Inampasa mfugaji kuweka kiwango sahihi na sawia kwa kuku
wake katika kila hatua ya ukuaji
- Vifaranga wa kuku wamayai wanahitaji chakula kisichopungua gramu 60 kwa siku. Wskishamaliza kiasi hicho kinachotakiwa wapatie mboga za majani ili kuhakikisha wanakula wakati wote.
- Kuku wa mayai wanaotaga wanahitaji chakula kiasi cha Gramu 130 hadi 140 kwa siku.
- Kuku wadogo wa mayai wanaokaribia umri wa kutaga, inatakiwa wapewe chakula kiasi cha Gramu 60 kwa siku kwa muda wa miezi 2 na 1/2 na baadae wapatie chakula cha 'Layer mash' kwa kiwango cha Gramu 140 kwa siku. Pia kwa kuwaongezea lishe zaidi wapatie mboga mboga pamoja na mabaki ya matunda yaliyoliwa.
- Kuku wa nyama wanahitaji kiasi cha Gramu 67 kwa siku (Kwa aina zote za chakula yaani 'Broiler starter' na 'Broiler finisher') mpaka siku watakapofikia umri wa kuchinjwa (Siku 35 - 42)
ILANI:
Kuku wa aina zote (wa mayai au wa nyama) wanaathiriwa sana
na sumu kuvu itokanayo na chakula (aflatoxins). Sumu kuvu hii hutokana na
malighafi za chakula zilizooza kama mahindi wakati wa kutengeneza chakula.
Epuka kutumia mahindi yaliyooza wakati wa utengenezaji wa chakula cha kuku.
NI WAPI UTANUNUA MALIGHAFI ZA KUTENGENEZEA CHAKULA CHA KUKU?
Mfugaji anaweza kununua malighafi za kutengenezea vyakula
hivi kama nafaka mbalimbali, Pumba, unga wa samaki n.k kwa kuvipata maeneo ya
sokoni. Masoko mbalimbali makubwa nchini Tanzania huuza malighafi haya. Pia
kupata aina mbalimbali za pumba hupatikana kwenye mashine mbali mbali ya
kukoboa au kukamua mafuta ya alizeti kama unahitaji mashudu ya pamba au ya
alizeti.
Kwa mahitaji ya vionjo (additives) kama 'Pre-mixes', 'Amino
acids', Unga wa mifupa, chokaa n.k ambavyo ndio nyongeza ya virutubisho
mbalimbali na muhimu kwenye chakula cha kuku hupatika kwenye maduka ya kuuza
pembejeo za mifugo yanayopatikana maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
MAMBO MUHIMU NA YA KUZINGATIA WAKATI WA UTENGENEZAJI CHAKULA
CHA KUKU
Wakati wa kutengeneza chakula cha kuku ni muhimu kufanya
majaribio kwa kuwatenga baadhi ya kuku wachache. Kuku hao uliowatenga walishe
chakula hicho kwa muda fulani ili kuona matokeo ya ubora wa chalula chako. Kama
chakula chako ni kizuri kuku wa nyama watakua kwa kasi na kuku wa mayai
wataongeza uzalishaji wa mayai kwa ongezeko lisilopungua yai moja kila baada ya
masaa 27.
Nunua Samaki au Unga wa samaki
uliosagwa kutoka kwa wauzaji wanaozingatia ubora. Kama umepanga kutumia unga wa
samaki kwa kutengenezea chakula hakikisha una ubora wa kutosha, kwani inaweza
ikatokea ukanunua samaki au unga wa samaki uliochafuliwa au kuvunda. Unga wa samaki
uliochafuliwa ni hatari kwa afya ya kuku, Mfugaji anashauriwa kutumia Unga wa
soya kama atashindwa kupata Samaki au Unga wa samaki wenye ubora.
Kabla ya kuchanganya malighafi za
chakula cha kuku, changanya kwanza vionjo (additives) kama Amino acids, Premix,
n.k. ndipo umalizie kuchanganya malighafi zingine kama Mahindi, pumba za
mahindi, Unga wa samaki n.k.
Wakati kuchanganya chakula cha kuku, tumia madumu maalumu ya
kuchanganyia kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Chonde chonde usitumie
koleo au sepetu kuchanganya chakula cha kuku kwa sababu malighafi
hazitachanganyika vizuri.
Kama una swali, ushauri au maoni yoyote kuhusiana na makala hii,
usisite kuyaandika hapo chini. Karibu sana!. Tukutane tena kwenye makala
zijazo, Nakutakia siku njema.
<<< SEHEMU YA PILI
<<< SEHEMU YA PILI
*MWISHO WA MAKALA HII*
Kama una maoni au ushauri wowote kuhusiana na makala hii usisite kuacha maelezo yako hapo chini, Karibu sana!.
Ahsanteni sana pia unafanyaje au jinsi gani utaweka chakula mpak ujue kuku kala gram kadhaa
ردحذفtunaomba tupate maelezo ya kutosha kuusu kuchanganya na jinsi ya kuakikisha uyo kuku kala ujazo unaostaili
ردحذفMNAHUSIKA NA UUZAJI WA MALIGHAFI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU?NA MNAPATIKANA WAPI?
ردحذفumetajiwa malighafi tafuta kulingana na eneo ulipo....
حذفHatimae utakuja uliza unafanyafanyaje mpka kuku ale...
إرسال تعليق