SEHEMU YA KWANZA
Magonjwa ya macho huwakumba
wanyama wengi wa aina zote, kwa mfano magonjwa ya macho yanayotokana na
majeraha endapo miiba itajeruhi macho wakati wa marisho. Pia kuna magonjwa ya
macho yanayotokana na vimelea.
Yafwatayo ni magonjwa makuu ya
macho yanayowakumba wanyama mbalimbali ikiwemo Ng'ombe, mbuzi na kondoo hapa
nchini Tanzania;
1. Pink Eye
2. Thelaiza Eye Worms
3. Squamous Carcinoma of the eye
Magonjwa hayo makuu matatu,
nimeyaandika kwa kingereza, sina maneno ya kiswahili lakini nitayafafanua
magonjwa hayo vizuri ndani ya makala hii.
CHANZO CHA MAGONJWA HAYA
Magonjwa haya ya macho yanakua na sababu au chanzo,
Vifuatavyo ni vyanzo mbalimbali vya ugonjwa huu;
- Kuumizwa na wadudu mbalimbli hususani wanaopaa.
- Kukumbwa na kupe kuzunguka eneo la macho.
- Uchafu kwenye macho, kama vumbi, nyasi n.k4. Majeraha ya macho yatokanayo na kuchomwa na miiba au nyasi.
- Magonjwa ya kuambukizwa yatokanayo na vimelea kama Pink eye au Camel pox.
- Utomvu au Maji maji yanayowasha yanayotoka kwa baadhi ya mimea kama Euphorbia candelabrum, Maji maji haya yakiingia kwenye macho huleta athari kubwa.
- Kemikali mabalimbali zinazoingia machoni, baada ya mfugo kuogeshwa au kunynyuziwa dawa ya kuua kupe.
- Sumu ya nyoka, Sumu hii ikiingia kwenye macho huleta athari kubwa.
DALILI KUU ZA MAGONJWA HAYA
- Macho yanatoa majimaji yenye rangi nyeupe au njano.
- Jicho au Macho yanafumba kidogo au yaafumba kabisa.
- Jicho au Macho yanavimba
- Macho yanakua mekindu
- Mboni ya jicho inaongezeka ukubwa, kunakua na ukungu mweupe unaongezeka kwenye mboni ya jicho.
NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA HAYA
Zuia magonjwa haya kwa kufanya yafwatayo;
- Mpake ng'ombe wako dawa ya kufukuza wadududu mbalimbali kama kupe na wale warukao.
- Waondoe kupe eneo la macho kwa kutumia mkono.
- Kama unamuongesha mnyama na dawa ya kuua kupe hakikisha haumpulizii moja kwa moja kwenye macho.
- Usimchape mnyama eneo la macho
- Usiwapeleke wanyama wako kwenye marisho yenye miiba mingi au mimea inayotoa majimaji yenye sumu.
- Unapojenga eneo la zizi hakikisha unatumia nyasi au matawi ya miti isiyokua na miiba.
- Wanyama waliougua ugonjwa huu wa macho, watenge na wengine wenye afya ili wasiambukizane.
- Dhibiti ugonjwa wa Camel pox.
UCHAMBUZI WA MAGONJWA MAKUU YA MACHO
Ufuatao ni uchambuzi wa kina kuhusiana na magonjwa makuu ya
macho, ambayo ni Pink Eye, Thelaiza Eye Worms na
Squamous Carcinoma of the eye;
1. PINK EYE (NEW FOREST EYE)
Ugonjwa huu hujulikana kama ugonjwa wa kope, kwa kimombo
huitwa Infectious Kerato Conjunctivitis. Ugonjwa huu huwakumba wanyama kama
Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo. Vimelea vinavyosababisha ugonjwa huu huwa na
mchanganyiko wa vimelea vifuatavyo; Moraxella Bovis, Mycoplasma species, Listeria monocytogenes na
Chlamydia.
Maambukizi hutokea kwa wanyama wa umri wote, lakini mara nyingi
wanyama wenye umri mdogo huathirika sana. Ugonjwa huu huathiri mbuzi na kondoo
kwa asilimia ndogo sana.
Picha: Ugonjwa wa Pink eye au 'New Forest Eye' kwa Ng'ombe Photo Credit: www.beef2live.com
Picha: Ugonjwa wa Pink eye au 'New Forest Eye' kwa Ng'ombe Photo Credit: www.fginsight.com
Namna unavyoenezwa
- Kimelea cha Moraxella bovis ndio kisababishi kikubwa na cha kwanza kusambaza ugonjwa huu kwa ng'ombe.
- Kipindi ambacho ng'ombe wanakula majani, kimelea cha Listeria husababisha ugonjwa wa kope. Lakini ukali wa ugonjwa huwa kidogo ukilinganishwa na pale ambapo ukisababishwa na Moraxella bovis.
- Kwa Kondoo na Mbuzi, kimelea cha Clamydia ndio kisababishi kikubwa cha ugonjwa. Ugonjwa wa kope huwakumba Kondoo na Mbuzi kwa kiasi kidogo sana.
