Ifahamu Saratani (Kansa) ya Kizazi kwa wanawake (Cervical cancer) na Baadhi ya vyakula vinavyoweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huo



Kansa ya kizazi huathiri Cervix, Cervix ni sehemu nyembamba ya mji wa mimba ambayo watoto wanazaliwa. Kansa ya kizazi huongezeka polepole sana kiasi kwamba wanawake wengi wanakuwa hawajui kama wanayo saratani hii. Katika aina hii ya saratani seli za juu ya uso wa kizazi kuanza kubadilika hatua kwa hatua hadi kufikia hatua isiyoweza kutibika kabisa. Hata hivyo kama mabadiliko hayo yanakaribia kufikia hatua mbaya ni muhimu kuwepo matibabu ya haraka ili kuzibiti ugonjwa huu.

Seli za kizazi zinaweza kupitia aina nyingi za mabadiliko, ambayo huwa hayahusiani na saratani. Mabadiliko hayo yanaweza kusababishwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na maambukizi ya HPV. HPVs (Human papilloma viruses) ni kundi la zaidi ya virusi 100 vinavyohusiana, virusi hivyo vinaweza kuambukiza kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia ngono. Zaidi ya aina 15 za virusi hivyo kati ya aina 100 za HPV huweza kusababisha kansa ya kizazi.


Mara nyingi, maambukizi ya HPV(Virusi wanaosababisha kansa) hufanyika hasa wakati kiwango cha homoni ya kike 'estrogen' kikiwa kikubwa zaidi isivyo kawaida, seli zilizoambukizwa na HPV(Virusi wanaosababisha kansa ya kizazi) hubadirika kuwa seli aina ya precancerous, ambayo inakukuwa kansa. Badala ya kufa, seli zilizoathiriwa na HPV (Virusi wanaosababisha kansa ya kizazi) huendelea kuishi kawaida hatimaye huvamia tishu za karibu, na wakati mwingine kuenea katika sehemu nyingine za mwili kupitia damu (mchakato uitwao metastasis).

Ingawa maambukizi ya HPV ni kisababishi kikubwa zaidi cha kansa ya kizazi, siyo hivyo tu Utafiti unaonyesha kuwa sababu nyingine ni pamoja na mwenendo wa maisha ya kila siku kuhusiana na vyakula mbalimbali tunavyokula. 

Video ifuatayo inaonyesha hatua mbalimbali za ukuaji wa kansa ya kizazi, Tazama kwa makini;




Zifuatazo ni baadhi ya dalili za Saratani ya kizazi;

1.Hedhi isiyo ya kawaida

2.Kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya Ukeni

3.Kutokwa na majimaji(yasiyo na harufu yoyote) Ukeni

4.Kutokwa na majimaji yaliyochangamana na damu

5.Maumivu ya kiuno na Mgongo

6.Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

7.Matatizo wakati wa kujisaidia haja ndogo na haja kubwa (hali iliyo tofauti na kawaida)

**Mara uonapo dalili hizo fika Hosipitali kwa Uchunguzi zaidi


VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA KANSA YA KIZAZI KWA WANAWAKE
Utafiti umeonyesha kuwa vitamini na madini yana jukumu kubwa katika kupunguza athari ya saratani. Vyakula vya kupunguza athari ya kansa hufaa kuliwa sio tu kwa wale walioathirika na kansa bali na wale wasiokuwa na ugonjwa huu, kwa sababu ugonjwa huu ukiwa kwenye hatua ya awali Muhusika hawezi kujua kabisa hivyo, wanashauriwa kwamba watumie vyakula hivyo kulinda afya zao. Vitamin E ina uwezo mkubwa wa kupambana na aina ya hii ya saratani ya kizazi na saratani zingine. Kwa sababu hiyo inatakiwa katika mulo wako wa siku jitahidi kuwa na vyakula vyenye Vitamin E.

Vyakula kama mafuta ya alizeti, karanga, mikate, nafaka isiyokobolewa na mboga za majani. Mboga za majani (mboga mboga) ni vyanzo vizuri vya vitamini E hivyo unashauriwa kuzitumia kwa kila mulo. Baadhi ya vyakula vingine ni pamoja na;


1. PAPAI
Papapi ni moja ya chanzo kizuri sana cha vitamini C (hata kuwa bora zaidi kuliko machungwa), lakini pia ina madini aina ya beta-cryptoxanthin na zeaxanthin. Madini haya husaidia kushusha kiwango cha maambukizi ya HPV (Virusi wanosababisha kansa ya kizazi), na wataalam wanaamini kwamba kula papai moja tu kwa wiki inaweza kupunguza hatari ya mwanamke kuambukizwa kansa ya kizazi.




2. KAROTI
Nadhani unajua au umeshasikia kwamba karoti ni nzuri kwa macho yako, je unajua kwamba inaweza pia kusaidia kukulinda dhidi ya kansa ya kizazi? Karoti ina madini ya falcarinol - kemikali ya asili ambayo inaonekana kuwa yenye ufanisi. Wanasayansi waligundua kwamba panya waliokuwa na uvimbe wa awali wa kansa kabla na wakalishwa karoti, uvimbe huo ulipungua theluthi moja chini ya uwezekano wa kuendeleza uvimbe kamili wa kansa kuliko wanyama wengine ambao hawakupewa karoti. 

Unashauriwa kutumia karoti kila wakati, pia wataalamu wanashauri kwamba karaoti ikatwekatwe baada ya kuchemshwa ili kutunza virutubisho vya falcarinol. Karoti iliyokatwa na kuchemshwa hupoteza virutubisho hivyo kwa kiasi kikubwa.




3. BINZARI
Binzari ni kiungo chenye rangi ya njano, kwa muda mrefu kimekuwa kikitumika kama dawa za asili balani Asia ya kutibu magonjwa mbalimbali. Katika miaka ya hivi karibuni, pia watafiti wa dawa nchi za magharibi zimeanza kutoa kipaumbele kikubwa katika mimea hii yenye mzizi jamii ya tangawizi. Watafiti wamegundua aina nyingi ya saratani zinazoweza kutibiwa na Binzari.

Bizari imeonekana kuwa na virutubisho vinavyoweza kutambua chembechembe za saratani kutokana na uwezo wa kikemia zilizonazo hivyo kuweza kupunguza na kuzuia hatari ya kupata saratani.





4. MAHARAGE
Maharage ni chakula kinachotumiwa na watu wengi sana, pia ni mojawapo ya chakula kinachotumia kupunguza hatari ya kupata saratani za aina mbali mbali. faida ya maharage ni pamoja na urahisi wa kupatikana kwake kwa pia ina protini nyingi inayozuia uharibifu wa seli zetu mwilini. Maharage yana kemikali inayoitwa phytochemicals inayopunguza ukuaji wa saratani, chemikali hii huzilinda na kuepusha seli za mwili kubadirika na kuwa seli zenye saratani.


Hivyo ni baadhi tu ya vyakula vinavyopunguza hatari ya kupata saratani ya kizazi.

CHANZO: MTANDAO WA INTANETI

***Tupe maoni yako





Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم