Kilimo cha Viazi mviringo - Sehemu ya pili (Growing Irish potato - Part two)



MAGONJWA (DISEASES)

1. Bacterial wilt
Huu ni ugonjwa wa bacteria unaoonekana karibu kila eneo la mmea. Pia ugonjwa huu unaathiri mazao mengine kama Nyanya, tumbaku na bilinganya.

Mmea ulioathirika unaanza kukauka kuanzia mwishoni mwa majani au semehu yalikoanzia matawi na baada ya hapo husambaa sehemu zote mmea.

Majani yanakua njano hatimae mmea mzima hukauka na kufa. Ukikata shina utaona michilizi ya rangi ya brauni. Ukikata kiazi chenyewe utaona michilizi ya rangi nyeusi au brauni. Hali hii ikizidi viazi huoza.

*Namna ya kidhibiti ugonjwa huu
Ugonjwa huu ni vigumu sana kuudhibiti kwa sababu bakteria anaesababisha anakaa kwenye udongo (soil borne diseases). Lakini unaweza ukafanya yafuatayo kupunguza athari ya ugonjwa;
~Badilisha mazao, usipande mazao jamii ya viazi kama nyanya na bilinganya
~Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kitaalamu.
~Usimwagilie kwa kutandaza maji kwenye udongo (Flooding) kwa sababu bakteria wanaweza kuenea shamba zima. Au zuia kusambaa kwa maji kutoka eneo moja hadi lingine la shamba.
~Choma moto masalia baada ya kuvuna.


2. Septoria Leaf spot
~Ugonjwa huu huathiri mimea michanga
~Utaona alama au kovu dogo lenye umbile la mviringo au umbile lingine la zigizaga, alama hizo huwa na rangi ya kijivu katikati na rangi nyeusi kwenye majani.
~Alama hizo huanza kwenye majani ya chini na taratibu zinasambaa mpaka majani ya juu.
~Baadae sana alama hizo hukusanyika pamoja na majani huwa na weupe.
~Majani yaliyoathirika huanza kupukutika
~Mashina ya mmea na maua huanza kuathirika
~Matunda huathirika kwa kiasi kidogo sana.

*Namna ya kudhibiti ugonjwa huu
Piga dawa za ukungu zenye sulfur au copper mfano "Blue copper" kila wiki mara moja baada ya kuona dalili za awali za ugonjwa huu ili kuzuia kuenea zaidi. Dawa zingine za ukungu tofauti na hizo za sulfur au copper (organic fungicides) haziwezi kuua vimelea vya leafspot bali zitazuia kukua kwa hivyo vimelea (spores).


3. Late blight
Ugonjwa huu unaharibu majani, mashina na matunda (viazi). Majani yaliyoathirika yanakuwa na makovu kana kwamba yameunguzwa na maji ya moto, baadae yanaoza na kukauka.

Mmea ukianza kukauka, majani hubadilika rangi na kuwa brauni au rangi nyeusi. Mashambulizi ya ugonjwa huu yakizidi alama (spot) huonekana chini ya majani na hufunikwa na ungaunga mweupe.

Shina lililoathirika huanza kuwa jeusi maeneo ya juu, na baadae hufa kabisa.

Mashambulizi ya ugonjwa huu yakizidi, majani huanza kuoza,kukauka na kuanguka, mashina nayo hukauka hatimae mmea hufa.

Viazi vilivyoathirika huonyesha madoa ya rangi ya brauni kwenye ngozi na ndani ya kiazi. Ugonjwa huu unashambulia kwa kasi sana, mmea ulioathirika usipotibiwa mapema, unaweza kufa ndani ya siku mbili au tatu.

*Namana ya kudhibiti ugonjwa
Udhibiti mzuri wa ugonjwa huu ni kutumia njia mbali mbali kwa wakati moja (Integrated disease management approach). Njia hizo ni pamoja na Njia za asili (kama usafi wa shamba, kubadilisha mazao n.k) na njia za kisasa (kama matumizi ya madawa ya kutibu magonjwa) pamoja na kutumia mbegu zinazohimili magonjwa.

