SEHEMU YA TATU
5. Bugs (Coconut bugs, Helopeltis bugs, stink bugs)
Wadudu hawa wana rangi zifuatazo; Coconut bugs (Pseudotheraptus wayi) wakiwa wakubwa wana rangi ya kahawia na urefu wa mm 10 hadi 15. Wakiwa wadogo wana rangi nyekundu iliyochangamana na kahawia na wana antena ndefu. Wadudu hawa wakubwa kwa wadogo hula matunda madogo na makubwa na kusababisha michubuko ambayo baadae huwa makovu.;
Picha: Coconut bug
Helopeltis bugs pia huitwa mbu wa chai (tea mosquito) wana urefu wa mm 7 hadi 10, pia wana rangi tofauti kati ya madume na majike, dume wana rangi ya Kahawia au njano iliyochangamana na nyekundu, jike wana rangi nyekundu. Bugs hawa wanakula kwa kufyonza maeneo machanga ya mmea kama majani, mashina na matunda. Maeneo yaliyoliwa huwa na michubuko, majani yaliyoathirika huwa na michubuko na hudondoka na matunda huwa na mabaka meusi.
Picha: Helopeltis bugs
Stink bugs wana rangi ya kijani hadi kahawia au rangi nyekundu iliyochangamana na kahawia. wadudu hawa wakishtuliwa hutoa harufu mbaya, mara nyingi hula na kuharibu matunda machanga. Eneo la tunda lililoathirika huwa na makovu na husababisha matunda kuwa muonekano mbaya (km. kupinda, mabonde mabonde n.k)
Picha: Green Stink bugs Photo Credit: www.extension.umd.edu
Namna ya kudhibiti
- Wahifadhi wadudu rafiki wanaokula wadudu hao kama weaver ants, udhibiti wa viuatilifu hauna umuhimu sana kwani athari ya wadudu hawa ni ndogo sana.
Picha: Weaver ants
Howard Ensign Evans, Colorado State University, Bugwood.org
licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 License.
6. Spider mites (Oligonychus spp.)
Hawa ni wadudu wadogo sana wasioweza kuonekana kwa macho ya kawaida, pia huweza kutoonekana vizuri kwa lensi ya mkononi. Wana ukubwa wa mm 0.1 – 0.2 na huwa na rangi ya njano au nyekundu. Wadudu hawa hutengeneza utando kama buibui wa kawaida, huvamia majani na mtawi na kuanza kuyafyonza kwa ajili ya chakula chake.
Majani yaliyovamiwa hubadirika rangi na kujikunja na hatimae hudondoka, matawi hubadirika rangi na kuwa na makovu.
Picha: Spider mites
Namna ya kudhibiti
- Watunze wadudu rafiki kwa kutumia viuatilifu visivyoua wadudu wa aina zote (non-broadspecrtum insectcides).
- Pia unaweza ukaosha majani au matawi kwa kutumia maji yenye mgandamizo mkubwa, hii itazaidia kupunguza idadi yao.
B: MAGONJWA
1. Scab (Sphaceloma perseae)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya fangasi unaoathiri majani machanga, matawi machanga na matunda machanga, maeneo yaliyoathirika huwa na madoa madogomadogo meusi, baadae madoa haya huungana na kutengeneza makovu juu ya matunda na majani. Hali ya ugonjwa huongezeka kutokana na ongezeko la unyevu.
Picha: Scab
Cesar Calderon, Cesar Calderon Pathology Collection, USDA APHIS PPQ, Bugwood.org
licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 License.
Picha: Scab
Cesar Calderon, Cesar Calderon Pathology Collection, USDA APHIS PPQ, Bugwood.org
licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 License.
Picha: Scab kwenye majani
Florida Division of Plant Industry , Florida Department of Agriculture and Consumer Services, Bugwood.org
licensed under a Creative Commons Attribution-Noncommercial 3.0 License.
Namana ya kudhibiti
- Ondoa matawi au mjani yenye ugonjwa, kwani hutunza vimelea vya ugonjwa
- Ondoa matunda yaliyodondoka na kuoza shambani
- Tumia dawa za kutibu fangasi zenye madini ya Copper kama Blue Copper, Red Copper n.k, dawa hizi ziwekwe wakati matunda yanaanza na baada ya kuvuna.
