Kilimo Bora cha Pilipili kichaa - Sehemu ya Pili (Growing Chili pepper - Part Two)


KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA PILI

11. Anaheim
Aina hii hutokea nchini Marekani jimbo la California, imepewa jina la jiji maarufu linaloitwa 'Anaheim', California. Aina hii hufikia urefu wa sm 15 - 25, na mara nyingi hutumika zikiwa bado za kijani lakini pia huweza kutumika zikiwa nyekundu (zikiwa zimeiva). Aina hii hukomaa kwa siku 75 - 80. 

12. Ancho
Aina hii ina ukali wa wastani 

13. Ancho Ranchero
Aina hii pia ina ukali wa wastani 

14. Bahamian
Aina hii imetokea Amerika ya kati 'Bahamas', ni aina ndogo na ina umbile la mviringo hufikia urefu wa sm 2.5. Ina rangi tofauti kama njano, rangi ya chungwa, kijani na nyekundu pia ni kali sana. 

15. Banana
Aina hii ina ukubwa wa kati, ina ukali wa wastani huwa na rangi ya njano mpauko, ikikomaa huwa na rangi ya njano, nyekundu au rangi ya chungwa. 

16. Barker's
Ni aina ya pilipili jamii ya 'Anaheim' hufikia urefu wa sm 12 - 18 (Inchi 5 - 7) ni kali sana hupandwa sana nchini mexico. 

17. Bird's eye (Jicho la ndege)
Aina hii hufanana na ile inayotokea barani Afrika, aina hii ni ndogo sana hupandwa sana nchini Cambodia, Vietnam, Ufilipino na maeneo kuzunguka nchi hizi, lakini kwa sasa aina hii hupatikana ulimwengu mzima. Kama ilivyo aina ya 'African Bird's eye', aina hii pia huitwa 'Bird's eye' au 'Jicho la ndege' kwa sababu ya udogo wake wenye umbile la mviringo pia ni kwa sababu husambazwa kutoka eneo moja hadi hingine kwa ndege, hufikia urefu wa sm 2.5. 


18. Bishop's Crown
Aina hii hufanana na kofia ya wachungaji au maaskofu wa makanisa, ina muonekano wa kipekee sana ndo maana ikaitwa 'Bishop's Crown' yaani 'Kofia ya kiongozi wa kanisa au askofu'. Ina radha ya matunda, hufikia urefu wa sm 2.5 na upana wa sm 5 - 8. 

19. Bolivian Rainbow
Aina hii hutokea nchini Bolivia, Amerika ya kusini, ina umbile linalovutia sana kama upinde wa mvua, zina rangi ya zambarau, zikiiva huwa na rangi ya njano au rangi ya machungwa kwenda nyekundu na zina ukali wa wastani. 

20. Brain Strain
Aina hii ni hatari sana kwani ni kali kupita maelezo, yaani ni kali sana, aina hii hutokea Carolina ya kaskazini nchini Marekani. 

21. Caribbean Red
Aina hii pia ni kali sana hutokea nchini Mexico, pia hupandwa sana visiwa vya Caribbean na maeneo kuzunguka Amerika ya kaskazini, matunda ya aina hii ya pilipili hufikia urefu wa sm 2.5 na upana wa sm 3.8 

22. Carolina Cayenne
Aina hii hufanana na aina nyingine ya Cayenne ambayo hutokea nchi mbalimbali duniani, tofauti yake tu ni kwamba hii hutokea California, nchini Marekani. Zinapoiva huwa nyekundu sana, na huwa na ngozi laini yenye kubonyea bonyea. 

23. Carolina Reaper
Aina hii ni kali sana kuliko aina zote za pilipili duniani , Kiwango chake cha ukali ni Scoville Heat Units (SHU) 1,400,000 – 2,200,000. 

24. Cascabel
Aina hii hutokea maeneo mengi nchini Mexico, ni ndogo na zina umbile la mviringo hufikia kipenyo cha sm 2 - 3 na zikikomaa huwa nyekundu. Ni kali kidogo, kiwango chake cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 3,000. 

25. Cayenne Buist's Yellow
Aina hii ina rangi ya njano, ni kali kidogo, kiwango chake cha ukali ni Scoville Heat Units (SHU) 1,000. 

26. Cayenne Golden
Aina hii ina rangi ya dhahabu yenye kuvutia sana na inakomaa kutoka rangi ya kijani kwenda rangi ya dhahabu iliyochangamana na njano. Zina umbile kubwa kuliko aina ya 'Red Cayenne' hufikia urefu wa sm 10 - 15 (Inchi 4 - 6). Ina ukali wa wastani, kiwango chake cha ukali ni Scoville Heat Units (SHU) 30,000 - 50,000. 

27. Cayenne
Aina hii ni ndogo, huwa na rangi ya kijani, ikikomaa na kuiva huwa na rangi nyekundu, hufikia urefu wa sm 5 - 7.5 (Inchi 2 - 3), ina ukali wa wastani, kiwango chake cha ukali ni Scoville Heat Units (SHU) 30,000 - 50,000. 



28. Charleston
Aina hii hufanana na 'Carolina Cayenne' ni kali zaidi kuliko aina nyingine ya 'Cayenne', kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 70,000 - 100,000. 

29. Chilaca
Aina hii ni ndefu, zina umbile lililopinda mfano wa nusu mwezi (Curved), hufikia urefu wa sm 15 - 23 (Inchi 6 - 9) na upana wa sm 2.5 (Inchi 1). Zina umbile bapa na ngozi yake imebonyea bonyea, ikikomaa na kuiva huwa na rangi ya kahawia. Ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 2,500. 

30. Chiles de Arbol
Aina hii ni ndogo hutokea nchini mexico, jina la 'chiles de arbol' humaanisha 'Pilipili ya kwenye mti' kwa kispaniola. Hufikia urefu wa sm 5 - 7.5 (Inchi 2 - 5) na upana wa sm 1.2 (Inchi 1/2). Zina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 50,000 - 65,000.



Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post