Hawa ni wadudu wadogo sana wenye
rangi nyeupe na wana mabawa wanapendelea kukaa chini ya majani. Wadudu hawa
wanaathiri mazao mbali mbali ya mbogamboga kama nyanya, maharage, bamia, n.k.
Hatua mbili za ukuaji wa mdudu
huyu kama Mdudu kamili mwenye mabawa na mdudu asiyekua na mabawa bado (Nymphs)
huathiri bamia kwa Kufyonza majimaji ya chakula kwenye mmea. Mmea ulioathirika
hupungukiwa kinga na hukauka, au hubadilika rangi kua njano na baadae hufa,
ikiwa wadudu hawa watazidi kuongezeka kwa muda mrefu. Mashambulizi ya wadudu
hawa huongezeka pale mmea unapopata tatizo la uhaba wa maji (Water stress).
Wadudu hawa hutoa uchafu kama
uteute ambao hutengeneza ukungu, Wakizaliana sana ukungu huo hutapakaa na
kufunika majani hatimae majani hubadilika rangi na kua meusi, hali hii hushusha
kasi ya utenengenezaji wa chakula (affecting Photosynthesis).
Picha: Whitefly wakiwa chini ya jani
Picha: Muonekano wa Whitefly kwa kutumia Hadubini
Picha: Muonekano wa Whitefly kwa kutumia Hadubini
- Wahifadhi wadudu rafiki wanaokula wadudu hawa kama Parasitic wasps na Predators (Wadudu wanaokula wadudu wenzao) kama Predatory mites, Lacewings na Ladybird beetles. Wadudu hawa huwadhibiti whiteflies pasipo kutumia dawa (Biological Control). Nimetumia lugha ya kingereza kueleza majina ya wadudu hawa kwa sababu sina maneno ya kiswahili yatakayoeleweka vizuri, ila tazama picha zifuatazo kuwatambua wadudu hawa.
A: PREDATORY MITES
Picha: Predatory mites wakiwa kwenye mmea
Picha: Muonekano wa Ptredatory mites akiwa amekamata mdudu
Picha: Muonekano wa Ptredatory mites akiwa amekamata mdudu
B: LACEWINGS
Picha: Lacewings
Picha: Lacewings akiwa juu ya mmea
Picha: Lacewings akila mdudu
- Tumia majani au matawi ya mti wa mwarobaini kudhibiti wadudu hawa (Chuma majani au matawi ya mti wa mwarobaini, Yatwange vizuri mpaka yalainike, Changanya na maji vizuri, Chuja na chujio kuondoa makapi na tumia pampu kupulizia), Maji ya mwarobaini (Neem extracts) husaidia kuzuia ukuaji wa hatua za awali za mdudu huyu, pia hufukuza Whitefly wakubwa na hupunguza kasi ya kutaga mayai.
- Pia Sabuni imeripotiwa kudhibiti wadudu hawa, kiasi cha sabuni kinachohitajika kuchanganywa na maji kitategemeana na aina ya sabuni.
- Kama umetumia njia nilizozieleza hapo juu na hujafanikiwa kudhibiti wadudu hawa, Tumia dawa za kemikali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
8. Root-Knot nematodes (Meloidogyne spp.)
Hawa ni minyoo wanaoishi kwenye udongo, wanaathiri mazao
yaliyomengi hususani jamii ya mbogamboga. Mara nyingi huathiri mimea
iliyopandwa kwenye udongo wenye ukichanga na mashamba yanayomwagiliwa kwa
mifereji. Mimea iliyoathiriwa hudumaa, huwa na rangi ya manjano na huwa na
tabia ya kunyauka wakati wa joto kali. Mizizi ya mimea iliyoathiriwa huwa na
vinundu vinundu.