2. Avocado root rot (Phytophthora cinnamomi)
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya fangasi aina ya Phytophthora cinnamomi, ugonjwa huu huathiri miparachichi ya umri wote, majani ya mti ulioathirika huwa madogo, na rangi ya kijani mpauko au njano, na mara nyingi hudondoka, hali hii husababisha mti kuwa nafasi nyingi zilizowazi kwenye matawi. Ugonjwa ukizidi matawi hufa, matunda hudumaa na kubakia madogo kwa hiyo uzalishaji hushuka kwa kiwango kikubwa.
Mizizi ya mparachichi hubadirika rangi na kuwa myeusi, huchakaa na kufa, mti ulioathirika hufa kabla ya wakati. Ugonjwa huu huathiri sana maeneo yenye mafuriko na udongo unaotwamisha maji, Vimelea vya ugonjwa huu husambaa kwa njia zifuatazo;
(a) Mbegu zilizotoka kwenye mmea ulioathirika
(b) Udongo wenye vimelea
(c) Miche michanga iliyoathirika
(d) Maji ya kumwagilia yenyevimelea vya ugonjwa huu.
Picha: Mizizi iliyoathiriwa na ugonjwa huu
Miti mingine inayoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na; Acacia, Camellia, Casuarina, Cypress, Eucalyptus na Grevillea, tazama picha hapo chini kufahamu aina ya miti hii. Kuna umuhimu sana kufahamu aina nyingine ya mimea inayoathirika na ugonjwa fulani, hii inasaidia kufahamu kama eneo lako linafaa au halifai kulingana na historia ya shamba lako kuhusiana na aina Fulani ya mimea yenye kuathiriwa na aina moja ya wadudu au magonjwa. Tazama picha zifuatazo kufahamu miti hiyo;
Picha: Mti wa Acacia
Picha: Mti wa Camellia
Picha: Majani na maua ya mti wa camellia
Picha: Mti wa cypress
Picha: Miti ya mikaratusi (eucalyptus)
Picha: Majani, maua na mbegu za mti wa makaratusi
Picha: Mti wa Grevillea
Picha: Majani na maua ya Grevillea
Namna ya kudhibiti
- Tumia mbegu zisizokua na magonjwa yaani zilizotoka kwenye mparachichi usiokua na ugonjwa huu
- Tibu mbegu zako kabla ya kuzipanda kwa kutumia maji ya moto (Hot water treatment), kwa kuziloweka kwenye maji ya moto yenye nyuzijoto 48ºC hadi 50ºC kwa dakika ishirini. Baada ya hapo haraka sana osha mbegu zako kwa maji masafi na ya baridi yanayotiririka na zianike mbegu zako kwa kuzisambaza juu ya turubai au sakafu safi kuepusha kugusana na udongo.
- Hakikisha udongo unaotumika kuandalia kitalu ni msafi yani usiotoka kwenye maeneo yenye ugonjwa huu, tumia udongo tifutifu wenye rutuba na na usiotwamisha maji.
- Panda aina ya mparachichi unaovumilia ugonjwa huu.
- Ondoa miti yote iliyoathirika shambani
- Epuka kuondosha udongo au maji kutoka maeneo yaliyoathirika kwenda kwenye maeneo yasiyoathirika.
- Wakati wa kuandaa shamba lima kwanza maeneo yasiyokua na ugonjwa halafu malizia maeneo yenye ugonjwa, hii itasaidia kuepusha kusambaza ugonjwa.
- Osha majembe ya kulimia na kuyakausha juani kila baada ya kuyatumia.
3. Anthracnose (Colletotrichum gloeosporioides)
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya fangasi aina ya Colletotrichum gloeosporioides, Athari za ugonjwa huu huonekana kwenye matunda baada ya kuvuna, wakati matunda yamekomaa. Vimelea vya ugonjwa huu huanza kwenye matunda wakati ni machanga, wakati huo vimelea hivyo huwa vimetulia pasipo kuleta athari yoyote. Athari huonekana wakati matunda yameiva, matunda huwa na madoa yaliyobonyea kwenye matunda, madoa hayo huwa yameoza, uozo huo hupenyenza mpaka sehemu ya ndani ya tunda.
Wakati wa kipindi cha joto madoa hayo hufunikwa na fangasi wenye rangi ya pinki, ugonjwa huu huenea zaidi kama mazingira ya stoo yana unyevu na joto. Vimelea wa fangasi wa ugonjwa huu huishi kwenye matawi, matunda yaliyooza yaliyoanguka na majani yaliyokufa au kukauka. Vimelea hawa huenezwa kwa michapo ya maji (water splash)
Picha: Anthracnose
Florida Division of Plant Industry , Florida Department of Agriculture and Consumer Services, Bugwood.org
licensed under a Creative Commons Attribution-Noncommercial 3.0 License.
Namna ya kudhibiti
- Ondoa matawi yaliyokufa kwani hutunza vimelea vya fangasi wa ugonjwa huu
- Ondoa matunda yaliyodondoka na kuoza shambani
- Tumia dawa za kutibu vimelea wa fangasi zenye madini ya copper kama Blue copper au Red copper kabla ya mmea kutoa maua, wakati wa utengenezwaji wa matunda na baada ya kuvuna.
4. Cercospora fruit spot (Pseudocercospora purpurea)
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea wa fangasi aina ya Pseudocercospora purpurea, ni tatizo sana kwa ubora wa matunda, vimelea hawa husababisha michilizi au madoa yenye rangi ya njano mpauko kwenye matunda na majani. Baadae madoa hayo huwa na rangi nyekundu iliyochangamana na kahawia, na hatimae huwa magumu na husababisha mpasuko kwenye matunda na majani. Ukali wa ugonjwa hutegemea msimu hadi msimu huweza kusababisha upotevu wa mavuno mpaka asilimia 60%. Ugonjwa huu huongezwa kasi na uwepo wa mazingira ya unyevu mwingi na joto kali. Vimelea wa ugonjwa huu husambazwa kwa michapo ya maji (water splash) na upepo.
Photo Credit: www.infonet-biovision.org Shared under a Creative Common Attribution license
Namna ya kudhibiti
- Ondoa matawi yaliyokufa kwani hutunza vimelea vya fangasi wa ugonjwa huu
- Ondoa matunda yaliyodondoka na kuoza shambani
- Tumia dawa za kutibu vimelea wa fangasi zenye madini ya copper kama Blue copper au Red copper kabla ya mmea kutoa maua, wakati wa utengenezwaji wa matunda na baada ya kuvuna.
MAVUNO
Mavuno ya mparachichi huanza baada ya miaka 3 - 4 tangu kupanda, itategemeana na aina ya mbegu na hali ya hewa, mara nyingi mavuno huwa tayari miezi 5 hadi 10 baada ya mparachichi kutoa maua. Mavuno mazuri huanza mwaka wa 6 na kuendelea, ni vigumu kusema muda gani maparachichi yanakuwa tayari kwa kuvunwa labda kwa aina ya maparachichi yanayobadirika rangi wakati yamekomaa. Ili kufahamu muda muafaka wa kuvuna vuna kiasi kidogo cha maparachichi alafu yaweke ndani ili yaive, ikiwa maparachichi yatalainika ndani ya siku 7 - 10 bila kubonyea mithiri ya kuoza basi matunda ya umri huo yanafaa kuvunwa.
Mti mmoja wa mparachichi uliotunzwa vizuri kwa mwaka wa 3 hadi wa 4 tangu kupanda huzalisha matunda kuanzia 300 hadi 500 kwa msimu, sawa na wastani wa matunda 400. Kwa ekari moja kunakua na wastani wa miti 100 sawa na matunda elfu arobaini (40,000) kwa ekari moja. Kuanzia mwaka wa 6 na kuendelea uzalishaji huongezeka hadi kufikia matunda 800 - 1000 kwa mti mmoja, sawa na matunda 80,000 - 100,000 kwa ekari moja.
Ili kufahamu uzito wa matunda yako unaweza ukakadiria kwa kufahamu wastani wa matunda mangapi yatakamilisha uzani wa kilo 1, Wastani wa matunda makubwa 2 hadi 3 yaliyojaa vizuri hukamilisha kilo 1 kwahiyo kama una matunda 400 kwa mti mmoja ni sawa na Kilo 130 (400/3). Pia kwa matunda madogo madogo manne (4) hukamilisha kilo 1 kwa hiyo kwa matunda 400 kwa mti mmoja ni sawa na kilo 100 (400/4).
Kama una maswali, maoni au ushauri wowote kuhusiana na makala hii, usisite kuacha ujumbe wako hapo chini, karibu sana!
** MWISHO WA MAKALA HII **
Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo
إرسال تعليق