Mmea ulioathirika huwa na rangi ya njano iliyochangamana na
rangi nyekundu mwishoni mwa pembe za majani (leaf tips), baadae hali hii
hulikumba jani zima. Hali hii pia husambaa kwa majani mengine, majani
yaliyobadilika rangi hunyauka.
Mmea ulioathirika sana hudumaa na hutoa matunda madogo na
yasiyokomaa, madhara ya kwanza hutokea kwenye mizizi ambapo husimama kukua na
baadae huoza. Hali hii husababisha majani kukauka mithiri ya hali ya ukame.
Namna ya kudhibiti
- Tumia vikonyo vya kupandia vilivyotoka kwenye mmea wenye afya ambao haukuonyesha dalili yoyote ya kunyauka
- Wadhibiti wadudu aina ya Mealybugs (Namna ya kudhibiti wadudu hawa, rejea hapo juu kwenye kipengele cha wadudu waharibifu.)
- Tibu vikonyo vya kupanda kwa kutumia maji ya moto yenye nyuzi joto 50°C, loweka vikonyo hivyo kwenye maji hayo kwa dakika 30. Hatua hii huondoa ugonjwa huu wa virusi pamoja na makoloni ya mealybugs kwa asilimia 100%. Vikonyo vilivyotibiwa na maji ya moto hukua haraka sana kuliko ambavyo havijatibiwa.
- Utafiti umebaini kwamba mimea iliyotokana na vikonyo vilivyotibiwa na maji ya moto, haipatati ugonjwa huu wa virusi au kukumbwa na mealybugs kwa zaidi ya miaka miwili tangu kupandwa kwenye shamba lilikoathirika sana na ugonjwa huu (Mealybug wilt).
- Panda aina ya nanasi inayovumilia ugonjwa huu kama Singapore spanish (Red Spanish), aina kama Cayenne na Masmerah huathiriwa sana na ugonjwa huu.
4. Yellow spot virus
Ugonjwa huu hufanana sana na ule unaoathiri zao la nyanya
(Tomato spotted wilt virus). Ugonjwa huu huathiri zaidi ya mamia ya aina
mbalimbali za mimea ikiwemo Pilipili, Nyanya, Tumbaku, Bilinganga, Viazi mviringo,
Jamii yote ya Maharage, Spinachi n.k.
Magugu aina mbalimbali yamekua yakitunza virusi hawa kama Machoma nguo (Black jack, Bidens pilosa), Emilia sonchifolia na Datura stramonium, Tazama picha hapa chini kuyafahamu magugu haya;
Photo Credit: www.researchgate.net
Magugu aina mbalimbali yamekua yakitunza virusi hawa kama Machoma nguo (Black jack, Bidens pilosa), Emilia sonchifolia na Datura stramonium, Tazama picha hapa chini kuyafahamu magugu haya;
B: EMILIA SONCHIFOLIA
Photo Credit: www.flickr.com
Photo Credit: www.commons.wikimedia.org
Photo Credit: www.weeds.brisbane.qld.gov.au
C: DATURA STRAMONIUM (JIMSON WEED)
Photo Credit: www.worldseedsupply.com
Photo Credit: www.rhs.org.uk
Photo Credit: www.plantsam.com
Photo Credit: www.monaconatureencyclopedia.com
Wadudu wanaosambaza virusi hawa wanaitwa Thrips, kuwaelewa zaidi rejea kipengele cha wadudu waharibifu. Kama magugu hayo niliyaekezea hapo juu yakaota karibia na mmea wa nanasi, basi utapata ugonjwa huu haraka sana kwa sababu wadudu hawa (Thrips) wanahama kutoka maeneo yenye magugu haya kwenda kwenye shamba la nanasi. Vilevile upepo unaweza ukawabeba wadudu hawa na kuwasafirisha umbali mrefu, pia ikawa ni chanzo kimojawapo cha kusambaza virusi wa ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa za ugonjwa huu ni pamoja na Tunda la
nanasi kuwa jeusi (Blackened), huwa linakuwa na uwazi kwa ndani uliokauka (Dry
cavity) kutokana na moja wapo macho ya tunda la nanasi kufa, Hali hii huitwa
"Macho yaliyokufa" (Dead eye). Macho ya tunda la nanasi ni kama
vijisehemu kwenye tunda la nanasi kama vina uwazi fulani hivi.
Ugonjwa huu husababisha madoa
madoa yenye rangi ya njano ambayo baadae yanaongezeka ukubwa hatimae maambukizi
hayo hulikumba tunda lote la nanasi. Ukifikia hatua hiyo majani ya juu ya tunda
la nanasi hukauka. Pia matunda machanga yakiathirika na ugonjwa huu
husaabisha matunda kudumaa na kushindwa kutengeneza majani ya juu (Crowns).
Namna ya kudhibiti
- Hakikisha shamba lako ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu ndani na nje ya shamba kwani kuna baadhi ya magugu yanaongeza kiwango cha Thrips wanaosambaza virusi wa ugonjwa huu.
- Ondoa mimea yote shambani inayoonyesha dalili za awali za ugonjwa huu, hii itasaidia kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu kwa mimea isiyokua na ugonjwa.
- Wadhibiti Thrips kwa kutumia dawa mbalimbali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
MAVUNO
Nanasi huwa tayari kuvunwa baada
ya miezi 17 (mwaka 1 na miezi 5) hadi miezi 28 (miaka 2 na miezi 4) tangu
kupanda vikonyo, itategemeana na aina ya nanasi na aina ya vikonyo ulivyotumia
kupanda. Nanasi zilizotayari kuvunwa huvunjika sehemu ya shina la tunda
lilipoegamia, Wakati wa kuvunwa nanasi hukatwa sehemu ya shina kwa kisu kikali
na kuacha shina ambalo baadae hupunguzwa hadi sentimita 3.4
Matunda ya nanasi yanayotegemewa
kuuzwa kwenye masoko ya karibu inatakiwa yavunwe yakiwa yameiva vizuri au
yakiwa na rangi ya njano. Kama ni kwa ajili ya kusafirisha umbali mrefu au kwa
ajili ya kuuza nje ya nchi inatakiwa
yavunwe yakiwa na rangi ya kijani iliyochangamana na njano au yakiwa yanaelekea
kuwa rangi ya njano.
Baada ya kuvuna ondoa vikonyo vyote aina ya 'Slips' na
ubakize kikonyo kimoja au viwili vilivyo na afya, ukiacha machipukizi mengi
utapunguza ukubwa wa tunda litakalovunwa baadae. Vikonyo vyote vilivyotolewa
(Suckers na Slips) vitatumika tena kupandia kwa msimu unaofwata.
Picha: Shamba la nanasi lililotunzwa vizuri Photo Credit: www.loopjamaica.com
Shamba la nanasi lililohudumiwa vizuri huzarisha mpaka Tani
70 kwa Hekta moja (70 Tonnes/Ha) au Tani 28 kwa Ekari moja (28 Tonnes/Acre)
<<< SEHEMU YA TATU
<<< SEHEMU YA TATU
MWISHO WA MAKALA HII
Kama una swali, maoni au ushauri
wowote kuhusu makala hii usisite kuweka ujumbe wako hapo chini, Karibu sana!.
Hongera sana kwa makala nzito na inayojitosheleza sana nimepitia makala nyingi sana na mbalimbali zinazohusiana na kilimo cha nanasi but this content is contented.hongera sana.
ردحذفAsante sana, Karibu sana!
حذف- Lusubilo A. Mwaijengo
إرسال تعليق