Picha: Mayai ya minyoo hawa (Root Nematodes) Photo credit: www.clfs.umd.edu
Picha: Root nematode ukipenyeza kwenye mzizi wa bamia (Muonekano huu ni kwa kutumia Microscope/Hadubini) Photo Credit: www.mnn.com
Namna ya kuwadhibiti
- Tumia mbegu za bamia zinazovumilia athari za minyoo hawa.
- Badirisha mazao (Kilimo mzunguko), Panda mazao mengine tofauti na bamia kama Vitunguu, mahindi, Uwele, mtama, Ufuta n.k
- Dhibiti kiwango cha maozea ya mbolea za asili kwenye udongo kwa kuhakikisha udongo umechanganyika vizuri na maozea.
- Kama utaweza tafuta unga wa mashudu ya mwarobaini (neem cake powder) au unga wa majani au matawi ya mwarobaini, na uchanganye unga ule kwenye udongo. Mazao ya mti wa mwarobaini husaidia kuua minyoo hawa.
9. Aphids (Aphis gosspii) [Vidukali Mafuta]
Wadudu hawa ndio wanaoathiri sana zao la bamia, wanachofanya
wanafyonza majimaji ya chakula kwenye mmea, kupitia majani au mashina.
Wanasababisha uharibifu kwa kupunguza kinga ya mmea na kutoa majimaji
yanayonata (honeydew), majimaji hayo yanayonata hupelekea kuzaliwa kwa ukungu
ambao huathiri shughuli ya mmea kujitengenezea chakula chake (Photosynthesis).
Matunda ya bamia hukosa soko zuri yakiwa na wadudu (aphids), maji maji
yanayonata (honeydew), ngozi za aphids na ukungu uliotengenezwa na honey dew.
Wadudu hawa husambaza ugonjwa wa virusi unaoitwa Vein Mosaic
Virus (VMV). Ili ugonjwa huu usiwepo kwenye bamia wadhibiti wadudu hawa haraka
iwezekanavyo. Sio kwamba madhara ya wadudu hawa ni kusababisha ugonjwa huo wa
virusi tu, bali hudhoofisha kinga ya mmea pamoja na kupunguza uzalishaji.
Picha: Aphids kwenye tunda/ua la bamia Photo Credit: www.missouribotanicalgarden.org
Picha: Aphids wakiwa kwenye majani Photo Credit: www.watchmyfoodgrow.com
Picha: Muonekano wa aphids kwa kutumia Microscope (Hadubini) Photo Credit: www.buildsowgrow.com
Namna ya kuwadhibiti
- Wahifadhi wadudu rafiki wanaokula wadudu hawa kama Ladybird beetles, damsel bugs, Lacewings, hover fly, Ground beetles, Minute Pirate Bugs, Soldier Beetles na Spined Soldier Bug. Wadudu hawa ndio njia ya asili ya kudhibiti Vidukali mafuta (Biological control). REJEA HAPO JUU KUWAFAHAMU, Wadudu kama Ladybird beetles na Lacewings nimeshaweka picha zao hapo juu, Zifuatazo ni picha za wadudu wengine waliobaki;
A: DAMSEL BUGS
Picha: Damsel bug Photo Credit: www.goodhousekeeping.com
B: HOVER FLY
Picha: Hover fly Photo Credit: www.gardeningknowhow.com
C: GROUND BEETLES
Picha: Ground beetles Photo Credit: www.goodhousekeeping.com
D: MINUTE PIRATE BUGS
Picha: Minute Pirate Bugs Photo Credit: www.goodhousekeeping.com
E: SOLDIER BEETLES
Picha: Soldier beetle Photo Credit: www.goodhousekeeping.com
F: SPINED SOLDIER BUGS
Picha: Spined Soldier Bug Photo Credit: www.goodhousekeeping.com
- Tembelea shamba lako mara kwa mara ili kubaini kiwango cha uharibifu.
- Tumia dawa zitokanazo na mwarobaini (neem-based pesticides)[Botanicals] kama Achook (Azadirachtin 15% w/w), au neem extract (Azadirachtin 0.6 w/w). Dawa hizi za mwarobaini huua vidukali mafuta na huulinda mmea dhidi ya wadudu hawa kwa msimu mzima. Wakati wa kupulizia hakikisha unapulizia mimea pekee iliyo na wadudu (spot spraying).
