Ufugaji wa Kuku wa kienyeji - Sehemu ya Saba (Indigenous Chicken Farming - Part Seven)


SEHEMU YA SABA

1. CHAWA, VIROBOTO NA UTITIRI WA KUKU
Wadudu hawa huathiri ustawi wa kuku kwa asilimia kubwa, humfanya kuku kutotulia bandani na afya yake hudhoofu. Pia hushambulia vifaranga na kusababisha vifo vingi, Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani sana lakini nao huathiriwa sana.

Dalili za kuwa na wadudu hawa
  • Kuku kutochangamka
  • Ukuaji mdogo wa kuku
  • Kuku kutotaga na kutoatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto (Kuku hatulii kwenye kiota chake)
  • Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu
Namna ya kudhibiti
  • Hakikisha banda la kuku linakua safi wakati wote
  • Tumia dawa mbalimbali za kudhibiti wadudu hawa kama za Unga au za maji, pia hakikisha unatumia dozi sahihi kama inavyotakiwa kitaalamu.
  • Badilisha mapumba ya mpunga au malanda kila yanapolowana.
  • Kama viriboto wamewakumba kuku maeneo ya usoni, wapake mafuta ya taa kwa kutumia kitambaa laini, ukifanya hivyo viroboto hao watakufa baada ya muda mfupi. Usafi wa banda ni muhimu sana kudhibiti wadudu hawa.
  • Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.
TAZAMA PICHA ZIFUATAZO KUWAFAHAMU WADUDU HAWA

A: CHAWA

Picha: Muonekano wa chawa kwa kutumia Hadubini (Microscope)

 Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

  Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

 Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

B: VIROBOTO

 Picha: Muonekano wa Kiroboto kwa kutumia Hadubini (Microscope)

  Picha: Muonekano wa Kiroboto kwa kutumia Hadubini (Microscope)

Picha: Viroboto wakiwa kwenye mwili wa kuku

C: UTITILI

 Picha: Muonekano wa Utitili kwa kutumia Hadubini (Microscope)

 Picha: Utitili na Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

Picha: Utitili na Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

2. MINYOO YA KUKU
Viumbe hawa hukaa ndani ya mwili wa kuku hususani kwenye mfumo wa chakula wa kuku, minyoo hao ni kama Roundworms, Tapeworms, gapeworms n.k

Dalili za minyoo
  • Kuku hukonda
  • Kuku huarisha
  • Kuku hukohoa
  • Kuku hupunguza utagaji
  • Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
  • Kuku hupungua uzito

Namna ya kudhibiti
  • Hakikisha unawapa chakula na maji katika nazingira ya usafi
  • Wapatie dawa za minyoo kama inavyotakiwa kitaalamu kila baada ya miezi mitatu
 Picha: Kinyesi cha kuku chenye minyoo

Picha: Utumbo wa kuku wenye minyoo

3. UKOSEFU WA VITAMINI A
Huathiri sana kuku wadogo, kuku hao huwa na dalili zifuatazo;

Dalili za ukosefu wa vitamini
  • Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowana.
  • Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi
Namna ya kudhibiti
  • Wapatie kuku wote dawa za vitamini za kuku zinazouzwa kwenye maduka ya madawa ya mifugo
  • Wapatie majani mabichi ya aina mbalimbali au mboga za majani kama mchicha, chainizi n.k., Fanya hivi mara kwa mara hii itasaidia kuwakinga kuku wako na tatizo hili.
4. TABIA MBAYA ZA KUKU
Kuku huwa na tabia mbaya bandani kama kudonoa wenzake mpaka kuwasababishia majeraha, kupasua na kula mayai yake au ya kuku wengine n.k

Namna ya kudhibiti tabia hizi
  • Wapatie kuku majani ili waendelee kudonoa majani badala ya kudonoana wenyewe.
  • Watenge kuku wenye tabia hiyo na wengine, kwa sababu ukiwaacha wataambuza tabia hiyo kuku wengine
  • Kama tabia hiyo itaendelea, wapunguze midomo (De-beaking) kwa kutumia kifaa cha moto kama kisu au kifaa kingine.
 Picha: Kuku wakila yai

Picha: Usawa wa kupunguza mdomo(De-beaking),  Photo Credit: Wikihow.com
* MWISHO WA MAKALA HII *

Muhimu*
Kama umependa makala hii au makala zingine kwenye blogi hii na unapenda kumshirikisha mwenzako kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Google+ n.k., bofya batani hapo chini na utapelekwa moja kwa moja kwenye mitandao hiyo

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post