Kilimo cha Bilinganya - Sehemu ya nne (Growing Eggplant - Part four)


KILIMO CHA BILINGANYA 
SEHEMU YA 4 (MWISHO)

Magonjwa:
1. Mnyauko Bacteria (Bacteria Wilt)
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafra hasa wakati wa jua kali.



Mnyauko bakteria unaweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano.

Njia nyingine ni kupanda aina za bilinganya kama vile Matale, Kopek na Rosita ambazo huvumilia mashambulizi ya ugonjwa huu.

2. Phomopsis Vexans
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria na hushambulia majani, shina na matunda.







3. Verticillium Wilt

Huenezwa na maji na husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kuanguka.


Magonjwa ya Phomopsis Vexans na Verticillium Wilt yanaweza kuzuiwa kwa kung'oa na kuchoma moto mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha mazao na kuweka shamba katika hali ya usafi wakati wote.



KUVUNA
Bilinganya huanza kutoa matunda yaliyokomaa baada ya miezi miwili hadi mitatu tangu kupandikiza. Uvunaji huendelea kwa muda wa zaidi ya miezi minne na hauna budi hufanyike mapema mara matunda yanapokomaa. Matunda yaliyokomaa sana hayafai kuliwa kwa sababu huwa na kambakamba na mbegu zilizokomaa. Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa kutumia kisu kikali ili usiumize matunda.


MAVUNO
Kwa kawaida zao hili huzaa sana iwapo limetunzwa vizuri. Shamba lililotunzwa vizuri linaweza kutoa mavuno tani 50 hadi 60 kwa hekta. Hata hivyo mavuno mengi hutegemea aina ya bilinganya, umwagiliaji na rutuba ya udongo.



*** MWISHO WA MAKALA HII ***

***ENDELEA KUFWATILIA MAKALA ZINGINE***

Makala hii Imehaririwa mara ya mwisho Tarehe: 04/09/2016

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post