KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA TATU
31. Chilhuacle Amarillo
Aina hii hutokea nchini Mexico,
zimegawanyika katika makundi mawili ikiwemo Chilhuacle Negro (Huwa na rangi ya
kahawia) na Chilhuacle Rojo (Huwa na rangi nyekundu). Zikianza kukua hadi
kukomaa huwa na rangi ya kijani na zikiiva huwa na rangi ya njano au rangi ya
chungwa, zina ukali wa kati.
32. Chili Pequin
Aina hii ya pilipili vilevile
huitwa 'Bird pepper' kwa sababu huliwa na kusambazwa na ndege. Zina umbile dogo
sana, neno 'Piquin' limetokana na neno kihispaniola "Pequeno"
likimaanisha 'ndogo sana'. Aina hii ya pilipili hufikia urefu wa sm 1.2 - 2
(Inchi ½ - ¾), ina ukali wa wastani, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 30,000 - 60,000.
33. Chiltepin
Aina hii ni ndogo sana, ina umbile la mvoringo, hupandwa
sana nchini Mexico na Marekani. Ina ukali wa wastani, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 50,000 - 100,000.
34. Chimayo
Aina hii hii pia huzalishwa nchini Mexico, hufikia urefu wa
sm 10 - 18. Ni kali kidogo kiwango cha ukali ni
Scoville Heats Units (SHU) 4,000 - 6,000.
35. Fresno
Aina hii ni huwa na rangi ya kijani, ikiiva huwa na rangi
nyekundu. Ina ukali kidogo, kiwango cha ukali ni
Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 10,000.
36. Ghost
Aina hii ni miongoni mwa pilipili
kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 855,000 -
1,041,427.
37. Gibralta / Spanish Naga
Aina hii hupandwa sana nchini hispania, ni miongoni mwa
pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni
Scoville Heats Units (SHU) 1,086,844.
38. Guajillo
Aina hii pia hutokea nchini
Mexico, ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 -
5,000.
39. Guindilla
Aina hii hutokea nchini Hispania,
ni nyembamba na ndefu, ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats
Units (SHU) 1,000 - 2,000.
40. Guntur
Aina hii hutokea maeneo ya 'Guntur' na 'Warangal' katika
jimbo la Andhra Pradesh nchini India. Aina hii ya pilipili imekua maarufu sana
maeneo hayo na imekua zao muhimu la biashara linalosaidia familia nyingi.
Umaarufu wake umeenea ulimwenguni kote, aina hii imesambaa maeneo mengi
ulimwenguni. Ina ukali wa wastani, kiwango cha ukali
ni Scoville Heats Units (SHU) 35,000 - 40,000.
41. Habanero
Aina hii hutokea katika jiji la La Habana nchini Cuba,
hufanana na Scotch bonnet pepper. Ina ukali wa kati, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 100,000 - 350,000.
42. Hatch
Aina hii hutokea katika bonde la Hatch nchini Mexico, ni
kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats
Units (SHU) 1,000 - 8,000.
43. Hawaiian
Aina hii hufikia urefu wa sm 5
(Inchi 2), hutumika zikikomaa na kuwa nyekundu. Ni kali kidogo, kiwango cha
ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 5,000.
44. Hidalgo
Aina hii pia hutokea nchini Mexico na Amerika ya kati,
hutengeneza matunda mengi kwa mche mmoja, hufikia urefu wa sm 5 (Inchi 2). Ina
ukali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats
Units (SHU) 6,000 - 17,000.
45. Hj8 Total Eclipse
Aina hii imekua ikipelekwa anga za juu kwa kutumia satelaiti
tangu miaka ya 1980 nchini china. Kila tripu ya kwenda anga za juu zaidi ya
mbegu 5,000 zimekuwa zikipelekwa mazingira ambayo hayana nguvu ya uvutano (zero
gravity) na mionzi ya angani (cosmic radiation). Baada ya hapo huzirudisha
46. Hungarian wax
Aina hii hutokea nchini Hungary, hufanana na pilipili aina
ya banana, lakini ni kali zaidi, ni kali kiasi, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 15,000.
47. Infinity
Aina hii hutokea nchini Uingereza, ni miongoni mwa pilipili
kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville
Heats Units (SHU) 1,176,182.
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Post a Comment