Ufugaji wa Kuku wa Mayai - Sehemu ya Nne (Layer Poultry Farming - Part Four)


SEHEMU YA NNE

KULEA NA KUWAKUZA VIFARANGA
Yafwatayo ni maelekezo muhimu sana ya kuwalea na kuwakuza vifaranga wako na Inakupasa uyafwate vema;
  • Inatakiwa uwatunze kwa uangalifu vifaranga wako mpaka watakapofikia wiki 4 hadi 5.
  • Baada ya kuwatoa vifaranga wako kwenye eneo maalumu la kuwalea (Brooder), wapatie chakula kizuri (Pellet Feed), Wakipatiwa chakula hiki kizuri itawasaidia sana mbeleni, Wakikua watataga sana mayai, pia watakua na afya nzuri na wataongezeka uzito. Kwa hiyo wakati wa ukuaji ni muhimu sana kuwapatia chakula bora.
KUKATA MIDOMO YA KUKU NA UMUHIMU WAKE
Kukata au kupunguza midomo ya kuku wa mayai ni muhimu sana. Zifuatazo ni faida muhimu za kuwakata kuku midomo;
  • Ukataji wa midomo husaidia kupunguza hali ya kuku kudonoana.
  • Husaidia kuzuia upotevu wa chakula.
  • Vilevile husaidia kupunguza tabia ya kudonoa mayai.
Namna ya kuwakata kuku midomo
  • Wakate vifaranga wako midomo wakifikia umri wa siku 8 hadi 10.
  • Wakate tena midomo wakishakua wakifikia umri wa wiki 8 hadi 12.
  • Kwa vifaranga wakate sm 0.2 kutoka kwenye pua.
  • Kwa kuku wanaokua wakate sm 0.45 kutoka kwenye pua.
  • Wakate midomo yote wa juu na wa chini, cha msingi zingatia kipimo sahihi cha kukata.
  • Usikate midomo yote miwili kwa pamoja, kata mmoja baada ya mwingine.
  • Tumia mkasi maalumu wa kukatia midomo
  • Usiwakate midomo siku mbili baada au kabla ya kuwapa chanjo, au kabla au baada ya kuwapatia dawa ya kutibu magonjwa kama Salfa (Sulfur).
  • Usiwakate midomo ikiwa kuku wamebanwa au wamefungwa vibaya, pia wakati kuna hali ya hewa mbaya na wakati kuku wameanza kutaga mayai (Wakate wiki ya 8 hadi 12 kabla ya kuanza kutaga mayai)
  • Siku tatu kabla ya kuwakata midomimo wapatie kuku wako maji ya kunywa yaliyochanganywa na vitamin "K".
  • Osha kifaa cha kukatia midomo kwa kutumia dawa maalumu ya kuua vimelea (Antiseptic).
  • Hakikisha unachunguza makali na joto la wembe wa kifaa cha kukatia midomo kabla ya kuanza zoezi.
  • Inatakiwa uwe makini sana, usidhuru macho na ulimi wa kuku.
  • Kata midomo ya kuku wakati kuna hali ya hewa ya baridi.
  • Baada ya kuwakata midomo wapatie maji ya kunywa,  pia wapatie baadhi ya vyakula vya kuongeza nguvu.
Photo Credit: wikihow.com

KUWAPA CHAKULA
Kuna makampuni mengi ya kutengeneza chakula cha kuku wa mayai ulimwengu mzima. Kwa hiyo unaweza ukanunua chakula kwa hao watengenezaji au ukatengeneza mwenyewe nyumbani kwako. Kama utanunua au utatengeneza mwenyewe lazima uhakikishe kwamba unapata chakula chenye ubora na chenye virutubisho vyote muhimu. Kirutubisho cha Protini na Madini ni muhimu sana kwa kuku wa mayai.

Wapatie madini ya Calcium 2% kwa wiki mbili baada ya kuzaliwa. Kama utaona hawaongezeki uzito kama inavyotakiwa, wapatie Chakula cha kuanzia (Starter feed) kwa wiki 8, wape mara 2 au mara 3 kwa siku hadi kufikia umri wa wiki 18.

Uhitaji wa chakula kwa kuku wa mayai huongezeka kwa kasi sana pale wanapoanza kutaga.

Wapatie chakula kulingana na umri na uzito wao, pia usipunguze kiasi cha chakula wakati wanaendelea kutaga hata kama uzito wao ukiongezeka

Kulingana na umri na aina ya kuku, Namna tofauti ya utoaji wa chakula huathiri sana uzito wa kuku (Kupungua au kuongezeka uzito). Wapatie vyakula vyenye mchanganyiko wa madini mbalimbali kama Calcium, Phosphorus, Vitamins, Amino acid na virutubisho vingine.

*Kiasi cha Chakula kinachotakiwa kuwapa kuku wako kulingana na Umri*

1. Chakula cha Vifaranga (Chick Mash)
Wapatie chakula hiki cha vifaranga kiasi cha gramu 35 hadi 75 kwa kifaranga mmoja na kwa siku moja (35 to 75g/chick/day) kuanzia siku 0 hadi siku 7 (wiki 1). Unatakiwa uongeze chakula taratibu hadi kufikia gramu 75 kwa kuku mmoja na kwa siku moja, kwahiyo utawapatia kuku wako kwa miezi sita zaidi kiasi cha gramu 75 kwa kuku mmoja na kwa siku moja (75g/bird/day).

2. Chakula cha kuku wanaokua (Growers Mash)
Wapatie chakula hiki baada ya Wiki sita za Chick mash kuisha, wapatie kiasi cha gramu 75 hadi 110 kwa kuku mmoja na kwa siku moja (75 to 110g/bird/day) kwa muda wa wiki 14, hadi kufikia wiki ya 20 (Kuku wa mayai wanaanza kutaga wakifikia wiki 20)

3. Chakula cha kuku wanaotaga (Layers Mash)
Wapatie chakula hiki kuku wanaotaga kiasi gramu 110 hadi 140 kwa kuku mmoja na kwa siku moja (110 to 140g/bird/day) kuanzia umri wa wiki 20 na kuendelea. Hakikisha chakula unachowapa kina ubora wenye kiwango cha juu.

NB:
Epuka kufanya mabadiliko ya ghafra ya chakula kama aina ya chakula na muda wa kuwapa chakula, Mabadiliko haya ya ghafra huathiri Utagaji wa mayai. Wapatie kuku wako maji safi na salama kila siku.

<<< SEHEMU YA TATU


Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post