Kilimo bora cha Nanasi - Sehemu ya Nne (Growing Pineapple - Part Four)


SEHEMU YA NNE

3. Mealybug or pineapple wilt virus
Mmea ulioathirika huwa na rangi ya njano iliyochangamana na rangi nyekundu mwishoni mwa pembe za majani (leaf tips), baadae hali hii hulikumba jani zima. Hali hii pia husambaa kwa majani mengine, majani yaliyobadilika rangi hunyauka.

Mmea ulioathirika sana hudumaa na hutoa matunda madogo na yasiyokomaa, madhara ya kwanza hutokea kwenye mizizi ambapo husimama kukua na baadae huoza. Hali hii husababisha majani kukauka mithiri ya hali ya ukame.

Ugonjwa huu mara nyingi hutokana na vikonyo vya kupandia vilovyoathirika na ambavyo havikuonyesha dalili yoyote hapo awali. Baada ya mmea kuanza kuota mdudu aina ya Mealybugs huanza kuusambaza ugonjwa huu kwenda kwenye mimea yenye afya.

Photo Credit: www.pestnet.org

Photo Credit: www.pestnet.org

Namna ya kudhibiti
  • Tumia vikonyo vya kupandia vilivyotoka kwenye mmea wenye afya ambao haukuonyesha dalili yoyote ya kunyauka
  • Wadhibiti wadudu aina ya Mealybugs (Namna ya kudhibiti wadudu hawa, rejea hapo juu kwenye kipengele cha wadudu waharibifu.)
  • Tibu vikonyo vya kupanda kwa kutumia maji ya moto yenye nyuzi joto 50°C, loweka vikonyo hivyo kwenye maji hayo kwa dakika 30. Hatua hii huondoa ugonjwa huu wa virusi pamoja na makoloni ya mealybugs kwa asilimia 100%. Vikonyo vilivyotibiwa na maji ya moto hukua haraka sana kuliko ambavyo havijatibiwa.
  • Utafiti umebaini kwamba mimea iliyotokana na vikonyo vilivyotibiwa na maji ya moto, haipatati ugonjwa huu wa virusi au kukumbwa na mealybugs kwa zaidi ya miaka miwili tangu kupandwa kwenye shamba lilikoathirika sana na ugonjwa huu (Mealybug wilt).
  • Panda aina ya nanasi inayovumilia ugonjwa huu kama Singapore spanish (Red Spanish), aina kama Cayenne na Masmerah huathiriwa sana na ugonjwa huu.
4. Yellow spot virus
Ugonjwa huu hufanana sana na ule unaoathiri zao la nyanya (Tomato spotted wilt virus). Ugonjwa huu huathiri zaidi ya mamia ya aina mbalimbali za mimea ikiwemo Pilipili, Nyanya, Tumbaku, Bilinganga, Viazi mviringo, Jamii yote ya Maharage, Spinachi n.k. 


Photo Credit: www.researchgate.net

Magugu aina mbalimbali yamekua yakitunza virusi hawa kama Machoma nguo (Black jack, Bidens pilosa), Emilia sonchifolia na Datura stramonium, Tazama picha hapa chini kuyafahamu magugu haya;

A: BLACK JACK



Photo Credit: www.ngoosen.fotki.com

BEMILIA SONCHIFOLIA

Photo Credit: www.flickr.com

Photo Credit: www.commons.wikimedia.org


Photo Credit: www.weeds.brisbane.qld.gov.au

CDATURA STRAMONIUM (JIMSON WEED)

