Kilimo cha Bamia - Sehemu ya Nne (Growing Okra - Part Four)


KILIMO CHA BAMIA - SEHEMU YA NNE

12. Semiloopers (Anomis flava) and Leafrollers (Haritalodes derigata)
Hawa ni aina ya viwavi wanaoharibu majani ya bamia. Aina zote hizi mbili huharibu majani ya bamia. Aina ya kwanza (Semiloopers), viwavi hawa hula na hutengeneza matundu kwenye majani, wengine hula sehemu ya chini ya majani na kuacha ngozi nyembamba ya juu ya jani kubakia (windowing).

Aina ya pili (Leafrollers), viwavi hawa huviringisha majani pamoja na kuanza kula majani, hatimae majani hujikunja na kudondoka. Viwavi wanaotoboa majani huleta athari sana kwenye mmea endapo watakua wengi hususani kwa mimea michanga.

Viwavi hawa wana rangi nyeupe inayong'aa au rangi ya njano mpauko lakini wanaweza kuonekana kama wana rangi ya kijani endapo wakila na kumeza majani ndani ya utumbo wao.


A: LEAFLOOPERS

Picha: Kipepeo wa kiwavi (Semiloopers)     Photo Credit: www.eagri.org

Picha: Kiwavi (Semiloopers)      Photo Credit: www.eagri.org

B: LEAFROLLER

 Picha: Kiwavi (Leafrollers)      Photo Credit: www.apnikheti.com


Namna ya kuwadhibiti
  • Pulizia dawa mbalimbali za asili zitokanazo na Mwarobaini, Pareto n.k au tumia dawa za kemikali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
  • Chunguza mara kwa mara uwepo wa viwavi hawa, kwa miche michanga unaweza ukawatoa kwa mkono kama shamba lako ni dogo.
13. Flower beetles (Mylabris spp. and Coryna spp.)
Hawa ni wadudu wanaokula maua ya bamia, hali hii husababisha uzalishaji wa matunda ya bamia kupungua kwa kiasi kikubwa, vilevile wadudu hawa hula majani na kubakiza makovu kwenye majani. Viwavi wa beetles hawa hawali mmea wa bamia bali hula mayai ya panzi, kwa hiyo viwavi hawa ni muhimu sana kwani huzibiti ongezeko la panzi Kibailojia (Biological Control)

Wadudu hawa(beetles) hutaga mayai kwenye udongo, mayai yakishaanguliwa hutengeneza viwavi. Viwavi hawa wanatembea sana kutafuta mayai ya panzi, Wadudu kamili (beetles) ni vigumu sana kuwadhibiti kwa sababu hawatulii sehemu moja wanatembea tembea sana. Kama beetles hawa wakiwa wachache, hawaleti athari sana kwenye mmea.

Picha: Flower beetle (Beetle wa maua)     Photo Credit: www.treknature.com


Namna ya kuwadhibiti
  • Tembelea na chunguza uwepo wa wadudu hawa shambani mara kwa mara.
  • Kama shamba lako ni dogo, wakusanye na watoe kwa mkono mara kwa mara kila unapowaona, hii itasaidia kupunguza idadi yao. Ingawaje usiwaondoe wote ila hakikisha wanabaki wa wachache. Vile vile unapokua unawashika hawa beetles hakikisha unavaa gloves kwa sababu wadudu hawa wakisumbuliwa hutoa majimaji yatakayoweza kuunguza ngozi.
  • Panda mazao mbadala yenye maua pembezoni mwa shamba
  • Pulizia dawa za asili zinazofukuza beetles hawa kama eucalyptus, lantana, kitunguu maji, kitunguu swaumu n.k. Namna ya kuchanganya dawa hizi za asili na maji fwata uwiano ufuatao;
* Changanya gramu 20 hadi 100 za mojawapo ya dawa hizo za asili kwa Lita moja (1) ya maji. Unachofanya unachukua kiasi cha majani makavu ya mojawapo ya dawa hizo, unayatwanga kisha unatumbukiza kwenye maji yanayochemka baadae unayaipua halafu uayaacha yapoe. Yakishapoa unayachuja halafu unapulizia mimea yako. Dawa hizi za asili zimeripotiwa kufukuza wadudu hawa shambani.

