Hawa ni panzi wanaovamia majani, panzi wakubwa wana rangi ya
kijani iliyochangamana na rangi nyeusi pamoja na rangi ya njano. Pia wana alama
zenye rangi nyeusi na njano mwili mzima.
Panzi wadogo ni weusi na alama za njano mwili mzima. Panzi
jike hutaga mayai chini ya udongo kwenye kivuli hususani chini ya mimea /miti
isiyopukutisha majani mwaka mzima na kubakia kijani (evergreen), mara nyingi
hutaga mayai nje ya shamba la mihogo. Hutaga mayai mengi na kuzungushia na
utando kama sponji. Mayai huanza kuanguliwa kipindi cha mwanzo wa msimu wa
kiangazi.
Athari
Panzi huathiri mazao mengi hususani katika umri wa miche.
Kwa upande wa mihogo hutafuna majani na mashina na husababisha majani
kupukutika na majeraha kwenye mashina. Hii hutokea sana kwenye shamba la muhogo
lilikokaribu na vichaka na kukiwa na ukame wa muda mrefu au msimu wa kiangazi
uliopitiliza.
Namna ya kuwadhibiti
- Kuwakamata kwa mkono, hii inafaa sana kwa shamba dogo.
- Pulizia mimea yako na juisi ya mwarobaini (Neem extracts), hii itasaidia kuwafukuza panzi hao na kuacha kula. Panzi hawapendi harufu ya mwarobaini. Kutengeneza juisi ya mwarobaini tumia mazao yoyote ya mwarobaini kama majani, mbegu, matawi, mashina au mizizi.
8. Whiteflies (Bemisia tabaci,
Aleurodicus dispersus)
Hawa ni wadudu wadogo sana wana
rangi nyeupe na wana mabawa, huathiri mazao mengi hususani mazao ya bustani
kama nyanya, n.k. Wadudu hawa pia huvamia zao la muhogo.
Wadudu hawa hukaa na huzaliana
chini ya majani na hutengeneza utando laini mweupe. Wadudu hawa majike hutaga
mayai chini ya majani.
B. tabaci adults feeding on the underside of a young cassava leaf photo by IITA shared under Creative license BY-NC 2.0
Picha: 'Whiteflies' wakiwa chini ya majani ya mihogo
Athari
- Wadudu hawa hufyonza maji maji ya chakula kwenye majani na kusababisha kupungua kwa mavuno hapo baadae endapo wadudu hawa wasipodhibitiwa. Pia wadudu hawa husambaza ugonjwa ya virusi wa muhogo unavyoitwa 'African Cassava mosaic virus', ugonjwa unaopunguza mavuno ya muhogo kwa maeneo mengi barani Afrika.
- Wadudu hawa hutoa uchafu au uteute (honeydew) ambao husababisha majani kuwa na fangasi nyeusi, hali hii husababisha majani yaliyokomaa kupukutika mapema.
Namna ya kuwadhibiti
- Waangamize wadudu hawa kwa kutumia dawa mbali mbali za asili kama juisi ya Mwarobaini (Neem extracts), kwa kupulizia chini ya majani.
- Watunze wadudu rafiki wanaokula wadudu hawa (predators), kwa kuepuka kupulizia dawa za kemikali zinazoangamiza wadudu wa aina zote (Broad spectrum Pesticides). Wadudu hao rafiki ni kama Parasitic wasps, Encarsia formosa na Encarsia haitiensis. Tazama picha hapo chini kuwafahamu.
9. Mchwa (Termites)
Mchwa huathiri mazao mengi ikiwemo
zao la muhogo, huaribu mashina na mizizi ya mihogo. Mchwa hawa huathiri muhogo
uliochelewa kupandwa au uliopandwa mwanzoni mwa msimu wa kiangazi, hususani
wakati ambapo mmea ukiwa bado mchanga katika kipindi hicho cha kiangazi.
Athari
- Wanakula na kutafuna vipande vya mashina ya muhogo vilivyopandwa hususani vipande vilivyoota vibaya, vilivyokufa na vilivyooza. Pia wanaweza wakaharibu shamba zima.
- Kwa mimea ya muhogo iliyozeeka mchwa hutafuna na huingia ndani ya mashina, hali hii husababisha mashina kudhoofika na kuvunjika kirahisi.
Namna ya kuwadhibiti
- Panda mapema mara tu mvua zinapoanza kunyesha.
- Epuka kupanda mihogo yako kwenye ardhi kavu sana na kwenye vichuguu.
10. Wadudu wa ghalani (Storage
pests).
Hawa ni wadudu wanaoharibu muhogo uliohifadhiwa ghalani
(Makopa), Wadudu hawa ni jamii ya 'Beetles' hula na huharibu mihogo mikavu
iliyohifadhiwa (Makopa). Baadhi ya wadudu hawa ni kama wafuatao; Dinoderus sp., Carpophilus sp., Coffee bean weevil (Araecerus fasciculatus), Lesser grain borer
(Rhizopertha dominica), na Larger grain borer (Prostephanus truncatus). Tazama
picha zao hapa chini kuwafahamu.
Picha (Juu): Carpophilus sp Ukubwa: mm 2 - 4
Picha (Juu): Dinoderus sp. Ukubwa: mm 4 Photo Credit: www.bookofinsect.com
Picha (Juu): Coffee bean weevil (Araecerus fasciculatus) Ukubwa: mm 3 - 5 Photo Credit: www.alchetron.com
Picha (Juu): Lesser grain borer (Rhizopertha dominica) Ukubwa: mm 2 - 3 Photo Credit: www.inpn.mnhn.fr
Picha (Juu): Larger grain borer (Prostephanus truncatus) Ukubwa: mm 6 Photo Credit: www.pvgard.com
Athari
- Wadudu hawa hubungua mihogo mikavu iliyohifadhiwa (Makopa).
- Uharibifu wa wadudu hawa huongezeka kipindi cha masika kuliko kiangazi kwa sababu kipindi cha masika kunakua na unyevu hewa sana (Humidity) kuliko kiangazi.
- Uharibifu wa wadudu hawa huanza miezi 6 hadi 8 tangu kuhifadhi makopa yako ghalani, kipindi hiki hubadilika kuwa vumbi yakiminywa.
Namna ya Kuwadhibiti
Tumia dawa za asili ili kuilinda mihogo yako mikavu
uliyohifadhi. Imeripotiwa kwamba kuhifadhi mihogo yako pamoja na kiasi kikubwa
wastani cha majani makavu ya mmea aina ya Lantana,
Eucalyptus au Mwarobaini husaidia kuwafukuza wadudu hawa.
A: MWAROBAINI (NEEM LEAVES)
B: MAJANI YA MKARATUSI (EUCALYPTUS)
C: MAJANI YA LANTANA
<<< SEHEMU YA TATU
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
Post a Comment