Jifunze kuondoa Chunusi kwa kutumia njia za asili (Remove your Pimples naturally)


Baadhi ya njia za asili zinazotumika kuondoa chunusi ni pamoja na kutumia vitu vitu vifuatavyo;

1. Magadi Soda
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na hasa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji ya baridi. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.



2. Matango
Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.

Matango ni mazuri sana kwa kusafishia uso na hasa ukiwa na chunusi. Kata tango na kisha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Acha ikae kwa muda wa dakika 15-20 kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.



3. Kitunguu swaumu
Unaweza kutumia kitunguu swaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu swaumu, huleta matokeo mazuri sana kwa kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria kwasababu kina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.




4. Mnana (Peppermint)
Unaweza kutumia majani ya Mnana kuondoa chunusi usoni. Majani ya mnana hutumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kichwani. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Acha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.







5. Limao
Kata limao na tengeneza juisi kisha tumia kijiti chenye pamba loweka kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia kupaka kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao yaliyosindikwa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali ambavyo huondoa ubora limao halisi, Hivyo unashauriwa kutumia limao halisi.




6. Asali
Matumizi ya asali ni ya asili na hufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi. 

Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Baada ya asali kukaa kwenye ngozi kwa muda utakaoridhika unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.




7. Papai
Matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.

Ponda ponda kiasi kidogo cha papai alafu paka sehemu iliyoathirika kisha acha kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Baada ya papai kukaa usoni kwa muda unaoupenda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya baridi. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kadiri unavyopenda.




8. Dawa ya Meno
Unaweza kushangaa sana, lakini ndio ukweli. Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika 5 mpaka 10. 

Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.




9. Matumizi ya Poda
Unaweza kutumia baby powder au poda aina nyingine kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na na kuiacha mpaka asubuhi.



10. Matumizi ya Mvuke
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.



>>Tazama video hapo chini jinsi chunusi inavyotengenezwa ndani ya ngozi








Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

4 Comments

  1. Dah, shukran sana ndugu kwa posti zako nzuri. Nimejifunza mengi kupitia kwako. Mungu akubariki mkuu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pia nami nakushukuru sana kwa kutembelea blog yangu, endelea kuwa nami kila wakati, nitajitahidi kuposti vitu vitakavyowasaidia wasomaji na kuwaburudisha pia. kama kuna mapungufu yoyote nijuze ndugu, ili niendelee kujiboresha siku hadi siku.

      Delete
    2. Bila shaka mkuu, Tuko pamoja.

      Delete

Post a Comment

Previous Post Next Post