14. Bugs: Cotton stainers (Dysdercus spp.)
Wadudu hawa huvamia matunda ya bamia na kusababisha makovu na madoa madoa yenye rangi nyeusi. Bugs hawa mara nyingi huvamia bamia wakati mmea ukitoa matunda. Wanaharibu matunda na mbegu zake kwa kutoboa na kufyonza majimaji yenye chakula, kwa hali hii uzalishaji upungua kwa kiasi kikubwa. Mimea michanga iliyovamiwa hunyauka na kufa. Wakila kwenye matunda huharibu mbegu za matunda. Vilevile wadudu hawa huvamia zao la pamba, wadudu hawa wanakua na urefu wa mm 14 hadi mm 24.

Picha: Cotton stainers       Photo Credit: www.projectnoah.org

Picha: Cotton stainers       Photo Credit: www.entnemdept.ufl.edu

Picha: Cotton stainers adult (Mkubwa)    Photo Credit: www.wildsingapore.com

Namna ya kuwadhibiti
  • Wakati wa kulima lima vizuri kwa kina cha kutosha ili kuaacha mayai ya wadudu hawa peupe. Mayai yakiachwa peupe juu ya ardhi huharibiwa na Jua.
  • Baada ya kuvuna hakikisha una unang'oa mashina yote shambani na kuyachoma moto.
  • Majani ya Custard apple yanasaidia sana kuwadhibiti wadudu hawa.
  • Zuia uwepo wa wadudu hawa shambani kwa kutumia njia zifuatazo;
*Usafi wa shamba: Ondoa masalia yote shambani mara tu baada ya kuvuna.
* Hakikisha stoo ya kuhifadhia mazao yako inakuwa safi wakati wote.
* Kama shamba lako ni dogo, unaweza ukawakusanya kwa mkono halafu ukawaondoa shambani na kuwaua.
* Tumia kuku kupunguza wadudu hawa, kuku wana uwezo mkubwa wa kupunguza idadi ya wadudu hawa. Idadi ya kuku 15 wanatosha kuwaondoa wadudu hawa kwa eneo lenye ukubwa wa hekta 0.1 sawa na mita za mraba 1000 (1000m2) au Robo akari. Njia hii ni nzuri kama shamba lako ni dogo na likiwa karibu na nyumbani.
  • Tumia njia ya kibailogia kama kutumia wanyama au wadudu wengine wanaokula wadudu hawa kama; Assassin bugs, jamii fulani ya sisimizi au siafu (Ants), buibui, Ndege (kama kuku) na Parasitic flies.
  • Mti wa mbuyu ndio mahala pekee ambapo wadudu hawa huzaliana na kustawi vema. Kwa hiyo kama umepanda bamia zako au pamba karibu na mti wa mbuyu jalikisha unapulizia dawa za asili (Biopesticides) au zinginezo kama Pareto (Pyrethrm) n.k.
15. Bugs: Stink bugs (Nezara viridula, Atelocera sp. and Halydicoris sp.)
Hatua zote mbili za mdudu huyu (Adult na Nymphs) wanakula kwenye machipukizi, maua, matunda na mbegu za matunda. Wana urefu wa mm 6 - 15. Wakivamia matunda husababisha makovu yanayopelekea kuwepo kwa mibonyeo kwenye matunda, pia husababisha mmea kupukutisha matunda.

Picha: Stink bugs    Photo Credit: www.motherearthnews.com

Picha: Stink Bugs   Photo Credit: www.whatgrowsthere.com

Namna ya kuwadhibiti
  • Tumia dawa za asili kama Mwarobaini, unaweza ukatumia mazao yoyote ya mti huu kama majani, matawi, mbegu, au magome. Chakufanya; baada ya kuchuma au kuandaa mojawapo ya mazao haya, yaanike sehemu yenye kivuli mpaka yakauke, yakishakauka yatwange mpaka yawe unga, changanya na maji kiasi kulingana na uhitaji wako, alafu yachuje ili kuondoa makapi, kicha tumia pampu kupulizia.
  • Hakikisha unapulizia mchanganyiko huu wa mti mwarobaini nyakati za asubuhi, kipindi hiki huwa wapo juu ya majani.
  • Dawa zingine za asili unazoweza kuzitumia ni kama Pareto, lantana, Kitunguu swaumu (garlic), oleander, African marigold, blackjack, goat weed, wormseed n.k.

Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم