Lifahamu gugu karoti na madhara yake ( Know the effects of Parthenium hysterophos weed to animals and humans)


Gugu karoti (Parthenium hysterophos) ni magugu hatari kwa afya ya mmea na wanyama (noxious weed). Magugu haya yapo sana bara la Amerika, Asia, Afrika na Austraria. Mwaka 2017, Gugu hili liliingia nchini Tanzania kupitia Arusha. Inasemekana kwamba gugu hili limetokea ethiopia kupitia kenya hadi Tanzania (Arusha).




Taasisi ya kudhibiti ubora wa madawa ya magonjwa na wadudu wanaoathiri mimea nchini Tanzania (TPRI) inafanya utafiti wa dawa za kudhibiti gugu hili, pia imeomba ushirikiano wa Taasisi zingine za kilimo kufanya utafiti wa gugu hili.

Mkuu wa Idara ya Utafiti wa Magugu ya TPRI Dr. Ramadhani Kilewa alisema gugu hilo ni geni nchini, limekua likiota pembezoni mwa barabara na mbegu zake husafirishwa kwa maji ya mvua na upepo mkali.

Dr. Kilewa alisema mpaka sasa dawa ya kudhibiti magugu hayo haijapatikana, bali njia iliyopo ni kuling'oa na mizizi yake na kisha kulichoma moto.

MADHARA YA GUGU KAROTI KWA MIMEA, WANYAMA NA BINADAMU
Binadamu akiligusa hili gugu huzalisha sumu mwilini hatimae mwili wake huvimba na kutoka vipele vya harara (contact dermatitis). Pia husababisha matatizo ya upumuaji (allergic respiratory problems) pamoja matatizo ya vinasaba (mutagenicity) kwa mifugo na binadamu.




Uzalishaji wa mazo hupungua kwa kasi kwa sababu gugu karoti hutengeneza kemikali kwenye udogo (growth inhibitors) ambayo huzuia kuota au kukua kwa mazao (allelopathy).

Gugu hili likitawala eneo la shamba huharibu mfumo mzima wa maisha ya mimea au mazao mengine (biodiversity).

Gugu karoti kubwa moja huzalisha mbegu hadi Laki moja (100,000), zaidi ya mbegu milioni 340 kwa hekta moja huwepo chini ya udongo. Mbegu za gugu karoti hazina muda wa kutokuota (Domancy period) na zina uwezo wa kuota muda wowote endapo maji au unyevu utakuwepo.

Mbegu za Gugu karoti huenezwa kwa njia zifuatazo; maji yanayotembea, wanyama, magari, mashine, mazao ya wanyama au mimea yanayosafirishwa kutoka nje ya nchi. Pia upepo usafirisha mbegu hizi kwa kiwango kidogo. Usambazaji wa masafa marefu ni kupitia magari, mashine za shamba na mafuriko.

NAMNA YA KUDHIBITI GUGU KAROTI
1. Ng'oa gugu hili kabla halijatoa maua na kutengeneza mbegu, fanya hatua hii wakati udongo una unyevu wa kutosha. Njia hii ni zuri zaidi kwani husaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha gugu hili katika eneo husika. Uking'oa gugu baada ya kutengeneza mbegu utasababisha usambazaji wa mbegu hizo shambani.

2. Kuchoma moto ni njia mojawapo ya kudhibiti gugu hili, lakini kuna uwezekano wa kuziacha mbegu zingine kuendelea kuota kwa msimu mwingine. Udhibiti wa asilimia 100% ni kuling'oa kabla halijatoa maua na kutengeneza mbegu.

3. Kutumia madawa ya kuua magugu: Madawa kama Glyphosate, atrazine na metribuzin yamekua yakitumika kuua gugu hili, lakini mafanikio yake ni madogo sana. Imeonekana kwamba ni vizuri kupiga dawa hizo za magugu kabla ya gugu karoti halijatengeneza maua au mbegu.

4. Njia ya kibaolojia: Wadudu mbalimbali na vimelea mbali mbali vimekua vikitumika kwa muda mrefu sana. Mdudu jamii ya bito (bwetle) Zygogramma bicolorata na Epiblema strenuana wanatumiwa na nchi nyingi kudhibiti gugu karoti. Zygogramma bicolorata anatumika kwa sasa nchini India kudhibiti Gugu pori. Nchini Australia wadudu hao wote wamekua wakitumika kudhibiti gugu hili na kuonyesha mafanikio makubwa.

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post