Muongozo wa dalili za ukosefu wa virutubisho au hali yoyote tofauti kwenye zao la Mahindi


MUONGOZO WA DALILI ZA UKOSEFU WA VIRUTUBISHO AU HALI YOYOTE TOFAUTI KWENYE ZAO LA MAHINDI

Ukosefu wa virutubisho kwenye mmea wa mahindi huonekana bayana, kwani mmea utaonyesha dalili mbalimbali kwenye majani au kwenye mmea wote ili kuashiria mapungufu ya virutubisho hivyo. Ufuatao ni mchanganuo wa dalili mbalimbali za mapungufu haya kwenye majani, mizizi na watoto wa mahindi.

A: MAPUNGUFU YA VIRUTUBISHO KWENYE MAJANI
Kabla ya kuona dalili za mapungufu kwenye majani, tutizame muonekano wa majani ya mahindi yenye afya, yasiyo na mapungufu yoyote.

Mmea wenye afya:
Majani yenye afya hung'aa na kua na rangi ya kijani iliyokolea sana.

Picha: Shamba la mimea ya mahindi yenye Afya

1. Mapungufu ya Phosphate (Fosforasi)

Dalili
Majani yenye rangi ya dhambarau iliyochangamana na wekundu, hususani kwa mimea michanga.

Photo Credit: www.thomascountyag.com

Photo Credit: www.cropnutrition.com


Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zenye kirutubisho cha Phosphate (Fosforasi) kwa kupandia au kukuzia kama DAP, NPK, TSP, NPS, NPS-Zn n.k

2. Mapungufu Potashi (Potasiamu)

Dalili
Sehemu za mwisho za majani (Tips and Edges of lowest leaves) hukauka hususani kwa majani ya chini
Photo Credit: www.thompsonslimited.com

Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zenye kirutubisho cha Potasiamu kwa kukuzia kama NPK, MOP (Murate of Potash) n.k

3. Mapungufu ya Naitrojeni
Dalili
Majani huwa na rangi ya njano inayoanzia mwishoni mwa jani (Tips), na unjano huo huongezeka kuelekea katikati ya jani.

Photo Credit: www.apps1.cdfa.ca.gov

Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zenye kirutubisho cha Naitrojeni kwa kukuzia kama UREA, NPK, NPS, NPS-Zn n.k. Tumia mbolea hizi wakati Mahindi yangali na umri mdogo kuanzia mwezi mmoja hadi miezi miwili, kwani ukiweka kwa kuchelewa huwezi kupata matokeo mazuri.

4. Mapungufu ya Magnesium (Mg)
Dalili
Majani huwa na michilizi yenye rangi nyeupe kuelekea urefu wa jani na mara nyingi rangi ya dhambarau huonekana chini ya majani kwa majani ya chini.


Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zilizongezwa magnesium kama NPK+Mg, au tumia mbolea za maji za kwenye majani (Booster), mara nyingi mbolea hizi za maji huwa zina virurutubisho vyote yaani virutubisho vikuu (Macro-nutrients) kama Nitrogen (N), Phosphorus (P) na Potassium (K); na virutubisho vidogo (Micro-nutrients) kama Magnesium (Mg), Zinc (Zn), Boron (Bo), Sulfur (S), Calcium (Ca) n.k


B: MAPUNGUFU YA VIRUTUBISHO KWENYE WATOTO WA MAHINDI

Muonekano wa mtoto wa mahindi aliye na afya:
Muhindi hua mkubwa na ujazo wa kutosha kuanzia sehemu ya kikonyo mpaka mwishoni mwa muhindi, ukijaribu kuuminya utaona ujazo halisi wa mahindi.


1. Mapungufu ya Potash (Potassium)
Muhindi uliokosa kirutubisho cha Potash huwa hauna ujazo na unakua na mapengo mengi. Ukijaribu kuuminya utaona mapengo mengi yasiyokua na mbegu za mahindi.

Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zenye Potassium kama NPK, MOP n.k hususani kwa kipindi cha awali cha ukuaji kabla mmea haujatoa mbelewele.

2. Mapungufu ya Phosphate (Fosforasi)
Upungufu wa phosphate hupunguza uwezo wa uchavushahi wa poleni za mahindi, hali itakayopekekea muhindi kutokua na ujazo na kua na mapengo mengi, pia husababisha watoto wa mahindi kuwa wadogo sana.

Namna ya kushibiti
Tumia mbolea zenye Phosphate kama DAP, NPK, TSP n.k hususani kipindi cha awali cha ukuaji kabla mmea haujatoa mbelewele.

3. Mapungufu ya Nitrojeni
Kirutubisho cha nitrojeni ni muhimu sana kwa mmea wakati wote wa ukuaji, mmea ukikosa kirutubisho hiki kwa mda mrefu, protini hupungua kwenye mmea hali inayopelekea watoto wa mahindi kuwa wadogo na mbegu za mahindi hazijai mwishoni mwa muhindi.

Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zenye Nitrojeni kama UREA, NPK, CAN, n.k. hususani kwa kipindi cha awali cha ukuaji kabla mmea haujatoa mbelewele.


C: MAPUNGUFU YA VIRUTUBISHO KWENYE MIZIZI

Mizizi yenye afya
Huwa nimirefu na iliyotawanyika vizuri.

1. Mapungufu ya Phosphate
Kirutubisho cha Phosphate (Fosforsi) ni muhimu sana kwa kuboresha mizizi hususani kwa mimea michanga, upungufu wa kirutubisho hiki husababisha mizizi kudumaa, kuwa mifupi na kutotawanyika vizuri. Mizizi ikidumaa, mmea nao hudumaa.

Namna ya kudhibiti
Tumia mbolea zenye phosphate kama DAP, TSP, NPK n.k. hususani kwa kipindi cha awali cha ukuaji kabla mmea haujatoa mbelewele.


D: UKAME

Dalili
Watoto wa mahindi huwa na rangi ya kijivu iliyochangamana na kijani na majani hujikunja na kujiviringisha na kua na unene wa kalamu ya risasi.

Photo Credit: www.neweralive.na

Namna ya kudhibiti
Mwagilia maji ili kudhibiti tatizo hili kabla ya 

E: KUUNGUZWA NA KEMIKALI (CHEMICAL BURN)
Mahindi yaliyounguzwa na Kemikali hususani madawa ya kuua wadudu huonyesha dalili zifuatazo;

Dalili
Pembe za majani au jani lote hua na muonekano wa kuungua mithili ya kunyauka, Tishu za jani au sehemu yoyote iliyogusana na kemikali hizi hufa na hunakiza muonekano mabaka meupe.

Namna ya kudhibiti
Tumia dozi sahihi ya kiua sumu kama kilivyoainishwa kwenye kibandiko cha chupa ya kiua sumu hicho.

NB:
Hayo ndio maelezo ya kina kuhusiana na mapungufu mbalimbali ya virutubisho pamoja na hali mbalimbali zilizotofauti kwa mmea wa mahindi. Kama una maoni au ushauri wowote kuhusiana na makala hii, usisite kutuachia hapo chini, Karibu sana!!.

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post