Hawa ni wadudu wadogo wanaofikia
urefu hadi mm 1.5, wembamba, wana rangi ya kahawia iliyochangamana na njano,
mabawa yake yenye rangi ya njano hufunika sehemu ya nyuma ya mwili wake kipindi
ambapo mdudu huyu amepumzika. Mdudu huyu akikomaa (Adult thrips) huwa na mabawa
angavu yanayong'aa.
Thrips hawa hususani wale
wanaovamia Vitunguu (Onion thrips - Thrips tabaci) na wale wanaovamia zao la
Pamba (blossom or cotton bud thrips - Frankliniella schultzei), wote hawa ni
wadudu hatari sana kwa uzalishaji wa nanasi kwani husambaza ugonjwa wa
"Madoa manjano" (Yellow spot virus) unaosababishwa na virusi.
Photo Credit: www.canr.msu.edu
Jamii ya Thrip anayekula maua (Blossom thrip) husababisha
ulemavu wa tunda unaoitwa "Dead eye". Thrip anayekula majani ya juu
ya tunda (Crowns) husababisha michilizi kwenye majani hayo "Concentric
ring patterns").
Namna ya kudhibiti
- Dhibiti magugu shambani kwako na kuhakikisha shamba lako linakua safi wakati wote, kwani baadhi ya magugu huongeza kiwango cha wadudu hawa.
- Waangamize wadudu hawa kwa kutumia dawa mbalimbali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo. Ukiwaangamiza wadudu hawa unaondoa uwezekano wa mmea kupata ugojwa wa virusi "Yellow spot virus".
- Watunze wadudu rafiki wanaokula thrips kama Predatory thrips, Lacewings na Predatory bugs. Usitumie dawa za wadudu zinazoangamiza wadudu rafiki (Natural enemies).
- Pia unaweza ukatumia dawa za asili (Botanicals or Biopesticides) kwa kupulizia kama; Juisi ya Vitunguu swaumu, juisi ya pareto (pyrethrum), mchanganyiko wa juisi ya vitunguu swaumu na pilipili kichaa, pia Juisi ya Rotenone (Hii ni jamii ya mkunde unaotambaa ambao ni sumu kwa binadamu na wanyama), tazama picha hapo chini kuona mkunde huu.
- Dawa hizi za asili zimeripotiwa kufanya vizuri kwa kuwaangamiza thrips. Pia "Spinosad", dawa iliyotengenezwa kutokana na bakteria (a bacteria derivative) nayo hufaa sana kuwaangamiza thrips.
B: MAGONJWA
Zao la nanasi hukumbwa na magonjwa
mara chache sana kama utatunza shamba lako vizuri. Magonjwa yaliyomengi
hutokana na wadudu waharibifu
1. Kuoza sehemu ya juu ya
nanasi na kuoza mizizi [Blossom or cotton bud thrips (Frankliniella schultzei)
top and root rot (Phytophtora cinnamomi and P. nicotianae var. parasitica)]
1.1. Kuoza sehemu ya juu ya nanasi
(Top rot)
Ugonjwa huu husababisha majani ya juu kubadilika rangi
kutoka kijani kwenda njano au kahawia yenye vijisehemu vyekundu. Sehemu za
mwisho za majani hujikunja na huwa rahisi kupukutika. Kwa ndani shina na sehemu
ya viungio vya majani huwa laini, hatimae huoza na kutoa harufu mbaya.
1.2. Kuoza mizizi (Root rot)
Kwa upande wa kuoza mizizi, dalili zake hufanana na kuoza
juu ya nanasi isipokua majani ya nje huwa yanalegea na kuinama pia sehemu za
mwisho za jani hunyauka, kwa hatua hii mizizi ya nanasi inakua imeshaoza na
unaweza ukaung'oa mmea kwa urahisi. Mara nyingine Kuoza mizizi kunaweza
kukaendelea na kusababisha kuoza juu ya nanasi (Top rot). Matunda ya nanasi
yaliyotoka kwenye mmea wenye maambukizi huwa ni madogo na yanakosa soko.
Photo Credit: www.mindenpictures.com
Namna ya kudhibiti
- Usipande zao lako kwenye udongo unaotwamisha maji (waterlogging)
- Boresha udongo wa shamba lako kwa kubadilisha mazao na kuongeza mbolea za asili kama samadi na mboji.
2. White leaf spot (Ceratocystis
paradoxa, Thielaviopsis paradoxa)
Ugonjwa huu husababishwa na fangasi aina ya Ceratocystis
paradoxa ambao husababisha majani kuwa na madoa meupe, kuwa na uozo wenye rangi
nyeusi na vivimbe vyenye majimaji juu ya majani. Baadae majani huwa membamba
kama karatasi na huwa na rangi ya kahawia.
Pia ugonjwa wa kuoza majani ya nanasi (Base or but rot of pineapple) mara nyingi huvikumba vikonyo
vya kupandikiza shambani kama Crowns, Slips na Suckers. Vikonyo hivi huoza kama
havikukauka vizuri kabla ya kupanda
Pia vimelea hivi vya fangasi huikumba mimea ya nanasi
iliyokomaa (Older plants) baada ya kuingia kupitia majeraha ya nanasi
yaliyotokana na shughuli mbalimbali za shamba kama palizi n.k. Hali ikizidi
sana mmea hubadirika rangi na kua mweusi na kuoza ndani ya siku 2 au 3.
Ugonjwa huu (Black rot), hutokea baada ya mavuno
(Post-harvest), Matunda ya nanasi yaliyojeruhiwa ndio hupata ugonjwa huu
ukiambatana na rangi nyeusi ikiwa na uoto wa fangasi (mycelium develops), pia
uoto huo huchangamana na vivimbe vyenye majimaji.
Namna ya kudhibiti
- Tumia vikonyo vya kupanda vyenye afya na vya aina moja na umri sawa.
- Chagua vikonyo vyenye maotea (nodes) angalau sehemu tatu, ili kuongeza uharaka wa kuota
- Aina za vikonyo ambazo huchelewa kuota inatikiwa zitibiwe na maji ya moto yenye nyuzi joto 50°C kwa masaa mawili (Loweka kwa masaa mawili).
- Epuka kuiacha ardhi ikiwa kavu sana au yenye maji sana (Extremely Wet or dry soil conditions)
- Usipande vikonyo vibichi vilivyoandaliwa punde, hakikisha vinakaushwa vizuri kabla ya kupanda.
- Kuepuka kusambaza ugonjwa kwa mimea iliyo na afya, hakikisha haujeruhi vikonyo au mimea iliyoota, pia mimea iliyoathirika iondolewe shambani na kuchomwa moto.
- Kama shamba lako linatwamisha maji, tengeneza mifereji ya kuondosha maji shambani, pia jitahidi kutopanda mimea yako wakati wa unyevu mwingi.
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
إرسال تعليق