- Ugonjwa huu hauambukizwi baina ya Mbuzi/Kondoo na Ng'ombe kwa sababu kimelea kinachosababisha ugonjwa huu kwa ng'ombe (Moraxella na Listeria) hakifanani na kimelea kinachosababisha ugonjwa huu kwa Mbuzi na Kondoo (Clamydia).
- Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusana baina ya mnyama mgonjwa na mzima hususani wakati wanyama hao wapo wengi au wanelundamana zizini.
- Wadudu wanaopaa (Flies) kama Inzi nao husambaza ugonjwa huu, pale wanapotua kwenye macho ya mnyama mgonjwa na kwenda kugusa macho ya mnyama mzima.
- Pia ugonjwa huu husambazwa kupitia mazingira ya vumbi, maeneo ya malisho hususani nyasi zilizochafuliwa na majimaji yaliyotoka kwenye macho ya kuku mgonjwa n.k
Dalili za ugonjwa
- Ugonjwa huanza siku 2-3 tangia vimelea viingie machoni (Incubation period), mara nyingine huenda mpaka wiki tatu(3).
- Macho yanakua na majimaji pia sehemu ya ndani ya kope huwa nyekundu na huvimba na mnyama hupapasa macho mara kadhaa mfululizo. Pia mnyama anakua hapendi kuangalia mwanga wa moja kwa moja.
- Utaona kitu kama kovu kwenye mboni ya jicho, mwanzoni kovu hilo huwa na rangi ya kufifia lakini baada ya masaa machache kovu hilo huwa zito.
- Baada ya siku mbili hadi tatu mboni yote hupoteza rangi yake ya kawaida na mnyama hupoteza kabisa uwezo wa kuona. Kama jicho limekua na rangi nyeupe au bluu hii hutokana na mlundikano na majimaji ya vimelea. Kama jicho limekua na rangi ya maziwa au njano hii hutokana na seli hai nyeupe zilizokufa na hii huashiria ukali wa ugonjwa (severe infection).
- Utaona mishipa ya damu inayoelekea kwenye mboni ya jicho.
- Pia utaona usaa karibia na mboni ya jicho
- Usaa ukizidi eneo la mboni husababisha mboni ya jicho kupasuka.
- Mnyama hukosa hamu ya kula kwa sababu ya maumivu na ile hali ya kutoona vizuri.
- Utoaji wa maziwa hupungua kwa kiasi kikubwa pia uzito hupungua sana.
Namna ya kuuzuia na kuudhibiti
- Epuka msongamano wa wanyama zizini, hii husaidia kuepusha mgusano na kuambukizana.
- Wanyama wagonjwa watengwe na wale wazima halafu watibiwe.
- Wanyama wagonjwa wawekwe kivulini.
- Hakikisha unasafisha zizi mara kwa mara ili kupunguza idadi ya inzi, kwani inzi hawa husambaza ugonjwa huu.
- Unaweza ukapiga dawa za kuua wadudu warukao zizini kama inzi, hii pia itasaidia kupunguza idadi yao na kupunguza maambukizi mapya.
Namna ya Kuutibu (Matibabu yanayofaa)
- Antibayotiki mbalimbali hutumika kutibu ugonjwa huu, na mnyama hupatiwa dawa hizi kupitia njia mbili ambazo ni; Kuchoma sindano au kuwekwa machoni.
- Antibayotiki aina ya Oxytetracycline hufaa sana kwa matibabu ya ugonjwa huu, dawa hii itumike kulingana na ushauri wa daktari wa mifugo na maelekezo ya mtengenezaji.
- Pia kuna antibayotiki zingine zinazofaa kutibu ugonjwa huu kama Ampicillin, Penicillin, gentamycin na Kanamycin, dawa hizi huchomwa sehemu ya macho (Injected into the eye) Uchomaji wa dawa hizi eneo la macho ufanywe na daktari wa mifugo.
- Kuweka dawa za maji (matone) au za unga machoni nako husaidia kutibu ugonjwa huu, ili mnyama apone haraka inatakiwa uweke dawa hii mara kwa mara hususani mara tatu kwa siku kila siku.
- Dawa hizi za maji (matone) au za unga huwa ni antibayotiki aina ya Oxytetracycline/Polymixin B, Gentamycin na Erythromycin. Dawa hizi zinafanya kazi vizuri hakikisha inawekwa kwa uangalifu ndani ya kope ya juu na kope ya chini.
- Pia matumizi ya dawa za matone aina ya Atropine 1% au za Unga husaidia kupunguza athari za ugonjwa
NB:
Kama uvimbe ndani ya jicho ukipasuka na kutoa usaa, jicho
hupasuka na kusinyaa. Wakati huo kunakua maumivu ya jicho na jicho kutoa
majimaji na usaa. Kumuondolea adhaa hii mnyama inatakiwa jicho litolewe na
daktari wa mifugo, ili ibaki misuli ya macho na sehemu ya jicho kushikana.
*Antibayotiki: Ni dawa za kuzuia ukuaji na kuua vimelea vya magonjwa kama bakteria na wengine isipokua virusi.
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Post a Comment