Kilimo bora cha Karanga - Sehemu ya Nne (Growing Groundnuts - Part Four)


SEHEMU YA NNE

7. Groundnut leafminer (Aproaerema modicella)
Hawa ni viwavi wadogo wenye rangi ya kijani iliyochangamana na njano pia huwa na kichwa cheusi kinachong'aa, viwavi hawa hufikia urefu wa mm 0.56. Viwavi hawa hutokana na aina fulani ya vipepeo ambao hufikia urefu wa mm 18, yaani vipepeo hawa hutaga mayai kwenye majani (Chini ya jani) baada ya muda mayai hayo huanguliwa na kua viwavi.

Photo Credit: www.www.nbair.res.in

Athari
  • Viwavi hawa hula majani kwa kutoboa katikati ya jani, kufwata ulalo wa jani yaani katikati ya ngozi ya juu na ngozi ya chini ya jani. Jani lililotobolewa hufa baada ya siku chache.
  • Kutokana na udogo wa viwavi hawa wanavyokua katikati ya jani huwezi kuwaona, ila kadiri wanavyokua huongezeka mwili hivyo husababisha ngozi ya juu au ya chini ya jani kupasuka, hatimae viwavi hawa huonekana chini au juu ya majani baadae hujiviringisha kwenye utando wa jani. Baada ya kujiviringisha na kuning'inia chini ya jani huendelea kula majani mpaka pale watakapobadilika kuwa 'Buu' (Hii ni hatua ya tatu ya ukuaji wa mdudu baada ya Yai na Kiwavi, hatua hii ni kama mdudu amekufa lakini huendelea kubadilika polepole na kua mdudu kamili ambae baadae tena hutaga mayai).
  • Majani yaliyoliwa hubadirika rangi na kuwa Kahawia (Brownish), pia hujikunja mithiri ya kuviringishwa na hukauka. Hali hii husababisha mmea kupukutisha majani mapema, ukuaji wa mmea huathiriwa na hupunguza kiwango cha mavuno.
Namna ya kudhibiti
  • Tumia aina za mbegu zinazovumilia uharibifu wa wadudu hawa.
  • Panda mapema kulingana na kalenda ya hali ya hewa ya eneo lako, hali hii husaidia mmea kukua vizuri kipindi ambacho kuna kiwango kidogo cha viwavi hawa,  pia kuepusha mmea kukumbana na kipindi cha ukame katikati ya msimu, Mmea wenye ukame hukumbwa zaidi na viwavi hawa kuliko mmea usio na ukame au unaomwagiliwa.
8. Root-knot nematodes
Hawa ni minyoo wadogo waishio kwenye udongo, huishi karibu na mizizi ya mimea mbalimbali ikiwemo karanga.

Picha: Mzizi wa karanga ulioathiriwa na minyoo hawa

"d2549-1" flickr photo by USDAgov  shared under a Creative Commons (BY) license
Picha: Mnyoo wa Nematode akipenyeza kwenye mzizi wa karanga

Athari
Husababisha mizizi ya karanga kuwa na vinundu, hali itakayopelekea mmea kudumaa na hatimae kukauka.

Namna ya kudhibiti
Badilisha mazao kwa kubadilishana na mimea jamii ya nafaka.

9. Spider mites (Tetranychus spp.)
Hawa ni aina ya buibui wadogo wenye rangi nyekundu au njano, hutoa utando kama buibui wa kawaida. Wadudu hawa huzaliana kwa kasi sana, huvamia majani ya karanga na mazao mengine ya mbogamboga.

Picha: Spider mites wamelizunguka jani

Picha: Spider mite akiwa peke yake

Athari
  • Wadudu hawa huvamia majani na huzaliana kwa kasi kipindi cha kiangazi au kipindi cha ukame. Wakivamia majani huanza kufyonza majimaji ya kwenye majani, hatimae majani hua na madoa madoa meupe na upande wa juu wa jani hua na utando mweupe kama ule wa buibui wa kawaida, ila utando wao unakua laini sana.
  • Athari ikizidi husababisha majani kukauka, hatimae mmea hudumaa na mavuno hupungua kwa kiasi kikubwa.
Namna ya kudhibiti
Tunza mimea yako vizuri, kwani mimea yenye afya huathiriwa kidogo sana na wadudu hawa. Pia hakikisha shamba lako lina unyevu wa kutosha wakati wote kwani hali ya ukame huongeza kasi ya uharibifu ya wadudu hawa.


>>> SEHEMU YA TANO

Makala na: Lususbilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post