Hawa ni minyoo wanaoishi ndani ya
kope za macho (Conjunctival sac) na huathiri jamii mbalimbali za wanyama
Duniani kote kama; Ng'ombe, Kondoo, Farasi, Ngamia, Mbuzi, Nguruwe, Mbwa, Paka,
ndege na Binadamu anaweza kumbukizwa. Minyoo hii ipo ya aina mbalimbali ikiwemo
Thelazia rhodesii ambayo huwakumba Ng'ombe na Kondoo. Minyoo hawa huwa na
ukubwa hadi kufikia urefu wa sm 2 na ni wembamba na weupe, Jicho moja au yote
mawili huweza kuathiriwa.
Namna inavyoenezwa
- Jamii mbalimbali za wadudu warukao ambao kiwavi (mnyoo) ni sehemu ya mzunguko wa maisha yao (Lyfe cycle), ndo husababisha kuenea kwa minyoo hawa kutoka mnyama mmoja hadi mwingine. Wadudu hawa warukao kama Inzi na wengine hutaga mayai au husambaza mayai ya mdudu mwenzie aliyetaga, hatimae mayai hayo huanguliwa na kuwa minyoo.
- Wadudu hawa warukao hufwata majimaji ya vimelea yanayotoka kwenye macho, hatimae huwa ndo mwanzo wa kusambaza minyoo hawa. Minyoo hawa huanza uharibifu kuanzia wiki 1 tangu vimelea viingie machoni na kuendelea hadi wiki 4.
- Minyoo hawa huishi ndani ya kope za macho, pia minyoo hawa wana ngozi rafu ambayo husuguasugua mboni ya jicho na kusababisha uvimbe.
Dalili za Minyoo hawa
- Macho ya mnyama hutoa machozi mengi kupita kiasi, machozi hayo huweza kuwa na usaa.
- Mnyama huepuka mwanga wa jua.
- Kuvimba kope za macho (Conjunctivitis).
- Mboni ya jicho huvimba na mara nyingine huwa na usaa.
- Mnyama kutopona baada ya matumizi ya dawa mbalimbali za antibayotiki [Kwa sababu dawa za antibayotiki huua vimelea vya magonjwa kama bakteria na wengine isipokua Virusi, minyoo haimalizwi kwa antibayotiki]
Kuchunguza Minyoo hawa
Mkaribie mnyama wako na chunguza
kwa makini machoni, utaona minyoo myeupe midogo midogo ikitembea juu ya uteute
wa jicho. Ingawa minyoo hawa wanaonekana kwa macho hakikisha unamuona daktari
wa mifugo ili athibitishe uwepo wa minyoo hawa.
Picha: Minyoo ya jicho ikionekana juu ya uteute wa jicho Photo Credit: www.vetbook.org
Picha: Minyoo ya jicho ikionekana juu ya uteute wa jicho la ng'ombe Photo Credit: www.intelligenceway.com
Namna ya kukinga minyoo hawa
Athari ya minyoo hawa ni ndogo
tofauti na ugonjwa wa Pink eye. Kwa hiyo kudhibiti wadudu warukao ni jambo jema
kwani itapunguza maambukizi mapya. Piga dawa mbalimbali za kuua wadudu hawa pia
safisha banda au zizi lako kila wakati ili kuondoa mazalia ya wadudu warukao.
Namna ya kutibu (Matibabu yanayofaa)
- Daktari wa mifugo anaweza akaondoa minyoo hao kwa kutumia vifaa maalumu (Forceps) baada ya kuweka dawa maalumu ya maji kwenye macho [Local anaesthetic solution au Eye wash yenye Local anaesthetic solution], dawa hizi maalumu za maji huwaondosha minyoo hawa kwenye macho.
- Mchanganyiko wa mls 10 za 2% Local anaesthetic solution na mls 40-50 za maji masafi hutengeneza EYE WASH iliyo kamili.
- Mls 5-10 za eye wash huwekwa kwenye macho, baada ya hapo subiri dakika mbili, baada ya dakika mbili kuisha yaoshe macho kwa kutumia maji safi ya baridi, kwa hatua hii minyoo wote watakua wameshatoka kwenye macho.
- Baadhi ya dawa mbalimbali za minyoo (Dewormers) kama Levamisole, Ivermectin na Doramectin kwa kuchoma chini ya ngozi (SC) au kwenye misuli (IM) husaidia kuua minyoo hawa.
3. SQUAMOUS CELL CARCINOMA
Huu ni ugonjwa wa kansa ya jicho,
ni uvimbe ambao mara nyingi huwakumba ng'ombe wa kisasa kama Friesian/Holsteins
na Ayrshires.
Kwa ng'ombe wa kienyeji ni mara
chache sana kupata ugonjwa huu.
Visababishi vya Ugonjwa
Sababu mbalimbali huchangia
kusababisha ugonjwa huu ikiwemo zifuatazo; Mwanga wa jua, Magonjwa ya kope,
Sababu ya vinasaba (Genetic make-up), Lishe duni na vimelea vya virusi.
Picha: Kansa ya jicho la ng'ombe Photo Credit: www.drssnairvet.blogspot.com
Picha: Kansa ya jicho la ng'ombe Photo Credit: www.acvs.org
Dalili za Ugonjwa
- Michilizi huonekana machoni na mboni ya jicho hubadilika rangi na kuwa nyeupe (mtoto wa jicho). Hali hii husababisha uvimbe ndani ya jicho usio wa kansa unaoitwa Papilloma (a small solid benign tumour with a clear-cut border that projects above the surrounding tissue). Baada ya huo uvimbe (Papilloma) kutokea, baadae kunazaliwa uvimbe wa kansa unaoitwa Cancerous squamous cell carcinoma.
- Macho yote mawili yanaweza kuathiriwa, pia kunakuwa na kutokwa kwa majimaji machoni.
- Uvimbe huweza kuwa mkubwa na kuathiri jicho lote, baadae jicho lote huharibika likiwa na ongezeko la uvimbe. Ikifikia hatua hii Hakuna Tiba.
TAZAMA VIDEO HAPO CHINI KUFAHAMU ZAIDI
Video Credit: Dr Sudheesh S Nair Youtube channel
Matibabu
- Matibabu ya mapema husaidia sana, aidha kwa kufanya oparesheni na kuondoa uvimbe au kama itashindikana ifanyike oparesheni ya kuondoa jicho lote.
- Madaktari wa mifugo waliofuzu vizuri taaluma yao wanaweza kuwa na njia nyingine za kutibu ugonjwa huu kama kutumia njia maalum ambazo ni; Cryotherapy, Hyperthermia, Radiation therapy na Immunotherapy.
*Cryotherapy ni njia ya kuondoa au kuharibu uvimbe kwa
kutumia Kimiminika maalum cha baridi sana (extremely cold liquid) au kwa
kutumia kifaa maalum.
*Lakini njia muhimu ya kudhibiti
ugonjwa huu ni pamoja na; Matibabu ya mapema, Uangalizi wa karibu na wa mara
kwa mara kwa mifugo yako ili kubauini magonjwa hayo.
<<< SEHEMU YA KWANZA
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
<<< SEHEMU YA KWANZA
*MWISHO WA MAKALA HII*
Post a Comment