NB: Magonjwa ya viazi yako mengi sana, kwenye makala hii nimeeleza magonjwa matatu tu. Endelea kutembelea blogi hii siku zijazo nitaongeza tena magonjwa mengine kwenye makala hii.


WADUDU WAHARIBIFU (INSECT PEST)
1. Potato tuber moth (Phthorimaea operculella)
Hawa ni wadudu wadogo na wana rangi ya kijivu iliyochanganyika na rangi ya brauni, wana mabawa, wana urefu wa mm 12, Viwavi wake wana rangi ya pinki mpauko au kijani mpauko na wana urefu wa mm 14 - 20.

*Uharibifu
Viwavi wake wanatoboa mashina ya majani na sehemu ya juu ya shina kuu.
Viwavi wanatoboa matunda (Viazi) na kupelekea kuoza.

*Namna ya kumdhibiti mdudu huyu
~Jaza udongo kwenye mashina kuhakikisha hakuna viazi vinavyoonekana nje ya udongo, hii itasaidia kupunguza athari ya ugonjwa.

~Piga dawa za kuua wadudu waharibifu wa kwenye mazao kama Karate, Serecron, Actellic n.k hii itasaidia kumua mdudu moth anaetaga mayai na kuzalisha viwavi, pia na kuua viwavi.



2. Potato Cut worm (Agrotis ypsilon)
Hawa ni viwavi wa kipepeo wenye urefu wa mm 40 - 48 , wana rangi ya kijivu au nyeusi wana tabia ya kujikunja mara unapowagusa.

*Uharibifu
Signs of damage on tubers are boreholes, larger than
Wanaharibu mashina na matunda (viazi) hasa giza likiingia.
Wanakata mashina ya miche michanga, kimo cha usawa wa ardhi. Mara nyingi Miche michanga inayoathirika ni yenye umri wa siku 25 hadi 35 baada ya kupanda.
Wanatoboa viazi na kusababisha matundu makubwa.

*Namna ya kumdhibiti mdudu huyu
Hakikisha shamba lako linakuwa safi wakati wote
Tumia dawa za kuuwa wadudu kama Carbaryl na nyingine nyingi




3. Epilachna beetle of Potato (Epilachna viginatioctopunctata)
Wadudu hawa wana maumbile tofauti na wengine, wana rangi ya brauni mpauko na madoa madoa meusi. Viwavi wake ni wa njano na wana manyoya mwili mzima.

Mdudu huyu na kiwavi wake hula umbijani la majani na kusababisha jani kuwa na matobo kama nyavu nyavu (skeletonised patches on leaves).

*Namna ya kumdhibiti mdudu huyu
Piga dawa ya wadudu inayopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo
Unaweza kuwakusanya hawa wadudu (beetle) kwa kutumia neti, ili kupunguza athari.
Tumia mwarubaini (Neem), hii ni njia ya asili, chakufanya chukua majani au mbegu zake, anika kivulini mpaka zikauke. Ukianika juani zinapunguza ukali wa dawa. Zikisha kauka saga au twanga alafu changanya na maji kiasi alafu piga shambani, itaua mdudu mwenyewe pamoja na kiwavi wake.



NB: Wadudu waharibifu wa zao hili wapo wengi, kwenye makala hii nimeeleza wadudu watatu tu. Endelea kutembelea blogi hii siku zijazo nitaongeza tena wadudu wengine kwenye makala hii.

MAVUNO (HARVESTING)
Viazi mviringo huwa tayari kuvunwa baada ya miezi mitatu hadi minne kutegemeana na hali ya hewa na aina ya mbegu. Ukifwata taratibu zote za kilimo bora unaweza ukapata tani 15/hekta moja.

<<< BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KWANZA <<<

MWISHO WA WA MAKALA HII

Makala hii Imehaririwa mara ya mwisho tarehe: 18/07/2017

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post