Photo Credit: www.worldseedsupply.com

Photo Credit: www.rhs.org.uk


Photo Credit: www.plantsam.com



Photo Credit: www.monaconatureencyclopedia.com


Wadudu wanaosambaza virusi hawa wanaitwa Thrips, kuwaelewa zaidi rejea kipengele cha wadudu waharibifu. Kama magugu hayo niliyaekezea hapo juu yakaota karibia na mmea wa nanasi, basi utapata ugonjwa huu haraka sana kwa sababu wadudu hawa (Thrips) wanahama kutoka maeneo yenye magugu haya kwenda kwenye shamba la nanasi. Vilevile upepo unaweza ukawabeba wadudu hawa na kuwasafirisha umbali mrefu, pia ikawa ni chanzo kimojawapo cha kusambaza virusi wa ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa za ugonjwa huu ni pamoja na Tunda la nanasi kuwa jeusi (Blackened), huwa linakuwa na uwazi kwa ndani uliokauka (Dry cavity) kutokana na moja wapo macho ya tunda la nanasi kufa, Hali hii huitwa "Macho yaliyokufa" (Dead eye). Macho ya tunda la nanasi ni kama vijisehemu kwenye tunda la nanasi kama vina uwazi fulani hivi.

Ugonjwa huu husababisha madoa madoa yenye rangi ya njano ambayo baadae yanaongezeka ukubwa hatimae maambukizi hayo hulikumba tunda lote la nanasi. Ukifikia hatua hiyo majani ya juu ya tunda la nanasi hukauka. Pia matunda machanga yakiathirika na ugonjwa huu husaabisha matunda kudumaa na kushindwa kutengeneza majani ya juu (Crowns).

Namna ya kudhibiti
  • Hakikisha shamba lako ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu ndani na nje ya shamba kwani kuna baadhi ya magugu yanaongeza kiwango cha Thrips wanaosambaza virusi wa ugonjwa huu.
  • Ondoa mimea yote shambani inayoonyesha dalili za awali za ugonjwa huu, hii itasaidia kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu kwa mimea isiyokua na ugonjwa.
  • Wadhibiti Thrips kwa kutumia dawa mbalimbali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
MAVUNO
Nanasi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 17 (mwaka 1 na miezi 5) hadi miezi 28 (miaka 2 na miezi 4) tangu kupanda vikonyo, itategemeana na aina ya nanasi na aina ya vikonyo ulivyotumia kupanda. Nanasi zilizotayari kuvunwa huvunjika sehemu ya shina la tunda lilipoegamia, Wakati wa kuvunwa nanasi hukatwa sehemu ya shina kwa kisu kikali na kuacha shina ambalo baadae hupunguzwa hadi sentimita 3.4

Matunda ya nanasi yanayotegemewa kuuzwa kwenye masoko ya karibu inatakiwa yavunwe yakiwa yameiva vizuri au yakiwa na rangi ya njano. Kama ni kwa ajili ya kusafirisha umbali mrefu au kwa ajili ya kuuza nje ya nchi  inatakiwa yavunwe yakiwa na rangi ya kijani iliyochangamana na njano au yakiwa yanaelekea kuwa rangi ya njano.

Baada ya kuvuna ondoa vikonyo vyote aina ya 'Slips' na ubakize kikonyo kimoja au viwili vilivyo na afya, ukiacha machipukizi mengi utapunguza ukubwa wa tunda litakalovunwa baadae. Vikonyo vyote vilivyotolewa (Suckers na Slips) vitatumika tena kupandia kwa msimu unaofwata.

Picha: Shamba la nanasi lililotunzwa vizuri      Photo Credit: www.loopjamaica.com

Shamba la nanasi lililohudumiwa vizuri huzarisha mpaka Tani 70 kwa Hekta moja (70 Tonnes/Ha) au Tani 28 kwa Ekari moja (28 Tonnes/Acre)

<<< SEHEMU YA TATU

MWISHO WA MAKALA HII

Kama una swali, maoni au ushauri wowote kuhusu makala hii usisite kuweka ujumbe wako hapo chini, Karibu sana!.

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

2 Comments

  1. Hongera sana kwa makala nzito na inayojitosheleza sana nimepitia makala nyingi sana na mbalimbali zinazohusiana na kilimo cha nanasi but this content is contented.hongera sana.

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post