Kilimo bora cha Karanga - Sehemu ya Tatu (Growing Groundnuts - Part Three)


SEHEMU YA TATU

3. Millipedes (Peridontopyge spp.)
Hawa ni wadudu wa kwenye udongo, wanaitwa jongoo, wana rangi ya Kahawia (Brown) kwenda rangi nyeusi (Blackish), wadudu hawa ukiwagusa wanajikunja.

Millipede! flickr photo by slopjop shared under a Creative Commons (BY-SA) license


Athari
  • Wanavamia mashina ya karanga kuanzia kuchipua hadi umri wa siku 20 tangu kupanda. Wanakula mimea mara tu inapoota kutoka ardhini, mimea iliyoliwa na wadudu hawa hudumaa.
  • Vilevile wadudu hawa huvamia mimea iliyokomaa hususani kipindi cha kutengeneza matunda (Karanga) kwa kula na kuharibu maua.
Namna ya kudhibiti
  • Hakikisha usafi wa shamba
  • Andaa shamba lako vizuri
  • Shamba lako liwe mbali na maeneo ya misitu, kwani maeneo ya misitu ndo mahala pa kuzaliana wadudu hawa.
  • Fukia matunda ya karanga yanayoonekana juu ya ardhi.
  • Ziba mipasuko yote juu ya ardhi
  • Panda aina za mbegu zenye matunda yasiyoongezeka juu ya ardhi bali yanayotawanyika vizuri chini ya ardhi
4. Vidukari Mafuta [Aphids (Aphis craccivora)]
Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyeusi au kahawia, wanaumbile dogo sana wenye urefu kuanzia mm 1.5 hadi mm 2.0. Wadudu hawa hufyonza maji maji ya chakula yaliyopo kwenye kwenye mmea.

"Aphids" flickr photo by sankax shared under a Creative Commons (BY-NC) license

Athari
Wadudu hawa husambaza ugonjwa wa virusi wa karanga unaoitwa 'Rosette Virus disease'. Wadudu hawa husambaza virusi vya ugonjwa huu kwa kufyonza majimaji ya chakula kutoka mmea mmoja hadi mwingine

Namna ya kudhibiti
  • Panda mapema na kwa nafasi iliyokaribiana kiasi ili kudhibiti wadudu hawa. Faida za kupanda mapema na kwa nafasi iliyokaribiana ni kama ifuatayo;
  1. Kupanda mapema husaidia karanga kutoa maua mapema kabra ya kuvamiwa na wadudu hawa (Aphids).
  2. Kupanda kwa nafasi iliyokaribiana kiasi huweka kizuizi kwa wadudu hawa kushindwa kupenyeza na kusambaa ndani ya shamba kutoka pembezoni mwa shamba.
  • Chunguza na fwatilia ongezeko la wadudu hawa shambani, pia chunguza uwepo wa wadudu rafiki wanaokula wadudu hawa kama 'Ladybird beetle'.
  • Watunze wadudu rafiki hao pasipo kuwaua na viua sumu mbalimbali kwani husaidia kupunguza idadi ya wadudu waharibifu shambani
  • Tumia dawa za asili kama juisi ya mbegu au majani ya mwarobaini.
  • Usipande karanga au mimea jamii ya mikunde mfululizo kwenye shamba moja, badirisha mazao kwa kupanda mazao mengine tofauti na karanga au mimea jamii ya mikunde kama mahindi, mtama, ulezi na mimea jamii ya mafuta kama alizeti.
  • Panda aina ya karanga inayovumilia wadudu hawa.
5. Groundnut hopper (Hilda patruelis)
Wadudu hawa wanafanana na vipepeo wanaofikia urefu wa mm 5, wana rangi ya kahawia au kijani na alama nyeupe na michilizi kwenye mabawa. Vipepeo wadogo (Nymphs) hufanana na vipepeo wakubwa, isipokua wanakua hawana mabawa au wana mabawa yanayoanza kuota. Vipepeo hawa huishi kwenye makundi (Clusters or Colonies) na wanaongozana na sisimizi wanaokula unato unaotoka mwilini mwa panzi hao.

"Leaf hopper" flickr photo by DocJ96  shared under a Creative Commons (BY-NC) license

Athari
  • Wadudu hawa huvamia na kufyonza majimaji ya mmea kwenye mashina usawa wa ardhi au chini ya ardhi. Wakifyonza majimaji hayo huacha sumu inayosababisha mmea kuwa na rangi ya njano, kunyauka na kufa.
  • Udhibiti wa wadudu hawa unahitajika pale kunapokua na idadi kubwa ya wadudu hawa shambani.
  • Dalili mojawapo ya uwepo wa wadudu hawa shambani ni kuwepo kwa sisimizi weusi shambani.
Namna ya kudhibiti
Tumia aina ya mbegu zinazovumilia wadudu hawa.

6. Thrips (Megalurothrips sjostedti and Frankliniella schultzei)
Hawa ni wadudu wadogo wanaoathiri majani na maua ya karanga.


Athari
  • Maua yaliyoathiriwa na wadudu hawa hubadirika rangi na kua na alama, vikonyo vya maua huwa na rangi nyeusi.
  • Majani yaliyoathiriwa huwa na madoa yenye rangi ya njano upande wa juu wa jani, na upande wa chini wa jani huwa na mabaka mabaka yenye rangi ya kahawia (Brown).
  • Majani huongezeka unene na baadhi hujikunja.
  • Athari ikizidi majani machanga huharibika kwa kujikunja, pia majani hubadirika rangi na kua kijani mpauko, baadae mmea hudumaa.
Namna ya kudhibiti
  • Lima vizuri shamba lako kabla ya kupanda, hii itasaidia kupunguza idadi ya wadudu hawa kwa kuua Buu (Pupae) wa wadudu hawa ndani ya udongo.
  • Tumia dawa za asili kama Pareto, Mwarobaini, Rotenone na Vitunguu swaumu. Mchanganyiko wa vitunguu swaumu na pilipili kichaa umeonekana ukifanya vizuri kuua wadudu hawa.
NB:
Rotenone hutokana na mizizi ya mmea unaoitwa Derris elliptica, Derris elliptica ni mmea jamii ya mikunde unaotambaa, hupatikana  kusini mwa bara la Asia na visiwa vilivyopo kusini magharibi mwa bahari ya Pasifiki.



<<< SEHEMU YA PILI


Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم