KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA TANO
66. Sandia
Aina hii hutokea nchini Mexico, hufanana na aina nyingine ya
'Anaheim', hufikia urefu wa sm 15 - 18 (inchi 6 - 7). Matunda huwa na rangi ya
kijani yakiiva huwa na rangi nyekundu, ina ukali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 5,000 - 7,000.
67. Santaka
Aina hii hutokea nchini Japan,
hufikia urefu wa sm 5 (inchi 2), ina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni
Scoville Heats Units (SHU) 40,000 - 50,000.
68. Scotch Bonnet
Aina hii hutokana na aina nyingine ya pilipili inayoitwa
'Habanero', ni miongoni mwa pilipili kali duniani, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 100,000 - 350,000.
69. Serrano
Aina hii hufanana na aina nyingine ya pilipili inayoitwa
'Jalapeño', hufanana rangi lakini ni ndogo hufikia urefu wa sm 2.5 -
10 (inchi 1 - 4) na wastani wa upana wa sm 1.3 (inchi ½). Ni kali
kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units
(SHU) 10,000 - 23,000.
70. Shipkas
Aina hii hutokea nchini Bulgaria, hujulikana kwa jina la
'Bulgarian Carrot Pepper' au 'Pilipili Karoti' kwa sababu muonekano wake
hufanana na karoti huwa na rangi ya chungwa, ndefu na nyembamba. Ina ladha ya
matunda, hufikia urefu wa sm 9 (inchi 3½). Ni kali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 5,000 -
30,000.
71. Super
Aina hii ina mvuto ikipandwa, hupendeza kama maua ya
kawaida, matunda ya pilipili hukua kwenda juu, hutengeneza makundi makundi na
yakiiva hubadirika kutoka rangi ya kijani kwenda rangi nyekundu. Matunda yake
ni madogo, hufikia urefu wa sm 4 - 5 (inchi 1½ - 2) na upana wa sm 1.3 - 2.5 (inchi ½
- 1). Zina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni
Scoville Heats Units (SHU) 40,000 - 50,000.
72. Tabasco
Aina hii ni kali, huelekeana na aina nyingine ya pilipili
inayoitwa 'Jalapeno', hufikia urefu wa sm 5 (inchi 2), huwa na rangi ya chungwa
kabla ya kuiva, zikiiva huwa na rangi nyekundu inayong'aa. Ni kali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 30,000 -
50,000.
73. Tabiche
Aina hii hutokea nchini India, lakini kwa sasa hupatikana
ulimwenguni kote, hufikia urefu wa sm 7.5 (inchi 3) na upana wastani wa sm 2.5
(inchi 1), ngozi ya matunda imebonyea bonyea. Matunda huwa na rangi kijani
yakikomaa na kuiva huwa na rangi ya njano mpauko. Ni kali, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 85,000 -
115,000.
74. Thai Hot
Aina hii hutokea nchini Thailand, kuna aina zaidi ya 79 za
pilipili ya 'Thai' zikiwa na viwango tofauti tofauti vya ukali. Ni kali, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 50,000 -
100,000.
75. Tiburon
Aina hii hutokana na aina nyingine ya pilipili inayoitwa
'Poblano', matunda yake ni makubwa hufikia urefu wa sm 13 - 18 (inchi 5 - 7) na
upana wa sm 6 - 9 (inchi 2.5 - 3.5). Ni kali kidogo, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 2,000.
76. Tien Tsin
Aina hii hutokea jimbo la 'Tien
Tsin' nchini China, huzalishwa sana nchini china, lakini kwa sasa hupatikana
maeneo mengi duniani. Ni kali, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU)
50,000 -
77. Tiger Paw Nr
Aina hii hutokea Carolina ya
kusini nchini Marekani, ni aina ya pilipili aina ya 'Habanero', aina hii
huvumilia sana mashambulizi ya minyoo fundo (Root nematodes). Ni kali sana, kiwango
cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 265,000 - 328,000.
78. Trinidad Moruga Scorpion
Aina hii hutokea nchini Mexico, ni miongoni mwa pilipili
kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville
Heats Units (SHU) 2,009,231.
79. Trinidad Scorpion Butch
Aina hii hutokea nchini Mexico, ina ngozi rafu na mkia kama
n'nge (Scorpion), ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 800,000 -
1,463,700.
80. Trinidad Scorpion
Aina hii hutokea Caribbean, zina
rangi nyekundu, ngozi yake imekunjamana yani kama imebonyea bonyea. Hufanana na
n'nge (Scorpion) kwa muonekano wa matunda pia na kwa ukali wake. Zinakomaa
baada ya siku 80 na kuendelea. Ni kali sana, kiwango cha ukali ni Scoville
Heats Units (SHU) 300,000 na kuendelea.
"Trinidad Scorpion Butch T pepper" flickr photo by Richard Elzey shared under a Creative Commons (BY) license
81. Tshololo
Aina hii hutokea nchini Brazil,
ina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 80,000 -
120,000.
82. Yatsafusa
Aina hii hutokea nchini japani,
mara nyingine huitwa 'Japanese chile'. Mmea wa pilipili hii huwa ni mfupi,
hutengeneza maua ya njano. Matunda yaliyokomaa hukaushwa kabla ya kutumia. Ina
ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 75,000.
NB:
Kama nilivyoeleza mwanzoni kabisa
mwa makala hii, mbali na aina ya pilipili husika, hali ya joto huongeza ukali
wa pilipili, kadiri joto linavyoongezeka ndivyo ukali wa pilipili unavyozidi
kuongezeka. Kiwango cha ukali wa pilipili hupimwa na kipimo kinachoitwa "Scoville
Heats Units (SHU)", kufahamu zaidi kuhusu kipimo hiki BOFYA HAPA.
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Post a Comment