Ufahamu Ugonjwa wa Pumu (Athima) [Understand Asthma disease in Humans]


Pumu (Athima) ni ugonjwa sugu (wa muda mrefu) wa mapafu ambao husababisha vivimbe kwenye mfumo wa hewa na kuzuia hewa inayoingia. Dalili zake ni pamoja Mapigo ya moyo kwenda kasi, kifua kubana na kuishiwa pumzi na kukohoa, kukohoa mara nyingi hutokea wakati wa usiku au asubuhi sana. hali hii hutofautiana baina ya mtu na mtu.

Pumu huathiri watu wa umri wote, lakini mara nyingi huanza wakati wa utoto. Nchini Marekani, zaidi ya watu milioni 25 wanaugua ugonjwa huu, Na kati ya hao milioni 7 ni watoto.

Mchoro ufuatayo unaonyesha eneo la mapafu na mfumo wa hewa mwilini. Kielelezo B kinaonyesha muonekano wa njia ya hewa ya kawaida bila ugojwa wa pumu. Kielelezo C inaonyesha muonekano wa njia ya hewa wakati dalili za pumu zimeanza.




CHANZO CHA PUMU
Chanzo cha pumu hakijulikani. Watafiti wanafikiri husababishwa na baadhi vinasaba vya kurithi na sababu za kimazingira zinazopelekea kusababisha pumu, mara nyingi hutokea kipindi cha utoto. Visababishi vya ugonjwa huu ni pamoja na;
  • Tabia ya kurithi kwa kuwa na aleji, inayojulikana kama atopy
  • Wazazi wenye pumu
  • Baadhi ya maambukizi kwenye mfumo wa hewa yaliyotokea kipindi cha utoto.
  • Kugusana na waathirika wa aleji mbalimbali zinazosambaa kwa mfumo wa hewa au kupata maambukizi ya baadhi ya virusi kipindi cha uchanga au utotoni wakati mfumo wa kinga ukijengeka.

DALILI
1. Kukohoa. Kukohoa kwa pumu mara nyingi ni kubaya wakati wa usiku au asubuhi sana, na kumfanya muhusika kushindwa kulala.

2. Mapigo moyo. Mapigo ya moyo yanayoenda kwa kasi hasa hutokea unapovuta hewa ndani.


3. Kifua Kubana. Unaweza kujisikia kama kitu ni kinakufinya au kukaa juu ya kifua chako.


4. Kushindwa kupumua. Baadhi ya watu walio na pumu wanasema hawawezi kupata pumzi zao au wanahisi hawapati pumzi kabisa. Unaweza kujisikia kama huwezi kupata hewa nje ya mapafu yako.


**Muhimu**
Si watu wote walio na pumu huwa na dalili hizi. Kadhalika, ukiwa na dalili hizi siku zote haina maana kwamba una pumu. Njia bora ya kutambua pumu ni kuhakiki utendaji kazi wa mapafu, historia ya matibabu (pamoja na aina na kutokea wa dalili), na kujaribu kufanya mazoezi ya viungo.

TIBA
Pumu haina tiba, Lengo la matibabu ya pumu ni kudhibiti ugonjwa huo. Njia bora za kudhibiti pumu ni pamoja na;

  • Kuzuia dalili sugu na zenye taabu, kama vile kukohoa na kushinwa kupumua
  • Kupunguza mahitaji ya madawa kwa ajili kupoza athari za ugonjwa huu
  • Jisaidie kudumisha utendaji kazi mzuri wa mapafu yako
  • Jitahidi kufwata ushauri wa daktari namna kudhibiti ugonjwa huu.
  • Kuepuka mambo ambayo yanaweza kuchochea ongezeko la ugonjwa. Hata hivyo, Kitu kingine ambacho unapaswa kufanya ni mazoezi ya viungo. Mazoezi ni sehemu muhimu ya maisha ya afya zetu. Ongea na daktari wako kuhusu madawa ambayo yanaweza kukusaidia kuwa salama wakati wote.
KUZUIA UGONJWA

Hakuna njia ya kuzuia pumu, lakini kwa kufanya kazi pamoja, wewe na daktari wako mnnaweza kubuni hatua kwa hatua mpango wa wewe mgonjwa kuishi na hali yako na kuzuia athari za pumu. Njia za kudhibiti ugonjwa huu ni pamoja na;

1. Kufuata mpango wako wa kudhibiti pumu. Wewe na daktari wako pamoja na timu ya huduma ya afya, lazima muandike mpango wa kina kwa ajili ya kutumia dawa na kusimamia mashambulizi ya pumu. Kisha kuwa na uhakika na kufuata mpango wako. Pumu ni hali inayoendelea ambayo inahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara na matibabu. Kufwata udhibiti wa matibabu yako inaweza kukufanya kuwa na hali nzuri na kudhibiti maisha yako kwa ujumla.


2. Kupata chanjo ya homa ya mafua na Homa ya mapafu. Kupata chanjo kunaweza kuzuia mafua na homa ya mapafu kuchochea ugonjwa wa pumu.


3. Kutambua na kuepuka vichochezi vya pumu. Aleji mbalimbali na vitu vingine kama vumbi, mbelewele, hewa ya baridi na hewa iliyochafuka huweza kusababisha ongzeko la pumu. Fahamu visababishi au vitu vinavyochochea pumu, na kuchukua hatua za kuepuka vichochezi hivyo.


4.Dhibiti pumzi yako. Unaweza kujifunza kutambua dalili zinazoelekea kwenye hali mbaya na ya hatari ya ugonjwa, kama vile kukohoa, Mapigo moyo au pumzi kupungua. Lakini kwa sababu utendaji kazi wa mapafu yako huweza kupungua kabla ya ishara au dalili, mara kwa mara pima na kurekodi kiwango cha juu kwa namna unavyopumua kwa kutumia peak flow meter(Kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini)




Tazama video hapo chini namna ya kutumia kifaa hiki




5. Kutambua na kutibu dalili mapema. Kama utachukua hatua za haraka, huwezi kupata athari kubwa za ugonjwa huu. Pia hutakua na haja ya kutumia dawa nyingi kudhibiti dalili zako.

6. Tumia dawa yako kama ulivyoagizwa. Ukiona unazidi kuwa na afya nzuri na ugonjwa wako umepungua kiasi fulani, usibadili jambo lolote bila kuongea na daktari wako kwanza. Ni muhimu kuwa na dawa zako kila mara unapomtembelea daktari, hivyo daktari wako atakufanyia uchunguzi na kukuelekeza matumizi sahihi ya dozi.

Chanzo: nhlbi.nih.gov & mayoclinic.org

** Tupe Maoni yako **




Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

1 تعليقات

  1. Maelezo mazuri sana tunaomba utafiti ufanyike kubaini Tiba ya pumu ( athima) ,tuokoe wengi tuishi wengi

    ردحذف

إرسال تعليق

أحدث أقدم