Ufahamu Ugonjwa wa Endometriosis kwa Wanawake. (Understand Endometriosis disease in Women)



Endometriosis (Jina la kimombo) ni ugonjwa wa wanawake ambao tishu zinazotengeneza ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi hukua sehemu ya nje ya mfuko wa uzazi. Sehemu ya ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi huitwa "endometrium" kwa lugha ya kimombo.

Endometriosis hutokea wakati ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi unapokua juu ya mfuko wa mayai ya uzazi (ovary), utumbo, na tishu zilizopo kwenye mifupa ya kiuno (pelvis). Si kawaida kwa tishu za endometrial  kuenea zaidi ya eneo la mifupa ya kiuno (pelvic), na huwa haiwezekani kutokea. tishu zinazokua ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi (Endometrial) na zinazoota au kukua nje ya mfuko wa uzazi (mji wa mimba) huitwa "endometrial implant" kwa lugha ya kimombo.
Tazama mchoro ufuatao kwa ufahamu zaidi;


Mabadiliko ya homoni ya mzunguko wako wa hedhi kusababisha kubadilishwa kwa tishu za ukuta wa mfuko wa uzazi. Hii ina maana kwamba tishu hiyo hukua, hukomaa, na kuvunjika. Baada ya muda, tishu iliyovunjika huelekezwa maeneo ya mifupa ya kiuno (pelvis) na kubakia mahali hapo.

Tishu zilizonyakuliwa na eneo la mifupa ya kiuno (pelvis) husababisha yafuatayo;
  • Maumivu ya kuchoma sehemu ya kiuno
  • Husababisha makovu maeneo ya uzazi
  • Tishu hizo hushikanisha viungo vilivyopo maeneo ya mifupa ya kiuno (pelvis)
  • Maumivu makali wakati wa hedhi
  • Matatizo ya Uzazi, Mwanamke kukosa uwezo wa kushika mimba


DALILI ZA UGONJWA

1. Maumivu
  • Maumivu makali kabla au baada ya hedhi
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
  • Maumivu ya tumbo, mgongo na maeneo ya mifupa ya kiuno (pelvis)
  • Maumivu unapotaka kwenda kujisaidia/kwenda haja
  • Maumivu ya miguu
2. Hedhi
  • Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, damu hiyo inaweza kuwa au kutokuwa na mabonge
  • Kuwa na hedhi ya muda mrefu isivyo kawaida
  • Kupata hedhi kabla ya muda wa kawaida
3. Uke
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
4. Matatizo ya Kibofu na Utumbo
  • Kutokwa na damu maeneo ya Kibofu au Utumbo
  • Kubadilika kwa hali ya utumbo i.e Kuwa na haja kubwa ngumu (constipation) na Kuharisha
  • Kukojoa mara nyingi isivyo kawaida
5. Kuvimba kwa tumbo wakati wa hedhi, kwaweza kuwa na maumivu au bila maumivu
6. Kuishiwa nguvu au uchovu wakati wa hedhi

CHANZO CHA UGONJWA
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kuchangia mwanamke kupata ugonjwa huu

1. Historia ya Familia
Mwanamke ambaye baadhi ya ndugu zake wa karibu walishapata ugonjwa huu basi na yeye yuko hatarini kuupata.

2. Historia ya kupata ujauzito
Kupata mimba imeonekana ni njia mojawapo ya kumlinda mwanamke kupata ugonjwa huu. Wanawake ambao hawajawahi kupata watoto wako hatarini kupata ugonjwa huu, ingawaje Ugonjwa huu pia huwakumba wanawake waliokwishapata watoto. 

3. Kudumaa ukuaji wakati wa utoto
4. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
5. Kupata hedhi ya kwanza kabla ya kufikia miaka 11
6. Mimba za Utotoni
7. Kuwa na uzito mdogo sana
8. Matumizi ya pombe

TIBA YA UGONJWA
Ugonjwa huu hauna Tiba, Matibabu ya dawa au Upasuaji yanaweza kufanywa ili kupunguza athari za dalili na kero ya ugonjwa.


NAMNA YA KUZUIA UGONJWA
Ugonjwa huu hauzuiliki kwa sababu chanzo hasa cha ugonjwa hakijulikani, Japokuwa Watafiti wanasema kwamba namna mojawapo ya kuuzuia ugonjwa huu ni pamoja na Mwanamke kupata mimba mapema, Siyo mimba za utotoni bali kutochelewa sana kupata ujauzito pia, Uzazi wa mpango pamoja na kufanya mazoezi

Tazama video ifuatayo kwa maelezo zaidi;



CHANZOjeanhailes.org.au, healthline.com & emedicinehealth.com






Imechapishwa na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم