Kilimo bora cha Mihogo - Sehemu ya Nne (Growing Cassava - Part Four)


SEHEMU YA NNE

Imehaririwa: 05 January, 2020

7. Grasshoppers (Zonocerus variegatus
Hawa ni panzi wanaovamia majani, panzi wakubwa wana rangi ya kijani iliyochangamana na rangi nyeusi pamoja na rangi ya njano. Pia wana alama zenye rangi nyeusi na njano mwili mzima.

Panzi wadogo ni weusi na alama za njano mwili mzima. Panzi jike hutaga mayai chini ya udongo kwenye kivuli hususani chini ya mimea /miti isiyopukutisha majani mwaka mzima na kubakia kijani (evergreen), mara nyingi hutaga mayai nje ya shamba la mihogo. Hutaga mayai mengi na kuzungushia na utando kama sponji. Mayai huanza kuanguliwa kipindi cha mwanzo wa msimu wa kiangazi.

Photo Credit: Rigobert T 

Athari
Panzi huathiri mazao mengi hususani katika umri wa miche. Kwa upande wa mihogo hutafuna majani na mashina na husababisha majani kupukutika na majeraha kwenye mashina. Hii hutokea sana kwenye shamba la muhogo lilikokaribu na vichaka na kukiwa na ukame wa muda mrefu au msimu wa kiangazi uliopitiliza.

Namna ya kuwadhibiti
  • Kuwakamata kwa mkono, hii inafaa sana kwa shamba dogo.
  • Pulizia mimea yako na juisi ya mwarobaini (Neem extracts), hii itasaidia kuwafukuza panzi hao na kuacha kula. Panzi hawapendi harufu ya mwarobaini. Kutengeneza juisi ya mwarobaini tumia mazao yoyote ya mwarobaini kama majani, mbegu, matawi, mashina au mizizi.

8. Whiteflies (Bemisia tabaci, Aleurodicus dispersus)
Hawa ni wadudu wadogo sana wana rangi nyeupe na wana mabawa, huathiri mazao mengi hususani mazao ya bustani kama nyanya, n.k. Wadudu hawa pia huvamia zao la muhogo.

Wadudu hawa hukaa na huzaliana chini ya majani na hutengeneza utando laini mweupe. Wadudu hawa majike hutaga mayai chini ya majani.

Picha: 'Whiteflies' wakiwa chini ya majani ya mihogo

Photo: www.pinpointpestcontrol.com       Picha: Whitefly

Athari
  • Wadudu hawa hufyonza maji maji ya chakula kwenye majani na kusababisha kupungua kwa mavuno hapo baadae endapo wadudu hawa wasipodhibitiwa. Pia wadudu hawa husambaza ugonjwa ya virusi wa muhogo unavyoitwa 'African Cassava mosaic virus', ugonjwa unaopunguza mavuno ya muhogo kwa maeneo mengi barani Afrika.
  • Wadudu hawa hutoa uchafu au uteute (honeydew) ambao husababisha majani kuwa na fangasi nyeusi, hali hii husababisha majani yaliyokomaa kupukutika mapema.
Namna ya kuwadhibiti
  • Waangamize wadudu hawa kwa kutumia dawa mbali mbali za asili kama juisi ya Mwarobaini (Neem extracts), kwa kupulizia chini ya majani.
  • Watunze wadudu rafiki wanaokula wadudu hawa (predators), kwa kuepuka kupulizia dawa za kemikali zinazoangamiza wadudu wa aina zote (Broad spectrum Pesticides). Wadudu hao rafiki ni kama Parasitic wasps, Encarsia formosa na Encarsia haitiensis. Tazama picha hapo chini kuwafahamu.

WADUDU RAFIKI

A: PARASITIC WASPS


Picha: Parasitic wasps wakila vidukali mafuta (Aphids) pia huwa wanakula 'Whiteflies' na wengineo  Photo Credit: www.blogs.discovermagazine.com


B: ENCARSIA FORMOSA

 Picha: Encarsia formosa

Picha: Encarsia formosa akitaka kumvamia  na kumla whitefliy


C: ENCARSIA HAITIENSIS

Photo Credit: www.nbair.res.in

9. Mchwa (Termites)
Mchwa huathiri mazao mengi ikiwemo zao la muhogo, huaribu mashina na mizizi ya mihogo. Mchwa hawa huathiri muhogo uliochelewa kupandwa au uliopandwa mwanzoni mwa msimu wa kiangazi, hususani wakati ambapo mmea ukiwa bado mchanga katika kipindi hicho cha kiangazi.



Athari
  • Wanakula na kutafuna vipande vya mashina ya muhogo vilivyopandwa hususani vipande vilivyoota vibaya, vilivyokufa na vilivyooza. Pia wanaweza wakaharibu shamba zima.
  • Kwa mimea ya muhogo iliyozeeka mchwa hutafuna na huingia ndani ya mashina, hali hii husababisha mashina kudhoofika na kuvunjika kirahisi.
Namna ya kuwadhibiti
  • Panda mapema mara tu mvua zinapoanza kunyesha.
  • Epuka kupanda mihogo yako kwenye ardhi kavu sana na kwenye vichuguu.

10. Wadudu wa ghalani (Storage pests).
Hawa ni wadudu wanaoharibu muhogo uliohifadhiwa ghalani (Makopa), Wadudu hawa ni jamii ya 'Beetles' hula na huharibu mihogo mikavu iliyohifadhiwa (Makopa). Baadhi ya wadudu hawa ni kama wafuatao; Dinoderus sp., Carpophilus sp., Coffee bean weevil (Araecerus fasciculatus), Lesser grain borer (Rhizopertha dominica), na Larger grain borer (Prostephanus truncatus). Tazama picha zao hapa chini kuwafahamu.

Picha (Juu): Carpophilus sp     Ukubwa: mm 2 - 4

Picha (Juu): Dinoderus sp.     Ukubwa: mm 4   Photo Credit: www.bookofinsect.com


Picha (Juu): Coffee bean weevil (Araecerus fasciculatus)  Ukubwa: mm 3 - 5  Photo Credit: www.alchetron.com


Picha (Juu): Lesser grain borer (Rhizopertha dominica)   Ukubwa: mm 2 - 3  Photo Credit: www.inpn.mnhn.fr

Picha (Juu): Larger grain borer (Prostephanus truncatus)   Ukubwa: mm 6   Photo Credit: www.pvgard.com


Athari
  • Wadudu hawa hubungua mihogo mikavu iliyohifadhiwa (Makopa).
  • Uharibifu wa wadudu hawa huongezeka kipindi cha masika kuliko kiangazi kwa sababu kipindi cha masika kunakua na unyevu hewa sana (Humidity) kuliko kiangazi.
  • Uharibifu wa wadudu hawa huanza miezi 6 hadi 8 tangu kuhifadhi makopa yako ghalani, kipindi hiki hubadilika kuwa vumbi yakiminywa.
Namna ya Kuwadhibiti
Tumia dawa za asili ili kuilinda mihogo yako mikavu uliyohifadhi. Imeripotiwa kwamba kuhifadhi mihogo yako pamoja na kiasi kikubwa wastani cha majani makavu ya mmea aina ya Lantana, Eucalyptus au Mwarobaini husaidia kuwafukuza wadudu hawa.

A: MWAROBAINI (NEEM LEAVES)


B: MAJANI YA MKARATUSI (EUCALYPTUS)



C: MAJANI YA LANTANA


<<< SEHEMU YA TATU


Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم