamins B, ni chanzo kizuri
cha nyuzi nyuzi (Fiber), madini mengine mengi na kiasi kidogo cha protein. Mikate
iliyotengenezwa kwa nafaka kama ngano humsaidia mjamzito kupata vitamini aina
ya Folic acid, Folic acid ni muunganiko wa vitamin B za aina mbalimbali
(Vitamin B complex), Vitamin B hizi husaidia katika ukuaji na kuzaliana kwa
seli hai za mwili. Kwa hiyo humsaidia mtoto aliyetumboni kupata ukuaji mzuri na
afya njema.
3. Kula Mbogamboga na Matunda
Mbogamboga na matunda huupa mwili
vitamini na madini mbalimbali na nyuzinyuzi (Fibers) zinazosaidia kuongeza kasi
ya mmeng'enyo wa chakula. Vitamini C inayotokana na matunda na mbogamboga
mbalimbali husaidia mwili wako kufyonza madini ya chuma (Iron) na kufanya fidhi
ziwe na afya nzuri wakati wote kwako wewe mama na mtoto wako aliye tumboni, kwa
kuzuia kupata ugonjwa wa fidhi unaoitwa KISEYEYE. Ugonjwa huu husababisha fidhi
kutoa damu na mdomo wako kunuka wakati wote. Mboga za majani zenye ukijani zina
vitamini A, Madini ya chuma na madini muhimu sana kwa afya ya mjamzito.
Mbogamboga zinazopatikana kwa wingi nchini Tanzania ni pamoja na Kabeji, Sukuma
wiki, Spinachi, Majani ya maboga, majani ya maharage na mbogamboga za asili
kama mlenda, kisamvu n.k. Pia matunda yanayopatikana kwa wingi nchini Tanzania
ni pamoja na Machungwa, Maembe, Nanasi, Maepo, matikiti, Maparachichi,
Mapasheni, mapapai, ndizi n.k.
Photo Credit: www.huffingtonpost.com
Photo Credit: www.en.wikipedia.org
4. Kula vyakula vya protini
Protini ni muhimu sana kwa ukuaji
wa mtoto wako, hususani wakati wa miezi mitatu ya pili (Second trimester) na
miezi mitatu ya mwisho (Third trimester). Samaki ni chanzo kizuli cha protini
na vitamini aina ya Omega-3 fatty acids ambayo husaidia ukuaji mzuri wa ubongo
wa mtoto aliyetumboni.
[Wazazi wanaopenda watoto wao wawe
na akili nyingi darasani, na upana wa kufikili kwa ujumla, wahakikishe Mjamzito
anakula samaki sana hasa wabichi, pia mtoto akizaliwa akifikia umri wa kuanza
kula mpatie samaki na mchuzi wake hadi afikishe umri wa miaka mitano, pia
ukiweza mpatie vyakula vya ngano pamoja na samaki]
Pia mjamzito ale vyanzo vingine vya protini kama Protini
zitokanazo na mimea kama; Mimea jamii ya mikunde Maharage, soya n.k. Protini
inayotokana na wanyama kama Nyama ya ng'ombe au kuku, maziwa, mayai, Siagi n.k
5. Kunywa bidhaa za maziwa
Bidhaa za maziwa ya ng'ombe au ya
mbuzi kama maziwa freshi, maziwa mgando, Siagi, jibini n.k huwa na madini aina
ya Calcium ambayo husaidia kuimarisha mifupa ya mtoto na meno. Vilevile bidhaa
za maziwa zina vitamini D na protini, Vitamini D husaidia kuzuia ugonjwa matege
kwa watoto (Rickets/Soft bone) na Protein husaidia katika ukuaji wa seli hai za
mwili.
6. Kunywa Maji
Maji yanabeba virutubisho vya chakula
ulichokula kupeleka kwa mtoto. Vilevile maji huzuia kupata Hajakubwa ngumu
(Constipation), bawasiri (hemorrhoids), uvimbe na maambukizi ya mfumo wa mkojo
na kibofu. Bawasiri au hemorrhoids kwa jina la kitaalam ni ugonjwa unaotokea
sehemu ya haja kubwa ambapo sehemu ya nyama ya mkundu na sehemu ya utumbo mpana
(Rectum) hutoka nje na kuleta maumivu makali sana, hali hii isipodhibitiwa
mgonjwa huweza kufariki. Ni jukumu la mjamzito kunjwa maji mengi kwa siku ili
kuwa na ujauzito wenye afya, Inatakiwa mjamzito anywe Lita mbili za maji kila
siku. Mimba inavyozidi kuongezeka, kunywa maji kiasi kidogo husababisha nimba
kutoka kabla ya muda muafaka (premature or early labor)
7. Tumia vyakula vya mafuta kwa
kiasi
Mafuta ndani ya mwili husaidia
kuhifadhi nguvu za mwili (energy storage). Kwa hiyo ni muhimu kufahamu aina
gani na kiwango gani cha mafuta hayo kinahitajika mwilini. Mwili wa mjamzito au
mwili wa mtu wakawaida unahitaji mafuta kwa kiwango kidogo. Mafuta
yamegawanyika katika makundi mawili, Unsaturated fats na Saturated fats (Mafuta
yasiyoganda na mafuta yanayoganda). Unsaturated fats ni mafuta yasiyoganda
yakiwa yamehifadhiwa hususani mafuta yatokanayo na mimea kama alizeti n.k.
Saturated fats ni mafuta yanayoganda yakiwa yamehifadhiwa hususani mafuta ya
wanyama. Inatakiwa mjamzito atumie mafuta yasiyoganda kama mafuta ya mimea na
awe anakula vyenye mafuta kidogo.
8. Lala kwa ubavu, usilale chali
Lishe bora ni pamoja na kupumzika, Mjamzito anashauriwa alale kwa ubavu aidha wa kushoto au wa kulia, kwa sababu ukilalia ubavu wa kulia au wa kushoto humpa mtoto nafasi nzuri ya kupumua kwani mfuko wa mtoto (Placenta) unakua umekaa vizuri. Ingawaje ni vizuri zaidi kulalia ubavu wa kushoto kwani tumbo la mama la chakula linakuwa chini ya mfuko wa mtoto, tofauti na akilalia ubavu wa kulia tumbo la mama la chakula linakua juu ya mfuko wa mtoto ambapo huweza kuleta madara ya upumuaji, mtoto anaweza kukosa hewa na kufariki au kuzaliwa na afya mbaya. Kutokana na kwamba ni vigumu kulalia upande mmoja wa kushoto kwa muda mrefu, Mama mjamzito anashauriwa kulalia ubavu wa kushoto au wa kulia lakini muda mwingi awe amelalia ubavu wa kushoto.
NB:
*Kufahamu mambo ambayo hupaswi kufanya wakati wa ujauzito Bofya hapa
*Kufahamu matatizo madogo madogo kwa wajawazito yatokanayo na chakula Bofya hapa
NB:
*Kufahamu mambo ambayo hupaswi kufanya wakati wa ujauzito Bofya hapa
*Kufahamu matatizo madogo madogo kwa wajawazito yatokanayo na chakula Bofya hapa
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
إرسال تعليق