Utaratibu wa Chanjo kwa vifaranga
ni Lazima, ili kuwafanya vifaranga wasikumbwe na magonjwa ya aina zote. Faida
kubwa za chanjo kwa Kuku ni kama ifuatavyo;
- Kuchanja kuku kwa wakati husaidia mwili wa kuku kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa.
- Kama ugonjwa umeingia, Idadi ya kuku watakaoathirika huwa ndogo sana
- Kuku watakao kufa kwa ajili ya ugonjwa huwa ni ndogo.
Kuna Chanjo za aina nyingi zinazotumiwa na kuku wa mayai
kama Marex, Ranikheth, Gumboro, Bruchaities, Bosonto,
Salmonela n.k.
ANGALIZO KABLA YA KUTOA CHANJO
Utoaji wa chanjo una taratibu zake, Inakupasa kuzifwata kwa
uangalifu taratibu hizo. Taratibu hizo ni kama ifuatavyo;
- Wakati wa kutoa chanjo washike kuku wako vizuri
- Wachanje kuku wako pasipo kutumia nguvu nyingi, washike taratibu.
- Usiwape chanjo kuku waliougua, wapatie kuku wenye afya tu.
- Fanya chanjo wakati wa hali ya hewa ya baridi (Cold weather condition)
- Baada ya kumaliza kufanya chanjo, osha vifaa vyako vyote na Maji ya moto au dawa za kutibu vifaa kutokana na vimelea vya magonjwa (germicide medicine/antiseptic)
KUTOA CHANJO
Utaratibu wa chanjo unatakiwa uwe
kama ifuayavyo kulingana na Umri wa kuku;
1. Chanjo ya Kideli (New Castle
Disease): Umri wa siku 7(wiki 1)
2. Chanjo ya Gumboro: Umri wa siku
14 (wiki 2)
3. Chanjo ya Fowl typhoid: Umri
wa wiki 9
4. Chanjo ya Fowl pox: Umri wa
wiki 18
5. Wiki ya 19 wapatie dawa ya
minyoo, inakua ni wiki moja kabla hawajaanza kutaga (Wanaanza kutaga wakifikia
umri wa wiki 20), baada ya hapo endelea kuwapa dawa za minyoo kila baada ya
miezi sita.
MAGONJWA MBALIMBALI YA KUKU WA
MAYAI NA NAMNA YA KUWADHIBITI
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ya
kuku wa mayai na kuku aina nyingine kama kuku wa nyama na wengineo;
1. TRUSH
Huu ni ugonjwa wa fangasi, husababishwa
na fangasi aina ya yeast (Candida
albicans). Huenezwa pale kuku wanapokula vyakula vilivyoota ukungu, pia
husambazwa zaidi pale wanapokunywa maji yaliyochafuliwa na fangasi.
Dalili za Ugonjwa
- Kuku wanazubaa na wanatulia sehemu moja pia wanakua na utando au vitu vigumugumu (Crusty) sehemu ya hajakubwa.
- Manyoya ya kuku yanakua rafu.
- Utaona majimaji mazito meupe ndani ya kifuko cha chakula cha kuku (Crop), Kifuko cha chakula cha kuku, kwa wale waliofuga kuku au kwa wale waliowahi kuchinja kuku, kifuko hicho cha chakula kipo katikati ya shingo na mwili wa kuku (sehemu ya kifua). Kifuko hiki cha chakula huonekana vizuri sana kama kuku ameshiba, huwa panavimba, sehemu hii huhifadhi chakula kabla ya kwenda kumeng'enywa.
- Kuku wanapata hamu ya kula sana isivyo kawaida.
Namna ya kuzuia na Matibabu
Ugonjwa huu hauna chanjo, ila una tiba, Tibu kuku wako kwa
kutumia dawa zinazoua vimelea vya Fangasi (Anti-fungal medicine) zinazopatikana
kwenye maduka ya dawa za mifugo. Ili kuzuia ugonjwa huu hakikisha unaondoa
vyakula vichafu na kuwapatia vyakula safi. Kumbuka kuosha vyombo vya chakula na
maji kila wakati.
2. AIR SAC DISEASE
Ugonjwa huu huathiri mfumo wa
upumuaji wa kuku, husababishwa na kimelea kinachoitwa Mycoplasma gallisepticum.
Dalili za Ugonjwa
- Kuku wanakua dhaifu na wanapunguza kutaga
- Siku zinavyozidi kwenda, kuku wanakohoa, wanapiga chafya, wanapumua kwa shida, wanavimba sehemu za maungio ya ya miguu au mabawa (swollen joints) na baadae wanakufa.
Photo Credit: www.poultrykeeper.com
Namna Unavyoenezwa
- Unaambukizwa baina ya kuku kupitia hewa au majimaji aliyotoa kuku kama kamasi n.k.
- Pia huambukizwa kutoka kwa ndege wa porini.
- Pia huambukizwa kutoka kwa Mama kuku kwenda kwa Kifaranga kupitia yai.
Namna ya kuzuia na Kutibu
Ugonjwa huu una chanjo na tiba,
Tibu kuku wako kwa kutumia dawa zinazoua au zinazozuia ukuaji na kuzaliana kwa
bakteria (Antibiotics) zinazopatikana kwenye maduka ya dawa za mifugo.
NB:
Kutokana na kwamba ugonjwa huu
huambukizwa baina kuku na kuku, yakupasa uwe makini sana na mchunguzi, chunguza
dalili hizo za kuku kwa makini, ili mara unapogundua ugonjwa huo uutibu haraka
na kwa ufanisi zaidi.
<<< SEHEMU YA KWANZA
<<< SEHEMU YA KWANZA
Makala na: Lusubilo Mwaijengo
إرسال تعليق