Kilimo Bora cha Pilipili kichaa - Sehemu ya Nne (Growing Chili pepper - Part Four)


KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA NNE

48. Jalapeno
Aina hii hutokea nchini Mexico, hufikia wastani wa urefu wa sm 5 - 9 (Inchi 2 - 3.5), pia huweza kukua na kufikia urefu wa sm 15 (Inchi 6). Ni kali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 8,000.

49. Jaloro
Aina hii hutokea nchini Marekani, zina rangi ya njano lakini zikiiva huwa na rangi nyekundu. Zina ukali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 5,000.

50. Jamaican
Aina hii hutokea nchini jamaica, imekua maarufu ulimwemguni kote, zina rangi ya kahawia na ngozi iliyojikunja, hufikia urefu wa sm 5 (Inchi 2). Zina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 100,000 - 200,000.

51. Jwala Finger
Aina hii hotokea nchini India, hutumika sana nchini India, neno 'Jwala', ni neno la kihindi linalomaanisha "Volkano". Aina hii hupatika maeneo ya Gujarat nchini India. Matunda ya pilipili huwa na rangi ya kijani, yakiiva huwa rangi nyekundu. Zina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 20,000 - 30,000.

52. Komodo Dragon
Aina hii utokea nchi za ulaya, ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,400,000 - 2,200,000.

53. Lemon Drop
Aina hii ina rangi ya njano iliyong'aa, ina ladha ya limao, hutokea nchini Peru. Hufikia urefu wa sm 5 - 7.5 (Inchi 2 - 3) na upana wa sm 1.2 (½ Inchi) na ngozi iliyobonyea bonyea. Ladha hii ya matunda huwavutia sana wale wanaopenda ladha ya malimao. Ina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 15,000 - 30,000.

54. Malagueta
Aina hii hufanana na pilipili aina ya 'Bird's Eye' kwa sababu ya rangi nyekundu inayong'aa, udogo na kuchongoka. Huanza zikiwa za kijani na hukomaa zikiwa nyekundu, pia hufikia urefu wa sm 5 (Inchi 2). Zina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 60,000 - 100,000.

55. Mirasol
Aina hii hutokea nchini Hispania, 'Mirasol' ni neno la kihispaniola likimaanisha "Kuangalia jua", ikielezea jinsi pilipili zinavyokua kwenye mmea, zinakua kuelekea juu. Zikishakauka huitwa "Guajillo". Ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 5,000.

56. Moshi
Aina hii hutokea mkoa wa Moshi, nchini Tanzania. Mkoa wa moshi upo mahali ulipo mlima Kilimanjaro, mlima mrefu barani Afrika (It is named for the region of Moshi, located at the base of Mount Kilimanjaro, Tanzania, East Africa). Aina hii huzaa sana, hufikia kimo cha mita 0.9 - 1.2, hutoa matunda ya kijani, yakiiva huwa na rangi nyekundu. Matunda hufikia urefu wa sm 5 (inchi 2), na ni kali sana.

57. Mulato
Aina hii hufanana na aina ya 'Ancho', lakini hutofautiana ladha, zote huwa zinakua kijani wakati zinakua lakini zikiiva, Mulato huwa kahawia wakati Ancho huwa nyekundu sana. Matunda yake hufikia urefu wa sm 10 (inchi 4). Ni kali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 3,000.

58. Naga Morich
Aina hii hutokea nchini India na Bangladesh, ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000,000 - 1,500,000.

"Naga Morich Pepper" flickr photo by blizzard shared under a Creative Commons (BY-NC-ND) license

59. Naga Viper
Aina hii ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,382,118.

60. New Mex Big Jim
Aina hii hutokea nchini Mexico, ni ndefu sana matunda yake hufikia urefu wa sm 25 - 30 (inchi 10 - 12). Zikiiva huwa na rangi nyekundu, lakini mara nyingi huvunwa wakati zina ukijani wake. Ni kali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 3,000.

61. New Mex XX Hot
Aina hii pia hutokea nchini Mexico, matunda yake yana ngozi laini, hufikia urefu wa sm 7.5 - 13 (inchi 3 - 5). Ina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 60,000 - 70,000.

62. New Mexico Scorpion
Aina hii pia hutokea nchini Mexico, ni kali sana, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,191,595.

63. Peter
Aina hii hutokea jimbo la Texas nchini Marekani, matunda yake hufikia urefu wa sm 7.5 - 10 (inchi 3 - 4) na upana wa sm 2.5 - 4 (inchi 1 - 1.5). Ina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 5,000 - 30,000.

64. Red Savina
Aina hii huzaa matunda yenye rangi nyekundu inayong'aa, huzaa mpaka matunda 50 kwa shina moja. Ni kali sana, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 200,000 - 580,000.

65. Rocoto
Aina hii pia hutokea nchini Mexico, Amerika ya kati na Columbia. Ina majina mengi, ina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 30,000 - 100,000.



Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

Previous Post Next Post