Kilimo bora cha Nanasi - Sehemu ya Tatu (Growing Pineapple - Part Three)


SEHEMU YA TATU

3. Thrips (Thrips tabaci and Frankliniella schultzei)
Hawa ni wadudu wadogo wanaofikia urefu hadi mm 1.5, wembamba, wana rangi ya kahawia iliyochangamana na njano, mabawa yake yenye rangi ya njano hufunika sehemu ya nyuma ya mwili wake kipindi ambapo mdudu huyu amepumzika. Mdudu huyu akikomaa (Adult thrips) huwa na mabawa angavu yanayong'aa.

Thrips hawa hususani wale wanaovamia Vitunguu (Onion thrips - Thrips tabaci) na wale wanaovamia zao la Pamba (blossom or cotton bud thrips - Frankliniella schultzei), wote hawa ni wadudu hatari sana kwa uzalishaji wa nanasi kwani husambaza ugonjwa wa "Madoa manjano" (Yellow spot virus) unaosababishwa na virusi.

Photo Credit: www.canr.msu.edu

Jamii ya Thrip anayekula maua (Blossom thrip) husababisha ulemavu wa tunda unaoitwa "Dead eye". Thrip anayekula majani ya juu ya tunda (Crowns) husababisha michilizi kwenye majani hayo "Concentric ring patterns"). 

Namna ya kudhibiti
  • Dhibiti magugu shambani kwako na kuhakikisha shamba lako linakua safi wakati wote, kwani baadhi ya magugu huongeza kiwango cha wadudu hawa.
  • Waangamize wadudu hawa kwa kutumia dawa mbalimbali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo. Ukiwaangamiza wadudu hawa unaondoa uwezekano wa mmea kupata ugojwa wa virusi "Yellow spot virus".
  • Watunze wadudu rafiki wanaokula thrips kama Predatory thrips, Lacewings na Predatory bugs. Usitumie dawa za wadudu zinazoangamiza wadudu rafiki (Natural enemies).
  • Pia unaweza ukatumia dawa za asili (Botanicals or Biopesticides) kwa kupulizia kama; Juisi ya Vitunguu swaumu, juisi ya pareto (pyrethrum), mchanganyiko wa juisi ya vitunguu swaumu na pilipili kichaa, pia Juisi ya Rotenone (Hii ni jamii ya mkunde unaotambaa ambao ni sumu kwa binadamu na wanyama), tazama picha hapo chini kuona mkunde huu.

  • Dawa hizi za asili zimeripotiwa kufanya vizuri kwa kuwaangamiza thrips. Pia "Spinosad", dawa iliyotengenezwa kutokana na bakteria (a bacteria derivative) nayo hufaa sana kuwaangamiza thrips.

B: MAGONJWA
Zao la nanasi hukumbwa na magonjwa mara chache sana kama utatunza shamba lako vizuri. Magonjwa yaliyomengi hutokana na wadudu waharibifu

1. Kuoza sehemu ya juu ya nanasi na kuoza mizizi [Blossom or cotton bud thrips (Frankliniella schultzei) top and root rot (Phytophtora cinnamomi and P. nicotianae var. parasitica)]

1.1. Kuoza sehemu ya juu ya nanasi (Top rot)
Ugonjwa huu husababisha majani ya juu kubadilika rangi kutoka kijani kwenda njano au kahawia yenye vijisehemu vyekundu. Sehemu za mwisho za majani hujikunja na huwa rahisi kupukutika. Kwa ndani shina na sehemu ya viungio vya majani huwa laini, hatimae huoza na kutoa harufu mbaya.

1.2. Kuoza mizizi (Root rot)
Kwa upande wa kuoza mizizi, dalili zake hufanana na kuoza juu ya nanasi isipokua majani ya nje huwa yanalegea na kuinama pia sehemu za mwisho za jani hunyauka, kwa hatua hii mizizi ya nanasi inakua imeshaoza na unaweza ukaung'oa mmea kwa urahisi. Mara nyingine Kuoza mizizi kunaweza kukaendelea na kusababisha kuoza juu ya nanasi (Top rot). Matunda ya nanasi yaliyotoka kwenye mmea wenye maambukizi huwa ni madogo na yanakosa soko.

Photo Credit: www.mindenpictures.com

 Photo Credit: www.growables.org

  Photo Credit: www.growables.org

 Photo Credit: www.growables.org

Namna ya kudhibiti
  • Usipande zao lako kwenye udongo unaotwamisha maji (waterlogging)
  • Boresha udongo wa shamba lako kwa kubadilisha mazao na kuongeza mbolea za asili kama samadi na mboji.
2. White leaf spot (Ceratocystis paradoxa, Thielaviopsis paradoxa)
Ugonjwa huu husababishwa na fangasi aina ya Ceratocystis paradoxa ambao husababisha majani kuwa na madoa meupe, kuwa na uozo wenye rangi nyeusi na vivimbe vyenye majimaji juu ya majani. Baadae majani huwa membamba kama karatasi na huwa na rangi ya kahawia.

Pia ugonjwa wa kuoza majani ya nanasi (Base or but rot of pineapple) mara nyingi huvikumba vikonyo vya kupandikiza shambani kama Crowns, Slips na Suckers. Vikonyo hivi huoza kama havikukauka vizuri kabla ya kupanda

Pia vimelea hivi vya fangasi huikumba mimea ya nanasi iliyokomaa (Older plants) baada ya kuingia kupitia majeraha ya nanasi yaliyotokana na shughuli mbalimbali za shamba kama palizi n.k. Hali ikizidi sana mmea hubadirika rangi na kua mweusi na kuoza ndani ya siku 2 au 3.

Ugonjwa huu (Black rot), hutokea baada ya mavuno (Post-harvest), Matunda ya nanasi yaliyojeruhiwa ndio hupata ugonjwa huu ukiambatana na rangi nyeusi ikiwa na uoto wa fangasi (mycelium develops), pia uoto huo huchangamana na vivimbe vyenye majimaji.

Namna ya kudhibiti
  • Tumia vikonyo vya kupanda vyenye afya na vya aina moja na umri sawa.
  • Chagua vikonyo vyenye maotea (nodes) angalau sehemu tatu, ili kuongeza uharaka wa kuota
  • Aina za vikonyo ambazo huchelewa kuota inatikiwa zitibiwe na maji ya moto yenye nyuzi joto 50°C kwa masaa mawili (Loweka kwa masaa mawili).
  • Epuka kuiacha ardhi ikiwa kavu sana au yenye maji sana (Extremely Wet or dry soil conditions)
  • Usipande vikonyo vibichi vilivyoandaliwa punde, hakikisha vinakaushwa vizuri kabla ya kupanda.
  • Kuepuka kusambaza ugonjwa kwa mimea iliyo na afya, hakikisha haujeruhi vikonyo au mimea iliyoota, pia mimea iliyoathirika iondolewe shambani na kuchomwa moto.
  • Kama shamba lako linatwamisha maji, tengeneza mifereji ya kuondosha maji shambani, pia jitahidi kutopanda mimea yako wakati wa unyevu mwingi.

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post