- Pia unaweza kutumia dawa zingine za kemikali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
10. Flea beetles (Nistostra spp, Podagrica spp)
Hawa ni wadudu wanaovamia sana bamia. Ni wadudu wadogo sana
wana miguu ya nyuma mikubwa kuliko ya mbele, hali inayowasaidia kuruka umbali
mrefu pale ambapo watasumbuliwa kwa kuguswa. Rangi ya beetles hawa hutofautiana
kwa kuwa na rangi kati ya zifuatazo; Nyeusi, Kahawia, Nyeusi iliyochangamana na
njano au rangi ya blue iliyochangamana na kijani itategemeana na aina yao.
Beetle mkubwa anakula mbegu za matunda, mashina, na majani. Wanatengeneza
vishimo vidogodogo kwenye majani, Kiwavi wa beetles hawa huishi kwenye udongo
na hula mizizi ya bamia, lakini uharibifu huu wa mizizi hauna athari kwenye
uzalishaji wa bamia. Mara nyingi beetles hawa huathiri sana mimea michanga, pia
kama miche michanga ikiwa na beetles hawa wengi hunyauka na kufa na kama wapo
wachache mmea hudumaa.
Uharibifu wa beetles hawa kwenye mbegu za matunda na majani
machanga husababisha upotevu mkubwa wa uzalishaji, pia husababisha ukuaji
usiofanana shambani. Vile vile beetles hawa wakiwa wengi shambani huharibu maua
na matunda hali inayosababisha upotevu mkubwa wa uzalishaji. Pia matunda
yaliyoharibiwa na beetles hawa hukosa soko. Baadhi ya aina fulani za beetles
hawa, zimeripotiwa kusababisha ugonjwa wa virusi wa bamia (Okra Mosaic virus)
hasa kwa maeneo ya Afrika magharibi.
Picha: Flea beetle Photo Credit: www.gardeningknowhow.com
Picha: Flea beetle akiathiri tunda la bamia Photo Credit: www.infonet-biovision.org
- Tumia dawa mbalimbali za kemikali zinazopatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo, pia unaweza ukatumia zao la pareto (pyrerhrum extracts) kutibu wadudu hawa.
11. Leafmining flies (Liriomyza
spp.)
Mdudu kamili pamoja na kiwavi wake hula majani kwa kukwangua
ngozi ya juu ya majani ya bamia (Mining), hali hii huathiri kitendo cha mmea
kujitengenezea chakula chake (Photosynthesis) hatimae mmea kushindwa
kutengeneza maua na matunda. Wadudu hawa wakiwa wengi majani hukwanguliwa
kabisa (completely mined) hatimae majani hukauka na kuanguka yakiwa bado
machanga. Hali hii husababisha mmea kukosa nguvu na kudhoofu hatimae mmea
hunyauka.
Picha: Leafmining fly Photo Credit: www.extension.umn.edu
Picha: Leafmining fly Photo Credit: www.daf.qld.gov.au
- Chunguza mimea yako kila wakati ili kubaini uwepo wa wadudu hawa.
- Watunze wadudu wengine wanaokula wadudu hawa kama Parasitic wasps (Conserve natural enemies). Parasitic wasps huwadhibiti wadudu hawa kwa kiwango kikubwa.
- Tumia dawa za kemikali kuwadhibiti wadudu hawa, ila kama hautakua makini kwenye matumizi sahihi ya dawa hizi za kemikali, utaua wadudu rafiki wanaokula leafminer hatimae kutakua na ongezeko la kasi la leafminer.
- Tumia mazao mbalimbali ya mti wa mwarobaini kama majani, mbegu au matawi yake kudhibiti wadudu hawa (Spray Neem extracts).
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
إرسال تعليق