Kilimo Bora cha Pilipili kichaa - Sehemu ya Tatu (Growing Chili pepper - Part Three)


KILIMO CHA PILIPILI KICHAA SEHEMU YA TATU

31. Chilhuacle Amarillo
Aina hii hutokea nchini Mexico, zimegawanyika katika makundi mawili ikiwemo Chilhuacle Negro (Huwa na rangi ya kahawia) na Chilhuacle Rojo (Huwa na rangi nyekundu). Zikianza kukua hadi kukomaa huwa na rangi ya kijani na zikiiva huwa na rangi ya njano au rangi ya chungwa, zina ukali wa kati.

32. Chili Pequin
Aina hii ya pilipili vilevile huitwa 'Bird pepper' kwa sababu huliwa na kusambazwa na ndege. Zina umbile dogo sana, neno 'Piquin' limetokana na neno kihispaniola "Pequeno" likimaanisha 'ndogo sana'. Aina hii ya pilipili hufikia urefu wa sm 1.2 - 2 (Inchi ½ - ¾), ina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 30,000 - 60,000.

33. Chiltepin
Aina hii ni ndogo sana, ina umbile la mvoringo, hupandwa sana nchini Mexico na Marekani. Ina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 50,000 - 100,000.

34. Chimayo
Aina hii hii pia huzalishwa nchini Mexico, hufikia urefu wa sm 10 - 18. Ni kali kidogo kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 4,000 - 6,000.

35. Fresno
Aina hii ni huwa na rangi ya kijani, ikiiva huwa na rangi nyekundu. Ina ukali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 10,000.

36. Ghost
Aina hii ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 855,000 - 1,041,427.

37. Gibralta / Spanish Naga
Aina hii hupandwa sana nchini hispania, ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,086,844.

38. Guajillo
Aina hii pia hutokea nchini Mexico, ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 2,500 - 5,000.

39. Guindilla
Aina hii hutokea nchini Hispania, ni nyembamba na ndefu, ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 2,000.

40. Guntur
Aina hii hutokea maeneo ya 'Guntur' na 'Warangal' katika jimbo la Andhra Pradesh nchini India. Aina hii ya pilipili imekua maarufu sana maeneo hayo na imekua zao muhimu la biashara linalosaidia familia nyingi. Umaarufu wake umeenea ulimwenguni kote, aina hii imesambaa maeneo mengi ulimwenguni. Ina ukali wa wastani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 35,000 - 40,000.

41. Habanero
Aina hii hutokea katika jiji la La Habana nchini Cuba, hufanana na Scotch bonnet pepper. Ina ukali wa kati, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 100,000 - 350,000.


42. Hatch
Aina hii hutokea katika bonde la Hatch nchini Mexico, ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 8,000.

43. Hawaiian
Aina hii hufikia urefu wa sm 5 (Inchi 2), hutumika zikikomaa na kuwa nyekundu. Ni kali kidogo, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 5,000.

44. Hidalgo
Aina hii pia hutokea nchini Mexico na Amerika ya kati, hutengeneza matunda mengi kwa mche mmoja, hufikia urefu wa sm 5 (Inchi 2). Ina ukali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 6,000 - 17,000.

45. Hj8 Total Eclipse
Aina hii imekua ikipelekwa anga za juu kwa kutumia satelaiti tangu miaka ya 1980 nchini china. Kila tripu ya kwenda anga za juu zaidi ya mbegu 5,000 zimekuwa zikipelekwa mazingira ambayo hayana nguvu ya uvutano (zero gravity) na mionzi ya angani (cosmic radiation). Baada ya hapo huzirudisha 

46Hungarian wax
Aina hii hutokea nchini Hungary, hufanana na pilipili aina ya banana, lakini ni kali zaidi, ni kali kiasi, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,000 - 15,000.

47. Infinity
Aina hii hutokea nchini Uingereza, ni miongoni mwa pilipili kali zaidi duniani, kiwango cha ukali ni Scoville Heats Units (SHU) 1,176,182.



Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم