Kilomo bora cha Maparachichi - Sehemu ya Pili (Growing Avocado - Part Two)


SEHEMU YA PILI

KUWEKA MBOLEA ZA ASILI
Mti wa parachichi unaweza kuzalisha kilo 250 – 300 za maparachichi kwa msimu mmoja wa mavuno, hali hii husababisha mahitaji makubwa ya virutubisho kutoka kwenye udongo. Kutambua kiasi sahihi cha mbolea kinachohitajika, inakupasa upime rutuba ya udongo kila mwaka. Kama kupima udongo itakuwia vigumu tumia muongozo ufuatao kutambua kiasi cha samadi kitakachowekwa kwa kila mti kama ifuatavyo;

Kama mkojo wa mnyama umekosekana unaweza ukatumia kinyesi cha kuku kwa kufwata muongozo ufuatao, lakini hakikisha unatandaza kinyesi hicho cha kuku mbali kidogo na shina la mti:

Ingawa utaweka mbolea nyingi za asili, mapungufu huweza kutokea kwenye miparachichi. Mara nyingi utaweza kuona mabadiliko ya rangi kwenye majani na matunda. Hali hii ni sababu ya ukosefu wa madini muhimu (Trace elements) kwenye udongo kama Zinc, Manganese, Iron, na Chroline. Kiwango cha upungufu huweza kupatikana baada ya kupima udongo maabara. Kama kupima udongo itakua changamoto unaweza ukatumia muongozo ufuatao;


KUPUNGUZA MATAWI
Kupunguzia matawi mapema husaidia kutengeneza muonekano mzuri wa mti, ingawaje matawi yatakayoondolewa ni yale yaliyozeeka au kufa na yenye wadudu au magonjwa.

WADUDU WAHARIBIFU NA MAGONJWA

A: WADUDU WAHARIBIFU
Zao la parachichi haliathiriwi sana na wadudu, wafuatao ni baadhi ya wadudu waharibifu wanaovamia zao hili;

1) False codling moth (Thaumatotibia leucotreta)
Hawa ni wadudu jamii ya vipepeo wenye rangi ya kahawia hadi kijivu na wenye mabawa yenye ukubwa wa mm 16 – 20. Wadudu hawa hupendelea kufanya shughuli zao wakati wa usiku. Jike la mdudu huyu hutaga yai moja kwenye tunda, baadae yai hilo huanguliwa na kua kiwavi ambaye hutoboa tunda na kuingia ndani. Kama mdudu huyu atataga yai lake kwenye tunda changa basi kiwavi huyo atakufa, kwa sababu kiwavi ataishi endapo yai litatagwa kwenye tunda linaloelekea kukomaa.

Kiwavi huyu akiwa mdogo anakua mweupe na kichwa chake huwa na rangi ya kahawia iliyofifia, akikomaa huwa na rangi ya pinki iliyochamana na wekundu. Kiwavi mkubwa huwa na urefu wa mm 15 hadi 20. Kiwavi huyu akikomaa hutoka kwenye tunda na hujificha kwenye udongo au majani yaliyopo ardhini na kuwa ‘pupa’ hii ni moja ya hatua ya ukuaji wa wadudu yaani; yai >> kiwavi >> pupa >> mdudu kamili. Kiwavi huyu huathiri matunda kwa kuyatoboa.

© Todd M. Gilligan and Marc E. Epstein, TortAI: Tortricids of Agricultural Importance, USDA APHIS PPQ, Bugwood.org
    Picha: False colding moth

© Tertia Grové, Institute for Tropical and Subtropical Crops, Bugwood.org
Picha: False colding moth

Namna ya kuwadhibiti
  • Hakikisha usafi wa shamba wakati wote
  • Hakikisha unayaondoa matunda yote yaliyoathiriwa (yaliyopo mtini na yaliyoanguka chini) mara kwa mara angalau mara mbili kwa wiki. Matunda hayo yaliyoathiriwa yafukie mbali na eneo la shamba kina cha sm 50 ardhini au yalifunike kwenye majaba yenye maji yaliyochanganywa na oil chafu. Acha matunda ndani ya jaba hilo kwa wiki moja. Vilevile mdudu huyu huathiri mazao mengine kama; mimea jamii jamii ya michungwa (citrus spp), pamba,mahindi, castor, chai, mapera (guava) na carambola fruits. Mimea mingine ni pamoja na mapera pori (wild guava plants), Oak trees na wild castor.
  • Kama athari bado ni kubwa ondoa mimea hiyo inayoweza kuwahifadhi tena wadudu hawa kama nilivyoiorozesha hapo juu. Au kama itakua ngumu kuiondoa unaweza ukahakikisha usafi wa shamba pia uhusishwe kwenye mimea hiyo.

2) Fruit flies (Ceratitis fasciventris)
Hawa ni wadudu wenye ukubwa wa mm 4.5 – 6, miili yao hung’aa huwa na rangi ya kahawia iliyochangamana na michirizi ya njano. Mabawa yake yana madoa madoa au huwa yamezungukwa na mistari ya njano na kahawia.

Miparachichi yenye matunda yenye gamba jembamba huathiriwa sana na wadudu hawa tofauti na ile aina yenye gamba nene. Wadudu hawa hutaga mayai ndani ya gamba la tunda liliokaribia kuiva au wengine hutaga mayai kwenye matunda machanga na yaliyokomaa.

Matunda yakifika ukubwa wa kati michilizi iliyozungukwa na utando mweupe huanza kuonekana kwenye matunda, kadiri tunda linavyoendelea kukua michilizi hiyo hubadilika na kuwa sehemu zilizokauka zenye mipasuko inayofanana na nyota.


Namna ya kudhibiti
  • Hakikisha usafi wa shamba
  • Chunguza mara kwa mara shamba lako ili kubaini wadudu hawa
  • Weka mtego wa kuwakamata wadudu hawa, mtego uwekwe mapema baada ya maua yaliyotengeneza matunda kufa. Wakati wa kuning'iniza mtego hakikisha hauvunji matawi. 

3) Scales [Soft scales (Coccus spp.); Armoured scales/coconut scale (Aspidiotus destructor)]
Hawa ni wadudu wadogo wasiotembea, wanakua mahala pamoja wenye rangi ya kahawia illiyochangamana na ukijani mara nyingi huonekana wakifyonza utomvu kwenye majani. Wadudu hawa (Soft scales) hutoa utomvu ambao husababisha uwepo wa fangasi kwenye majani, matawi na matunda. Utomvu huu hupendwa sana na sisimizi wadogo au wale wakubwa, kwa hiyo sisimizizi hawa ndio huwapa ulinzi wadudu hawa wasiliwe na wadudu wengine.

Aina nyingine ya wadudu hawa, Armoured scales kama coconut scale (Aspidiotus destructor) aina hii hawatoi utomvu bali wanatengeneza utando wa kutu kwenye matawi , majani na matunda. Wadudu hawa sio tatizo sana kwa miparachichi, ingawa tatizo huwa kubwa kwa miche michanga ambapo matawi machanga huweza kufa. Athari ya wadudu hawa kwa miti mikubwa ni pamoja na ngozi ya tunda kuharibiwa hali itakayopelekea sehemu ya ndani ya tunda kuharibika. Tatizo hili hupunguza ubora wa tunda na kukosa soko hususani kama utasafirisha nje ya nchi.




Namna ya kudhibiti
  • Wahifadhi wadudu rafiki wanaokula wadudu hawa kama parasitic wasps, ladybird beetles and lacewings (kwa kutokutumia dawa za kemikali zinazoangamiza wadudu aina zote ‘Broad spectrum insecticides)
  • Waangamize sisimizi wakubwa au wadogo kwa kutumia dawa isiyoangamiza wadudu aina zote (non-broad spectrum pesticides)
Wadudu rafiki

Picha: Parasitic Wasp (Nyigu)

Picha: Ladybird beetle

"Lacewing" flickr photo by jans canon  shared under a Creative Commons (BY) license
Picha: Lacewings

4) Thrips (mfano; thrips wa zao la chai mweusi ‘Heliothrips haemorrhoidalis’ na thrips mwekundu ‘Selenothrips rubrocinctus’)
Hawa ni wadudu wadogo wenye umbile bapa na urefu wa mm 1 – 2 na jora mbili za mabawa, wadudu hawa wakiwa hawajakomaa huwa na rangi ya njano na wakikomaa huwa na rangi ya kahawia au nyeusi

Wadudu hawa hawana athari sana kwa zao hili, ila huweza kusababisha majeraha kwenye majani na matunda, sehemu iliyoathiriwa huwa na rangi ya kijivu iliyochangamana na nyeupe na mara nyingi huwa alama za matone yenye rangi.

Kwenye matunda wadudu hawa hula kuanzia sehemu ya chini ya tunda na kutengeneza makovu na baadae makovu hayo huenea tunda zima. Wadudu hawa huathiri sana matunda machanga yenye urefu wa sm 2 (yenye umri wa wiki 2 hadi 3 baada ya kutengeneza tunda). Matunda yaliyokomaa huathiriwa kidogo sana na wadudu hawa na wakati mwingine hayaathiriwi kabisa.

© Lyle Buss, University of Florida, Bugwood.org
Picha: Thrips

Namna ya kudhibiti
  • Wahifadhi wadudu rafiki wanaokula wadudu hao kama lacewings na predatory bugs, udhibiti wa viuatilifu hauna umuhimu sana kwani athari ya wadudu hawa ni ndogo sana.


Makala na: Lusubilo A. Mwaijengo

Post a Comment

أحدث أقدم