Kilimo cha Matikiti - Sehemu ya Kwanza (Growing Watermelons - Part one)


KILIMO CHA MATIKITI SEHEMU YA KWANZA

Tikiti Maji (Citrullus lanatus) ni zao linalopendelea mazingira ya joto, pia ni jamii ya mazao kama Maboga na matango. Inatakiwa Mkulima achague aina ya Matikiti yanayozaa sana na yanayohimili magonjwa na wadudu. Matikiti yenye rangi ya kijani iliyofifia au kijani kijivu hayaathiriwi sana na jua kali kuliko matikiti yenye rangi ya kijani iliyokolea. Matikiki yanayo vumilia magonjwa kama Mnyauko Fuzari (Fuzarium Wilt) na Chule (Anthracnose) ndiyo yanayopaswa kupandwa.

AINA
Zifuatazo ni aina 18 za matikiti, Baadhi ya aina hizi hulimwa nchini Tanzania. Katika makala hii ya kwanza utaziona aina 7 za matikiti na tabia zake, Makala ya pili utaona aina zingine 11. Tazama vizuri aina hizi za matikiti kwa kutizama picha na maelezo yake;

(1Charleston Gray strains
Aina hii inakomaa kwa siku 85, ina mashina marefu na matunda yake yana rangi ya kijani kwa nje na ni matamu sana, yana rangi nyekundu kwa ndani. Uzito wake hufikia kilogramu 13.



(2) Crimson Sweet
Aina hii hukomaa kwa siku 85, Inahimili sana magonjwa, matunda yake yana rangi nyekundu kwa ndani na ni matamu na yana sukari sana. Uzito wake hufikia kilogramu 11.
(3Jubilee

Aina hii hukomaa kwa siku 95, Inakua vizuri maeneo yenye joto, matunda yake yana michirizi ya kijani, kwa ndani yana rangi nyekundu na ni matamu. Uzito wangu hufikia kilogramu 18.



(4) Carolina Cross
Aina hii hukomaa kwa siku 100, yana umbile kama yai, kwa ndani yana rangi nyekundu na ni matamu. Uzito wake hufikia kilogramu 90 na kuendelea.




(5Ruby Hybrid Seedless
Aina hii hukomaa kwa siku 85, yana umbile la yai, ni matamu sana, yana rangi nyekundu kwa ndani na hayana mbegu. Uzito wake hufikia kilogramu 3.6



(6) Orangeglo
Aina hii inakomaa kwa siku 90, ni matamu sana, yana umbile la yai na Uzito wake hufikia kilogramu 18, kwa ndani yana rangi ya njano na mbegu nyeupe.



(7) Black Diamond
Aina hii inakomaa kwa siku 90, yana umbile la mviringo na uzito wake unafikia kilogramu 34, kwa ndani yana rangi nyekundu na ya kuvutia.



Makala hii Imehaririwa mara ya mwisho Tarehe: 04/07/2017

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post