Habari ya majukumu ndugu wasomaji wangu?, Leo nimekuja na maada inayoelezea makosa mbalimbali ya kifedha tunayoyafanya kwenye maisha yetu ya kila siku. Watu wengi waliofanikiwa sana kiuchumi wanazungumzia jambo moja tu, nalo ni 'NIDHAMU YA FEDHA'. Jambo hili linameza ustaarabu wote wa matumizi ya fedha hata kama unapata kiasi kidogo tu kwa muda fulani. Kadiri unavyokua na nidhamu ya matumizi ya fedha ndivyo utakavyoona mabadiliko ya ukuaji wako wa uchumi kuongezeka. Yafuatayo ni baadhi ya makosa ya kifedha tunayofanya kila siku kwenye maisha yetu;
KOSA LA 1: KUANZA BIASHARA NA HELA YA MKOPO
Usikope pesa ya riba ili uanzishe
biashara. Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha
uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.
KOSA LA 2: MATUMAINI YA PESA USIYOKUWA NAYO
Usitumie pesa ambayo bado haipo
mikononi mwako. Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani. Kama kuna mtu
kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako" Basi wewe usiende kukopa
vitu kadhaa dukani au hata kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na wewe
umeahidiwa. Ni kosa. Unaweza kuingia
kwenye matatizo.
KOSA LA 3: KULA FAIDA YA BIASHARA
Kama unataka kuhifadhi/kutunza
pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza
kiasi kitakachosalia. Hivyo basi,
ukipata tu pesa, weka pembeni
kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi
kilichobaki.
KOSA LA 4: KUTOTAFUTA MAARIFA MAPYA YA BIASHARA
Ukipata nafasi ya kuonana na mtu
tajiri, kamwe usiombe pesa. Omba maarifa
ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo. Maarifa ndio mtaji wa kwanza. Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una
mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema,
"Omba ndoano, usiombe samaki"
KOSA LA 5: KUHIFADHI PESA PASIPO KUIZALISHIA
Usitunze mbegu badala ya
kuipanda. Watu wengi hufurahia pesa
wanayolipwa/kuipata kisha wanaiweka bank
au nyumbani bila kuiwekeza. Wekeza pesa ili uzalishe zaidi. Usiogope kuingia hasara, kila aliefanikiwa
alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa. Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata
matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa.
KOSA LA 6: KUMKOPESHA MTU PESA AMBAYE UNAAMINI HATORUDISHA
Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo
unahisi hatorudisha. Unapomkopesha mtu
huyo pesa, jiridhishe mwenyewe moyoni
kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi
kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri
aende bank akakope.
KOSA LA 7: KUMDHAMINI MTU AMBAYE HATOLIPA PESA ANAYODAIWA
Usikubali uwe shahidi , tena kwa
kusaini kabisa ili umdhamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile
unachomdhamini. Kumbuka kuwa, dhamana
maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa.
KOSA LA 8: KUTEMBEA NA PESA NYINGI ZISIZOKUA NA MATUMIZI
Epuka kutembea na pesa nyingi
ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo. Unaweza kujikuta unafanya matumizi
ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni. Ili
kuepuka haya, tembea na pesa uliyopanga
kuitumia katika safari yako. Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo
salama.
KOSA LA 9: KUTUNZA PESA MAENEO YASIYO SALAMA
Epuka kutunza pesa mahali pasipo
sahihi. Maeneo kama kwenye soksi, sidiria,
chini ya mto wa kulalia, chini ya
begi, kwenye kopo au hata kwenye begi la
safari, si maeneo salama. Ni rahisi
kusahau, kuibiwa au kupoteza pesa
zako. Ni bora ukatunza pesa
kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya
kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo
kwenye nguo zako hasa uwapo safarini.
KOSA LA 10: MATUMIZI YASIYOKUA YA LAZIMA
Usitumie pesa kwa kitu ambacho
hakikuwa kwenye ratiba yako. Jiulize kwanza kabla hujanunua, "Bila kitu
hiki, maisha yataenda au lah? Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha
kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.
Usiingiwe tamaa kwa kununua kitu
ambacho ungeweza kununua kwa bei ya punguzo mahali pengine zaidi. Labda tu uwe
una pesa nyingi.
KOSA LA 12: MATUMIZI KUZIDI MAPATO
Matumizi yako ya pesa yasizidi
pato lako. Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato
lako. Unapaswa kuwa bahili katika
matumizi yako. Cheza na pato lako. Fanya
matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka. Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya
mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa.
KOSA LA 13: KUKURUPUKA KUFANYA MAAMUZI
Una ndoto kubwa hapo baadae; labda
kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki.
Usikurupuke, ukanunua kitu cha ndoto
yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo. Usichanganye kati ya
mahitaji ya baadae na ya sasa. Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa
mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto. Hii itakuepushia kuingia katika
madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa. Jipange taratibu kutimiza ndoto
yako.
Kama umependa au umeguswa na maada hii, mshirikishe mwenzako kwenye mitandao ya kijamii kwa kubofya hapo chini batani za Facebook, twitter, Whatsapp n.k.
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Post a Comment